Dkt. Abbas na Abdul Nondo watofautiana namna watoto wa kike wanaopata mimba shuleni watakavyoendelea na masomo

Dkt. Abbas na Abdul Nondo watofautiana namna watoto wa kike wanaopata mimba shuleni watakavyoendelea na masomo

Ndugu sidhani kama katika hili kuna U CCM na Upinzani, ni swala la Cultural and values za jamii yetu.

Hili sio swala la Mh. Rais wala CCM, ni swala sheria za nchi toka awali.

Kama umepita pita kwenye sekta ya elimu unaweza ukawa na mtizamo tofauti na hisia zako.

Sheria za shule, miongozo inayotolewa kuhusu mimba mashuleni ikiwa ni pamoja kitabu cha Kiongozi cha Mkuu wa Shule na Vyuo (1997) kilichotolewa na Wizara ya Elimu na Utamaduni zinasema wazi wazi makosa yanayoweza kumfukuzisha shule mwanafunzi ni pamoja KUMPA MTU MIMBA au Kupata Mimba wala si swala lililoasisiwa na JPM wala CCM ni swala la sheria za nchi.


Kama kutakuwa na mapungufu basi ni swala la wizara husika kurekebisha na si kumbebesha mtu au chama flani.

Umeuliza kama "tumepima madhara kama akirejea darasani ikishakaa na ananyonyesha" kutakuwa na madhara gani. Ni vema ukatambua kwamba sheria zinapotungwa zinakuwa zimezingagia si tu Falsafa inayoongoza nchi katika eneo hilo Bali pia huwa utafiti wa kina umefanyika. Je unaweza kumuadhibu mama mwenye kichanga cha miezi mitatu pale anapokosea kama ukiwa mwalimu?...he unajua atapata utulivu upi darasani wa kuzingatia masomo akiamua mume wake, mtoto na cha kumnyonyesha mwanae?...sasa kwa nini tusiwaruhusu wazee na wabibi waliokosa elimu kusoma katika madarasa ya kawaida na bint yako ambaye hajavunja ungo darasa moja?....he unajua umuhimu wa Peter peer grps katika kusoma?

Namba tatu unauliza vipi kwa mwanafunzi mwenzake aliyempa mimba? ...he unajua juvenile court unakazi gani?

Kifupi huna hoja.
Hujataka tu kuzitambua hoja zangu!
1.Rejea ilani ya CCM 2015,Pia rejea hotuba ya Mama Samia suluhu akiwa huki kaskazini akizungumza jukwaani kuwa serikali itawapa fursa watoto watakaozaa kurudi shuleni na baada ya kauli hiyo ndipo JPM akatoka hadharani na kusema kwenye serikali yake hatasomesha mtoti atakaye zaa!So hiyo ni yake!
2.Unazungumzia Juvenile court lakini hapo ni ni kwa criminal case!Mtoto wa miaka 15 kumpa mimba mtoto wa miaka 15 unasema wa kiume anapelekwa juvenile court na wa kike anafukuzwa shule,hapa huna hoja maana hakuna criminal case hapo!Hakuna kosa la kumpa mtu mimba bali kuna makosa kama kumbaka mtu!Sasa watoto wamekubaliana,wakafanya ngono na mmoja akapata ujauzito,hapo hakuba ubakaji!Ubaki unatoke kwa namna hizi tu
-Mtu mzima kufanya mapenzi na mtoto!
-Kufanya mapenzi na mtu bila ridhaa yake!
So kwenye pointi hiyo huna hoja!

3.Eti tukiruhusu watoto waliojifungua unasema basi vikongwe warudi kusoma na watoto maana ni kitu hicho hicho!
Hivi mtoto akipewa mimba ndio umri unaongezeka na anakuwa mtu mzima?Mtoto akibakwa na ikapelekea kupata mimba akijifungua akiwa na miaka 12,baadaye na mimi mtu mwenye miaka 30 nikamtongoza binti huyo akiwa na miaka 13,nikafanya naye ngono,nakuwa sijambaka kwa scenario yako ya kujifungua tayari ni mtu mzima??Mbona sheria inamtambua mtoto kwa umri na sio kama amezaa au la?
4.Huko nyuma mabinti ambao walikuwa wakijifungua,kama wazazi wanauwezo walikuwa wanafanya mpango na akijifungua anaenda kusoma shule nyingine,na wengi tumewaona wanaweza kuwa mashuhuda!
5.Hoja ya kwamba itakuwa ngumu kumuadhibu nayo ni mfu!Anaweza kuadhibiwa vizuri tu kutokana na kosa alilotenda lakini kuna mazingira akasamehewa bila wenzake kujua!Mfano hakumaliza honework,unaweza kumwita ofisini na kumwuliza kwanini, labda akakueleza kuwa mtoto alikuwa anaumwa basi unamwelewa kutokana na mzigo alionao!Kuna watoto wengi tu wenye matatizo mbalimbali na wanapewa excuse kwenye baadhi ya mambo,sio lazima wenzake wajue!Nayasema haya kwasababu nimeona baadhi ya cases!
6.Nimekupa mfano wa Kenya na Uganda,tungeenda kujifunza huko pengine tungepata kitu!
Tamaduni hubadilika kulingana na wakati!Mfano kwenye makabila mbalimbali mtoto wa kike alikuwa hapaswi kwenda shule,kwingine ilikuwa wanakeketwa wasiwe malaya,kwingine hawakuruhusiwa kula baadhi ya vyakula NK!Mambo yamebadilika sana,hatupaswi kuwa sehemu ya kutengeneza wajinga bali kuwakomboa!Huko katika mfumo usio rasmi ni kwa kupunguzia ujinga tu,ni dumping area!

