TANZIA DJ Steve B afariki dunia

Kwa nini alitoka clouds media?
Bora hayo tuyaache ndugu yangu. Kikubwa wampe heshima kama moja ya icon wa ile radio.

Baada Boniluv kuachana na Clouds upande wa Djz ni kama kulipoa sana hadi walipomchomoa DJ Steve B kutoka E.A Radio. Alileta vibe mpya kabisa kwenye kipindi cha Dr Beat.

Ukimtoa Boniluv pale clouds hakuna Dj aliye influence madj wengi kutamani kufanya kazi na Clouds kama DJ Steve B.
 
Bora hizi pombe za ngano kuliko spirits, spirits zinachoma kabisa.

Visungura na Double Kick vitaleta balaa kwa vijana wengi sana miaka 10 inayokuja

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
Hizo pombe chafu ndio hatari,ila kama unakunywa gin au whisky unamix na barafu mbona hazina shida,baba yangu kanywa whisky n gin zaidi ya 40yrz hakuwahi kua na shida ya figo...unatakiwa unywe maji mengi sana unapokunywa pombe kali
 
Ni kweli kabisa figo ni balaa sana hta Jasiri Mwongoza Njia alisanda na tulipitishiwa bakuli na kuchangia
 
Yaani mtu alieleta impact Clouds media,sasa ilikuwaje akaachwa. Any wa Apumzike kwa amani.Binafsi sikuwahi kumsikia as huwa sisikilizi musics huko clouds media.Mie ni taarifa ya habari na wakati mwingine kiduchu ninasikiliza michezo.
 
Ni kweli kabisa
 
Aliacha kazi mwenyewe,alipiga mshindo akaamua kununua vifaa vya muziki na kujitegemea
 
Dj skills alipata mgawao wa hela toka kwao,akaamua kujiajiri kwa kununua vifaa vya muziki, na kuamua kutoka clouds fm
 
Dj skills alipata mgawao wa hela toka kwao,akaamua kujiajiri kwa kununua vifaa vya muziki, na kuamua kutoka clouds fm
Nilikuwa shabiki wa test za mixing na playlist zake. Baada ya Dj John Dilinga kuacha radio yeye ndio alibakia kuwa na test tofauti. Siku hizi bila jingle wanaweza kupiga madj hata watatu usijue ni akina nani sababu wanafanana sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…