TANZIA DJ Steve B afariki dunia

TANZIA DJ Steve B afariki dunia

Moja kati ya Ma-DJ ambao waliowahi kufanya vizuri katika muziki wa Bongo Flava hapa nchini akifanya kazi Clouds FM Radio, Steve Mdoe a.k.a "DJ Steve B" "DJ Skills" amefariki dunia jioni ya leo Julai 31, 2023 katika Hospitali ya Muhimbili Mloganzila alipokuwa akipatiwa matibabu.

Kwa muda mrefu DJ Steve B alikuwa akiugua maradhi ya Figo.

Inna lillahi wa inna ilayhi rajiun.

UPDATES:
Zoezi la kutoa Heshima za mwisho zinatarajiwa kufanyika katika viwanja vya Leaders Club, jijini Dar es Salaam
Jumamosi tarehe 05/08/2023.

Mazishi yanatarajiwa kufanyika siku hiyohiyo ya Jumamosi tarehe 05/08/2023 kwenye Makaburi ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam.

=============

Steven Mdoe maarufu kama DJ Steve B amefariki dunia leo katika Hospitalini ya Mloganzila jijini Dar es salaam huku chanzo kikitajwa kuwa ni kupanda kwa Shinikizo la Damu.

Amstrong Mdoe ambaye ni Kaka wa Marehemu amesema kuwa Steve B ambaye alikuwa akisumbuliwa na figo toka mwaka 2019 alipelekwa Hospitali na kuwekwa Chumba cha Uangalizi Maalumu (ICU) baada ya Kupata Shinikizo la Juu la Damu na baadaye Shinikizo hilo lilipanda zaidi na kumsababishia kupoteza fahamu kwa siku tatu kabla ya kufariki.

"Steve B alipoteza fahamu kwa siku 3 ambapo jioni ya leo saa 10 akafariki, alikuwa na tatizo la Figo kwa miaka minne tangu 2019 lakini Figo sio chanzo cha Kifo chake, taratibu za mazishi bado tunazungumza tupange utaratibu lakini tunapokea rambirambi kwa namba 0678689383"

"Steve hakuwa na Mke wala hajaacha Mke na wala Mtoto, hatuna taarifa za Mtoto wake"
R. I. P, Steve B. DJ Skills.

Nimekumbuka moja ya wimbo iliyoupenda sana enzi izo
 
Attachments

  • Juelz Santana ft j. isaac - How I Roll_HIGH.mp4
    5.9 MB
Nilikuwa shabiki wa test za mixing na playlist zake. Baada ya Dj John Dilinga kuacha radio yeye ndio alibakia kuwa na test tofauti. Siku hizi bila jingle wanaweza kupiga madj hata watatu usijue ni akina nani sababu wanafanana sana.

MTAZAMO ni kweli ,kuna kipindi East Africa Radio kipindi cha The Crewz yaani akiwa DJ JD hata asipopiga Jingle unajua kabisa yupo mtamboni due to uniqueness zake za mixing.
 
Pombe zote tu sio nzuri🤣 j
Bora hizi pombe za ngano kuliko spirits, spirits zinachoma kabisa.

Visungura na Double Kick vitaleta balaa kwa vijana wengi sana miaka 10 inayokuja

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
Hizo za ngano mwisho wake ni kisukari tu. Utajaza tumbo mafuta mwisho wa siku ni diabetes 2.
 
Hizo pombe chafu ndio hatari,ila kama unakunywa gin au whisky unamix na barafu mbona hazina shida,baba yangu kanywa whisky n gin zaidi ya 40yrz hakuwahi kua na shida ya figo...unatakiwa unywe maji mengi sana unapokunywa pombe kali
Pombe ni mbaya ila hutu twa kuuzwa buku 2 ni hatari zaidi. Nakubaliana na wewe pombe inahitaji uwe mnywaji maji sana ili kuwa safe.
 
Moja kati ya Ma-DJ ambao waliowahi kufanya vizuri katika muziki wa Bongo Flava hapa nchini akifanya kazi Clouds FM Radio, Steve Mdoe a.k.a "DJ Steve B" "DJ Skills" amefariki dunia jioni ya leo Julai 31, 2023 katika Hospitali ya Muhimbili Mloganzila alipokuwa akipatiwa matibabu.

Kwa muda mrefu DJ Steve B alikuwa akiugua maradhi ya Figo.

Inna lillahi wa inna ilayhi rajiun.

UPDATES:
Zoezi la kutoa Heshima za mwisho zinatarajiwa kufanyika katika viwanja vya Leaders Club, jijini Dar es Salaam
Jumamosi tarehe 05/08/2023.

Mazishi yanatarajiwa kufanyika siku hiyohiyo ya Jumamosi tarehe 05/08/2023 kwenye Makaburi ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam.

=============

Steven Mdoe maarufu kama DJ Steve B amefariki dunia leo katika Hospitalini ya Mloganzila jijini Dar es salaam huku chanzo kikitajwa kuwa ni kupanda kwa Shinikizo la Damu.

Amstrong Mdoe ambaye ni Kaka wa Marehemu amesema kuwa Steve B ambaye alikuwa akisumbuliwa na figo toka mwaka 2019 alipelekwa Hospitali na kuwekwa Chumba cha Uangalizi Maalumu (ICU) baada ya Kupata Shinikizo la Juu la Damu na baadaye Shinikizo hilo lilipanda zaidi na kumsababishia kupoteza fahamu kwa siku tatu kabla ya kufariki.

"Steve B alipoteza fahamu kwa siku 3 ambapo jioni ya leo saa 10 akafariki, alikuwa na tatizo la Figo kwa miaka minne tangu 2019 lakini Figo sio chanzo cha Kifo chake, taratibu za mazishi bado tunazungumza tupange utaratibu lakini tunapokea rambirambi kwa namba 0678689383"

"Steve hakuwa na Mke wala hajaacha Mke na wala Mtoto, hatuna taarifa za Mtoto wake"

Rest well DJ Steve Bongofleva
 
Back
Top Bottom