Narudia,sijaona sababu yoyote significant ya kumzuia mtoto wa kike kurudi shule kama ikitokea akajifungua!
 
Ndugu yangu hawatakuelewa hata kidogo. Wao na JPM wao! Wangekuwa wanaunga mkono maagizo ya Mungu hivyo hii nchi ingekuwa ya walokole! Tangu tupate uhuru hizo mimba zipo. Waathirika wapo wengine ni wakurugenzi katika mashirika ya umma na kampuni binafsi. Hilo hushughulikiwa kwa busara. Wote wanaopata ujauzito kwa sababu tofauti tofauti, mimba huwafukuza shule! Haiwekani kuhudhuria masomo na mimba. Hilo haliingii akilini. Wengi wao baada ya kujifungua hurudi shule. Hapa ndipo hutumika busara. Mhusika ataendelea na shule wapi na kivipi halikuwa tatizo.
Ile tu kusema sitasomesha mzazi ina maana walikuwa wanasoma! Huyo anayekataa alikuwa mbunge na kwenye baraza la mawaziri miaka 20. Miaka yote hiyo asijifunze hekima iliyokuwa inatumika! Tatizo la nchi za vita ya wenyewe kwa wenyewe huwa ni hilo la kukosa maarifa. Kila mmoja anasema yeye 'mwanaume bwana' Hapo ni risasi au panga tu! Huyu ukimkalisha chini ukamuuliza tatizo kwani liko wapi? Jibu utalopata: kwenye utawala wangu sahau kitu kama hicho. Nimeishasema. Mimi sio wachezomchezo. Kama hunifahamu uliza!
Kabisa mkuu,umeandika jambo kubwa sana ila hawa watu hawawezi kufungua akili zao!Kipindi cha nyuma walikuwa wanaondolewa shuleni kutokana na hali zao za Mimba,ila baadaye walirejea na mambo yalienda vizuri tu!Hakukuwa na mgogoro wowote,nini kimemkumba JPM mpaka kuliibua hili?Taifa hili si familia,unaweza kukuta kwenye familia mtu ndio msimamo wake huo,mtoto anapewa nafasi moja tu,akiharibu ndio basi!Sasa mambo kama hayo kuyaleta kwenye kutawala nchi inakuwa tatizo!
 
Hawa watoto hii sheria ya miaka 30 jela ndiyo wameamua kuifanya ngao ya kuendelea kufanya ushenzi wao, wanajua hawaguswi wakikutwa ni balaa kwa mwanaume tu. Hawa feminist waliyoipigia debe ipite, walifikiria kutetea jinsia yao na si kuzuia tatizo. Wanatongoza badala ya kutongozwa

Hizi mimba ndiyo zinazidi na ukisema umrudishe alozaa, ndiyo ataenda shawishi wengine nao waendeleze huo mchezo. Mwishowe darasa litakuwa na wazazi watupu, watoto wanamaliza shule ni wazazi.

Kuwakataza wasirudi, inawapa somo wengine kuwa hiko kitu siyo na wakiepuke. Ila kuruhusu warudi kutaongeza mfumuko wa mimba, maana ile sheria ndiyo imewapa go ahead ya kufanya ujinga wao.
Haya ni mawazo yako and as long as you have an identity huwezi kusema ukweli wako. Ukisema kinyume, UNAO!
 
