Dkt. Abbas na Abdul Nondo watofautiana namna watoto wa kike wanaopata mimba shuleni watakavyoendelea na masomo

Kiitifaki, huyo bwana mdogo alitakiwa akutanishwe na Mwenyekiti wa UVCCM; Katibu Mkuu ni nafasi kubwa katika Utumishi wa Umma; waandaji wa kipindi hawajatenda haki kwa Katibu Mkuu.

Katika mjadala huu, kwa kushirikiana na Benki ya Dunia, baadhi ya wanaharakati, asasi za kiraia na wapinzani wanakusudia kuhujumu elimu yetu na maendeleo endelevu ya taifa kwa ujumla.
Katika hili, msimamo wa serikali uungwe mkono.
 
data

mkuu, una binti nyumbani kwako ?
alafu mbona hata hawa wanaosoma mfumo rasmi wanabeba sana mimba na wanazitoa, kuna jamaa yangu tulipokuwa high school demu wake alitoa mimba 3
hili swala mnabidi mtoe maamuzi like parents,


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa ukiona mtu kama Sarungi na Fatuma Karume wanavyojishaua na wengine kule twitter huwa nashangaa sana!

Alafu mtu kama Zitto tulifikiri msomi atoe mawazo chanya kwa jamii lakini lenyewe lipo tu kutetea ujinga halina tofauti kabisa na ccm

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hao wote wanasimamia misimamo ya maboss zao, suala la hizo pesa ni la kimkataba na sio zawadi Tz tumekubali masharti you tuliyopewa na WB kuhusiana na wanafunzi wenye mimba kurudi kusoma ktk mfumo rasmi au usio rasmi, kinachosema kwenye mkataba ndicho kitafuatwa na sio maneno ya Hawa wanaosifu mabwana zao bila kuangalia uhalisia was mkataba.
 
Duh......!
 
Akalee mtoto... Mtoto akikua naye atakua amekua.. Atachagua mfumo atao ona unafaa akajiendeleze. Ipo mingi...
 
Dogo kinachombeba ni upande aliopo wala si hoja zake
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu tunaongea kana kwamba Watoto wa kike ni jamii kutoka sayari nyingine.

Hizo mimba wanapewa na kina nani?

Kwa nini mnataka wakishapata mimba waingizwe kwenye kundi tofauti kabisa na jamii? kana kwamba wameshatoka kwenye ubinaadamu wa kawaida na sasa wao hawafai tena.

Ningetamani sana nao wabaki na heshima ile ile hata baada ya kupata mimba na kujifungua. Kama tuliwaheshimu awali sioni kwa nini tuwapotezee heshima hiyo baada ya kuzaa.

Kwa upande mmoja tutajifanya ni jamii yenye kumuheshimu Mwanamke na upande mwingine tunamnyanyapaa Mwanamke huyo huyo kwa kisingizio cha kuzaa mapema, ili hali aliyempa mimba ni huyo huyo Mwanaume.

Hizi vita na mabavu yetu dhidi ya Mabinti hawa Wadogo, ni bora tungeelekeza kwenye kuhakikisha Wanaume Mabazazi hawawapi Mabinti hawa hizo mimba.

Tuheshimu Wanawake na tuheshimu karama yao ya uzazi...Mama ni Mama hata kama alikuzaa akiwa anasoma, tena wapo wanaoongea hovyo ili hali nao wamezaliwa na Mama aliyekuwa bado anasoma.
 
Kweli kabisa maana dogo kapwaya sana, alikuwa anaongea kama amekaririshwa maneno na ZZK. Alikua anag'ag'ana tu ubaguzi ubaguzi. Haangalii hata hoja ya msingi kama mwanafunzi anatakiwa asome katika mazingira ya saikolojia nzuri,sio mazingira yanayompa fikra kuwa ngono na mimba ni jambo la kawaida.
 
Hizo nafasi tu, hata Waitara ni N/waziri lakini huwezi mweka meza Mona na Nondo kihoja.
 
Watoto wa kike hawatakiw kusamehewa hata kidogo wanafanya makusudi
Wewe ni mojawao?Umefahamuje ni makusudi wanafanya?Huwa wanabebeshwa mimba kama ndoo ya Maji?Hukumu ya wanaowapa ujauzito nayo iwe kuhasiwa,maana hiyo ndiyo angalau italingana na hukumu Kali ya kifungo cha ujinga kwa maisha yao yote.
Tuwe fair,tutafute namna ya kuwahakikishia wasichana hawapati ujauzito,wanaowabebeaha ujauzito wapewe adhabu itakayotoa funzo kwa wanaotarajia kujihusisha na wanafunzi kingono(wabakaji) badala ya kuwahukumu wahanga.
 
Bodi ya mikopo Kama umesoma private o level mkopo utausikia kwa jirani
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…