The Sunk Cost Fallacy
JF-Expert Member
- Dec 1, 2021
- 19,582
- 14,167
Makamu wa Rais, Dk. Philip Isdori Mpango amesema hajaridhishwa na kasi ya ujenzi wa mradi wa umeme wa Gridi ya Taifa katika Mkoa wa Katavi na kuiagiza Wizara ya Nishati kuhakikisha ifikapo 2023 mradi uwe umekamilika na hataki kusikia kiswahili wala kisingizio anataka Mkoa wa Katavi uwe umeunganishwa na umeme.
“Oktoba 2023 sitaki Kiswahili, sitaki kisingizio Mkoa wa Katavi uwe umeunganishwa na Gridi ya Taifa nafikiri tumeelewana, napenda niseme kwa uwazi kabisa sijaridhishwa na kasi ya ujenzi wa huu mradi wananchi wa wa Katavi wamesubiri umeme muda mrefu” amesema Dk. Mpango
SOURCE: ITV
Safi ,huku ndio kumsaidia Rais sio kuwa VP wa matamasha na sijui kutumwa hapana..
Wakisingua hao Waziri atasogeza file kwa Maza kupitisha wino mwekundu..