Kwa kuwa barabara hizo zimejengwa Tanzania na sio Burundi basi hakuna tatizo kabisa.
Yeyote atajayeleta hoja kama hii atakuwa ameishiwa, labda kama angekuwa anajenga barabara kwao tu, lakini Magufuli tumeshuhudia bajeti ya wizara yake anabalance pande zote za nchi.Miaka michache iliyopita waziri alivyokuwa Mramba nakumbuka wakati wa kipindi fulani alipeleka bajeti iliyojaa barabara za nyumbani kwake tu, ikaleta sana mgogoro bungeni.Kwa Magufuli sijawahi kusikia hiki.Yupo busy pande zote za nchi anahangaika na Barabara.
Kama tunachagua rais kwa record yake, basi hakuna kama Magufuli.Hao wengine tunaoona hawajakosea lolote serikalini kama akina Dr Slaa ni kwa sababu hawajawahi kuwa viongozi.
Tukiwajudge kwa uongozi wao ndani ya Chadema kuna uchafu mwingi kuliko uadilifu, na kama watu wanahoji taarifa ya CAG basi warejee pia taarifa hiyohiyo imesema kuwa Chadema mahesabu yao hayapo sawa, sasa tucoclude kuwa hiyi pesa Dr Slaa amekula?
Kuhusu nyumba, jana hiyo hoja imeelezwa kwa urefu sana na Sumaye, kaeleza mchakato mzima wa kufikia maamuzi yale,hakukuwa na uamuzi wa wizara, ilikuwa juu ya wizara.Maamuzi yale yalitokana na tume mbalimbali zilizoundwa na Rais, kwa miaka mingi tofautitofauti, na akasema kuwa uamuzi wa kuuza nyumba ulitolewa na Rais mwenyewe.
Ni muhimu tujitahidi kuwatendea watu haki.
Na ata kama Magufuli angekuwa amefanya uamuzi huo mwenyewe, bado yeye ni binadamu, hakuna mtu anayeweza kufanya maamuzi kwa miaka karibu 20 sasa serikali alafu asifanye ata moja la kukosea, ni binadamu sio malaika.Lazima kuna vitu binadamu atakosea, mpime kwa ujumla wake.Otherwise itabidi tuachane na wanadamu turudi misikitini na makanisani mpaka Mungu amshushe malaika mmoja aje kuwa Rais, maana kwa mwanadamu hayupo asiye na kosa ata moja.Hayupo!!