Dk. Jonh Pombe Magufuli achukua fomu kugombea urais wa Tanzania

Dk. Jonh Pombe Magufuli achukua fomu kugombea urais wa Tanzania

Makada wawania urais kupitia CCM wamiminika Dodoma kuchukua fomu.

Safari ya chama cha mapinduzi ya kupata mgombea wa urais katika uchaguzi mkuu ujao imeendelea kushika kasi baada ya makada sita wa chama hicho kuchukua fomu hii
leo na kufanya jumla ya makada 11 wa chama hicho kujitokeza ndani ya siku mbili tangu zoezi hilo lifunguliwe rasmi june tatu mwaka huu.

Miongoni mwa waliojitokeza kuchukua fomu hii leo ni pamoja na waziri mkuu mstaafu awamu ya tisa Mhe Edward Lowassa mbunge wa jimbo la Monduli ambaye amejinadi kuwa hana mpango wa kushindwa na amechoka na siasa za matusi na tuhuma na kudai kuwa hiyo sio demokrasia kwa viongozi wenye nia ya kweli ya kulikomboa taifa.

Mwingine ni aliyewahi kuwa waziri mkuu wa awamu ya nane Fredrick Sumaye ambaye amebainisha kuwa endapo atapata ridhaa ya chama hicho ya kuwania urais na kushinda atahakikisha anatokomeza kabisa tatizo sugu la rushwa kwa kuunda vyombo maalum ikiwemo mahakama ya wala rushwa huku akitumia rasilimali za asili zilizoko nchini kuinua uchumi wa watanzania.

Kada mwingine aliyejitokeza ni John Pombe Magufuli ambaye hivi sasa ni waziri wa ujenzi lakini pia amewahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini na ndani ya CCM kwa ufanisi wa hali ya juu ambaye yeye ametamba kipaumbele chake cha kwanza ni kutekeleza kwa vitendo ilani ya chama cha mapinduzi.

Makada wengine waliojitokeza ni makamu wa rais Dk Mohamed Gharib Bilal, balozi Ali Karume na mwanafunzi wa chuo kikuu cha Mzumbe Morogoro Amos Siyatenzi huku makada wengine zaidi wakitarajiwa kujitokeza katika muda ambao chama hicho kimeweka kuanzia June 3 mpaka Julai 2.

 
Hakuna bora wote ni wachafu hawafai bilioni 262 siyo pesa ndogo atuambie alizipeleka wapi kwanza?

Yaani ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa huyu jamaa anapendwa balaa na wananchi wa vijijini. Mambo ya nyumba za serikali hawana muda nao na hawataki kujua kwa sababu hayagusi maisha yao ya kila siku, vilevile ya CAG tunayajua sisi tu ila wananchi hawana time nayo.
Kama uamini ngoja jamaa atembee vijijini huwa ni maarufu kuliko waziri yeyote na hata rais ameshakutana na hali hiyo. Watu wanampenda Balaa.
 
Jambo usilolijua ni kama usiku wa giza huyu ripoti ya CAG imebaini bilioni 262 hajijulikani zimeenda wapi.

Iko wazi CAG ni mshirika wa team EL. Vipi mbona huzungumzii ufisadi wa chadema kwenye report ya CAG ?
 
Siwezi sikiliza rubish, nyuma zimeuzwa kwa usimamizi na ushauri wake. Kimadawake amepata nymba mwenge kabomoa kajenga Kebbys hotel, hivyo ndiyo wananchi wanajua na ndiyo ukweli wa hilo jambo

We kibaraka wa EL kaa kimya wewe....tuletee huo ushahidi..sio unaleta story za vijiweni na propaganda mnazotumwa kueneza baada ya kupokea mpunga kutoka kwa uncle E. Ongezeni bidii or else hizo pesa zitawatokea puani, nyama mkebe wee!
 
Huna hoja, sikiliza hapo mhusika mkuu, Waziri Mkuu, anaeleza walioshauri nyumba ziuzwe na aliyefanya uamuzi nyumba ziuzwe na kwanin nyumba ziliuzwa.

https://www.youtube.com/embed/LofQGOS0bCM?wmode=opaque

Hiyo hoja ya nyumba ameishaimaliza Sumaye jana, asubuhi na mapema!tafuteni nyingine!

Kaka asante sana kwa kuweka hiyo video clip...jamaa wamejitahidi sana kumaukumia Magufuli mzigo wa mavi kwa lengo la kumchafua...tutatumia hiyo clip na watanzania watajua ukweli!
 
Huyu jamaa kafanya madudu sana wizara ya Ujenzi, alitumia sana mabavu kupisha sheria na maamuzi, kwa mfano project nyingi amezipeleka sehemu ambayo hata siyo feasible. kwa mfano kuna feasibility study ilifanyika mwaka 2004. Study ilisema sehemu ya Kyamyorwa - Buzirayombo (120km) inayopita nyumbani kwa Magufuli (Chato) siyo feasible sehemu iliyokuwa feasible ni ya Usagara - Geita. Ila kwa ujeuri wake na kutojali fedha za walipa kodi alibadilisha maamuzi ili mradi upite nyumbani kwake. Sehemu ya kwake ilijengwa 2005, sehemu iliyokuwa feasible ilijengwa 2009. huo ni mfano mmoja tu wa madudu ya huyu jamaa, akipewa nchi si itakuwa balaaView attachment 257150View attachment 257151

Kwasasa Tanzania inahitaji rais mwenye elements zifuatazo
1) Msafi
2) Anayetumia mabavu

Chapter closed
 
BAADA YA KUSIKIA JUU YA MAGUFULI KAKIMBIA MBIO, NI NANI PPM??









PPM HUO UMASKINI WAKO UTAKUUA, YAAN LOWASSA KWA PESA ZAKE NDIO KAKUPA KAZI YA KUSHINDA KWENYE MTANDAO???nilitaka kushangaa ni nani huyu??kumbe kila unachoandika kwenye thread zote ni kwa maslahi ya LOWASSA.


Guys, muwe macho na watu kama PPM, watu wanalipwa humu na hawa mafisadi kuchafua watu.

PPM is racing against time! Ameshakula pesa na team EL haielekei kuchukua ushindi...hizo pesa atazitolea kupitia shimo la nyuma
 
Emma, kama huna ya kuongea kaa kimya, siku ya pili sasa huna hoja nyingine?kila sentesi mbili unarudia hayohayo.Grow!!

Achana na Emma..hiyo ni misukule imenunuliwa smartphones afu ikawa programmed kutoa jibu hilohilo kila baada ya dakika 5.
 
Back
Top Bottom