Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi amewataka Wanasiasa Nchini kutumia vizuri ndimi zao na kamwe wasitoe matamshi ambayo yanaweza kuhatarisha amani na utulivu.
Balozi Dk. Nchimbi ameyasema hayo jana August 13, 2024 alipokua akiongea na Wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Uwanja, Geita Mjini.
Balozi Nchimbi amesema Wanasiasa wasijisahau katika kuchagua maneno yanayoweza kuhatarisha amani ya Tanzania na kuongeza kuwa wako Watu wanajisahau, hivyo amewaomba Watanzania wasijisahau.