Hoja yangu haikuwa hiyo uliyoileta wewe. Badala yake, mzizi wa hoja yangu ulikuwa katika itifaki. Huyo kiongozi wa ACT halingani kihadhi na Katibu Mkuu.
Hoja za kijana wa ACT zingeweza kujibiwa na kiongozi wa UVCCM anayeuelewa vizuri msimamo wa serikali au raia huru yeyote anayeweza kutoa hoja kinzani.
Kwa meneno mengine, pengine kwa uwazi zaidi, katika mjadala husika, wanaharakati, asasi za kiraia na wapinzani wana hoja dhaifu mno zisizohitaji kujibiwa na Katibu Mkuu.
Hata kama tungejitahidi kudunisha nafasi ya Katibu Mkuu, hatuwezi kuondoa ukweli kwamba hiyo ni nafasi nyeti na muhimu serikalini.