.Eti tukiruhusu watoto waliojifungua unasema basi vikongwe warudi kusoma na watoto maana ni kitu hicho hicho!
Hivi mtoto akipewa mimba ndio umri unaongezeka na anakuwa mtu mzima?
takataka zingine usibishane nazo
 
Hakuna mtoto anampa mimba mtoto mwenzake, tumia akili sawa, mimba inawekwa na mtu aliekomaa kutoa mimba, awe na umli mdogo hata kama anasoma ataenda jela tu, au hilo nalo hujui?
Kijana wa kiume mwenye miaka 15 kampa mimba mtoto wa kike mwenye miaka 15!Inamaana wa kike anakuwa mtoto na wa kiume anakuwa mtu mzima?
Akili yako hujaitumia vizuri,hakuna kosa la kumpa mtu mimba bali kuna kosa la kubaka!Mimba ni matokeo tu!
Sasa nenda kwenye sheria ya ubakaji ukajifunze ili mtu awe amebakwa inatakiwa kuwe na mazingira gani!Kwa kukusaidia ni hivi
1.Mtu mzima kufanya ngono na mtoto(haijalishi kama wamekubaliana au lah)
2.Kufanya mapenzi na mtu bila ridhaa yake!

Sasa hapo,watoto wawili wenye miaka 15 wamekubaliana kufanya ngono,utasema nani kamlaghai mwenzake?Wote hawajakomaa kiakili!
Usiwe unakurupuka!
 
Hapo ndio kumaanisha wametofautiana? Au msimamo wa serikali upo palepale? Maana Abdul Nondo anataka warudi shuleni baada ya kujifungua kama nani?
Inashangaza....
Abdul Nondo 😀 😀 ni nani mpaka anachosema kwa jazba kikubalike na msemaji wa serikali??
Anajifananisha na mtoto wa baba, Naibu Raisi...

Everyday is Saturday.....................😎
 
Wewe ni mojawao?Umefahamuje ni makusudi wanafanya?Huwa wanabebeshwa mimba kama ndoo ya Maji?Hukumu ya wanaowapa ujauzito nayo iwe kuhasiwa,maana hiyo ndiyo angalau italingana na hukumu Kali ya kifungo cha ujinga kwa maisha yao yote.
Tuwe fair,tutafute namna ya kuwahakikishia wasichana hawapati ujauzito,wanaowabebeaha ujauzito wapewe adhabu itakayotoa funzo kwa wanaotarajia kujihusisha na wanafunzi kingono(wabakaji) badala ya kuwahukumu wahanga.
Hili tatizo ni gumu kuisha kwa kumuazibu mwanaume aliefanya hvyo njia pekee ni kuwapatia dawa za uzazi wa mpango wasichana wa shule
 
Je watoto wakiume wanaowabebesha mimba wafanyweje?
Sheria ile ile inayotumika kwa mtoto wa kike ndio inayotumika kwa mtoto wa kiume iwapo itathibitika ndiye aliyempa ujauzito mtoto wa kike. Tatizo mara nyingi linakuja kwenye "kuthibitisha".
 
hili la kurudisha wazazi darasani kwakweli hapana!
 
Hili tatizo ni gumu kuisha kwa kumuazibu mwanaume aliefanya hvyo njia pekee ni kuwapatia dawa za uzazi wa mpango wasichana wa shule
Dawa zinaweza kuwa one of the solutions,je kuna utafiti wa kisayansi kuonyesha sababu za mimba za utotoni?Huwezi kutatua tatizo bila kufahamu asili yake.
Hatua Kali kwa watoto wa kike kuachishwa masomo katika mfumo rasmi na kutokuwa na uhakika wa kupatiwa hata hiyo isiyo ya mfumo rasmi siyo sawa.Ni uvunjifu wa haki ya msichana/mwanafunzi/mtoto kupata ulinzi,elimu,afya bora na uhakika wa maisha yao.Tena wakati huo huo lazima kama Taifa tuweke utaratibu bora wa malezi watoto wanaozaliwa na wasichana/watoto/wanafunzi maana hawa ni innocent Tanzanians. Tusikubali kuwa sehemu ya ukatili dhidi ya watoto kwa kutokufahamu/kukusudia.
 
Hili tatizo ni gumu kuisha kwa kumuazibu mwanaume aliefanya hvyo njia pekee ni kuwapatia dawa za uzazi wa mpango wasichana wa shule
Dawa zinaweza kuwa one of the solutions,je kuna utafiti wa kisayansi kuonyesha sababu za mimba za utotoni?Huwezi kutatua tatizo bila kufahamu asili yake.
Hatua Kali kwa watoto wa kike kuachishwa masomo katika mfumo rasmi na kutokuwa na uhakika wa kupatiwa hata hiyo isiyo ya mfumo rasmi siyo sawa.Ni uvunjifu wa haki ya msichana/mwanafunzi/mtoto kupata ulinzi,elimu,afya bora na uhakika wa maisha yao.Tena wakati huo huo lazima kama Taifa tuweke utaratibu bora wa malezi watoto wanaozaliwa na wasichana/watoto/wanafunzi maana hawa ni innocent Tanzanians. Tusikubali kuwa sehemu ya ukatili dhidi ya watoto kwa kutokufahamu/kukusudia.
 
Back
Top Bottom