Dj Majizo, Muasisi wa muziki wa Mchiriku, Mnanda, Singeli redioni!

Dj Majizo, Muasisi wa muziki wa Mchiriku, Mnanda, Singeli redioni!

Huyu kutwa kukimbizana na kina Lulu Insta halafu huo ubunifu atautoa wapi? It's only a matter of time before we see his radio station go down the drains. Huwezi ukaendesha biashara ya radio kwa uswahiliswahili. You got to have the needed talent.
Hahaha ujue unachekesha sana....hivi huu uzi una husu nini? Ambaye husikiliza E-FM anaweza kukushangaa...! Hata hivyo mbona hata wamiliki wa vituo vingine nao wanakimbiza tuu kama Majizzo! Lakini ninacho jiuliza unaumia nini?
 
ndo wale kwenye show wavulana hucheza wameinama na kuachia saburi juu ?
 
Hata gigi mahela anakikubali kisingeli...PolePole...chini bahariaaaaa

 
Aisee kweli hata mimi huu muziki nimetokea kuupenda sana yaani dah huwa nikisikiliza nafurahi sana. Jamaa wana maneno balaa afu yanachekesha kinoma.
Na huu ndiyo muziki halisi wa kitanzania ambao unaweza kututambulisha kimataifa. Na siyo vionjo vya kisauzi au kinaijeria tena.
 
Skide a.k.a Mtoto wa mama shamte! Ni hatari hata usipo zipiga kwenye radio watazipiga kwenye bodaboda
Skide ana ngoma yake inaitwa mbagala ni nomaaa. Sharobaro wa kwanza kuvaa singlendi ya mikono mirefu
 
Man Fongo sio mtu mzuri kabisa, ngoma zake zote ni hatari tupu. Pale TEKENYA, kule HAUNA, hapa HAINAGA USHEMEJI. huyu mtu aachwe kama alivyo aisee
 
Teh zile style zao za kucheza sasa, Shurti uwe na miguu mizima
C.c Kaboom, Benny, Raimundo

Aisee mi siku moja nitajitoa ufahamu niende show hata moja ya kina Msaga Sumu, kuna dogo MC Sudi (aliimba wimbo wa Naipenda Simba), Man Fongo, Dogo Side Mtoto wa mama Shamte (aliimba kabla hajatoka Dayamondi, na hii ya sasa Huku Kwetu Mbagalaaaa), noma.

Kuna wimbo mmoja siukumbuki kitu kama Mambo ya Mtaa wa Kongo, jamaa kapanda gari kutoka Gongo la Mboto, kufika mtaa wa Kongo akalizwa hadi nauli.
 
Hahaha ujue no achekesha sana....hivi huu uzi una husu nini? Ambaye husikiliza E-FM anaweza kukushangaa...! Hata hivyo mbona hata wamiliki wa vituo vingine nao wanakimbiza tuu kama Majizzo! Lakini ninacho jiuliza unaumia nini?
Nimegundua hujanielewa point. Nilichokuwa
najaribu kusema Majizzo ni mmoja wa vijana
wenye uwezo mkubwa sana kwenye tasnia ya media lakini nahisi hajatumia uwezo wake to the maximum
 
Mashabiki wengi wa singeli ni wahuni wa mtaani wavuta bangi na wabwia unga.
Majizzo naona kaamua kuwapa shavu "wateja wake" as per mange's dot dot.....
Huyo ataendelea kuponda tu wakati mwenzake pochi inavimba, anaingiza mavumba kwa kuipatia untapped market.
 
Huko uswazi sasa... wahuni wanataka nyimbo za singeli mwanzo mwisho kwenye vigodoro!
Sumu jichanganye uweke track za majuu wanateleza na spika n.k....
 
Huyo Majizzo inabidi muwe mnampa ushauri halisi. Mkiishia kumsifia atajaa kichwa na kujiiona kashafika. Radio yake ilitakiwa ilete changamoto halisi kwa radio zilizopo, lakini hili silioni zaidi hivyo visingeli. Visingeli itafika kipindi vitapoteza umaarufu. Sasa sijui atahamia kwenye reggae? Awe mbunifu apunguze ukilaza
*visingeli ndio mziki unaokuja kasi Tanzania, mark my words
 
Aisee mi siku moja nitajitoa ufahamu niende show hata moja ya kina Msaga Sumu, kuna dogo MC Sudi (aliimba wimbo wa Naipenda Simba), Man Fongo, Dogo Side Mtoto wa mama Shamte (aliimba kabla hajatoka Dayamondi, na hii ya sasa Huku Kwetu Mbagalaaaa), noma.

Kuna wimbo mmoja siukumbuki kitu kama Mambo ya Mtaa wa Kongo, jamaa kapanda gari kutoka Gongo la Mboto, kufika mtaa wa Kongo akalizwa hadi nauli.
Hahah siku moja jitoe tu kwa kweli, utaenjoy na roho yako
 
Back
Top Bottom