Dk. Anna Makakala, utoaji Pasipoti kwa vijana wa Kitanzania unaambatana na fogery Kwasababu maafisa wako wanalazimisha watoto wetu kudanganya

Suluhisho kubwa ni kutenganishwa kwa wizara ya Home affirs na immigration services.

Nida madhumuni yake makubwa yalitakiwa yawe kama marekani Social security number id. Yaani mtoto akizaliwa anapata nida na hiyo inamsadia bila kuhangaika sijui baba yake nani na blah blah zingine anapata Passport.

Tanzania kwa fertility rate yetu na ongezeko la watu ni lazima kuwe na jitihada rasmi za kutoa raia wetu njee waende wakapate ajira na elimu na ujuzi ili tuendelee. Hili linaonekana sana Zimbabwe,Kenya,Ghana na Nigeria wanaweka mazingira rahisi kwa raia wao kutoka nje ya nchi yao kutafuta maisha. Wanaijeria wapo mpaka Namibia wamewekeza kwenye Sme lakini waliingia kama immigrants tuu.

Dhana ya ujamaa ndio inabana wananchi wasipate hata passport, rushwa inatawala kwenye uapataji wa pasi za kusafiria. Hapa ukienda ku renew passport watakutaka uende na mualiko au Hotel reservation ni mambo ya ajabu sana kutokea duniani yanatokea Kurasini. Sio kazi ya serikali kujua mwananchi anataka asafiri kwenda wapi kufanya nini. Yaani iko kama North Korea. Tuna tatizo kubwa la mindset na ushamba kwa wahusika. Naamini ujio wa Venus Nyota pale mjengoni kutasaidia mambo ya maana kama ya passport kuwa total online and electronic maana atashauri mambo ya duniani alikotembelea kwa Hangaya.
 
Watu ✅
Siasa Safi ❌
Ardhi ✅
Uongozi bora ❌

Tanzania 🇹🇿
 
Yaani ukisogelea swala la passport ni gumu utafikiri mtu sio mtanzania, utasikia ukifata process zote unapewa passport yako, pale ni pesa tuu ata with hours unapewa pass yako.
 
Na hv ninatarajia kwenda kupambania kupata passport, sijui itakuaje hukooooo
 
Sasa vijana wenye asili ya India, Waarabu, Wasomali na wengine wanahusika vipi na kero za kuomba pasi ya kusafiri Uhamiaji? Wao ndiyo wanafanya kazi Uhamiaji? Matatizo yenu mnalaumu wengine. Rushwa mnazopenda kuchukua mnalaumu wengine, kero za Uhamiaji mnalaumu wengine. Utafikiri hao "wageni" wasingekuwepo nchi hii ingekuwa kama Switzerland. Kweli vichwa vyenu mmejaza mawe badala ya akili.
 
Mtanzania Mwenye Kitambulisho cha Taifa ambacho habari zake zimo humo.
Apewe pasport yake bila kuzungushwa zungushwa.
Tena Tanzania ina waomba pasport wachache sana kuliko nchi nyingi sana za Kiafrika.

Tena basi wengi wanao omba passport ni wale wasio na asili ya Kitanzania.
Ndio maana Watanzania ni wachache sana katika nchi za wenzetu hasa Ulaya, Amerika na Asia.
Juzi kati zimetokea fulsa za Madereva wa Malori huko Canada na wamezitangaza sana.
Watanzani wameshindwa kuwania nafasi hizo kwa huu huu ukiritimba wa Passport.
Anaye taka kwenda nchi za nje tuwaachia Mabalozi wa nchi hizo wahakiki nia ya safari ya mtu wao watajua wamruhusu ama la.

Mtu ana kitambulisha cha Taifa unamwambiaje aanze kuthibitisha Uraia wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…