Ndugu sidhani kama katika hili kuna U CCM na Upinzani, ni swala la Cultural and values za jamii yetu.
Hili sio swala la Mh. Rais wala CCM, ni swala sheria za nchi toka awali.
Kama umepita pita kwenye sekta ya elimu unaweza ukawa na mtizamo tofauti na hisia zako.
Sheria za shule, miongozo inayotolewa kuhusu mimba mashuleni ikiwa ni pamoja kitabu cha Kiongozi cha Mkuu wa Shule na Vyuo (1997) kilichotolewa na Wizara ya Elimu na Utamaduni zinasema wazi wazi makosa yanayoweza kumfukuzisha shule mwanafunzi ni pamoja KUMPA MTU MIMBA au Kupata Mimba wala si swala lililoasisiwa na JPM wala CCM ni swala la sheria za nchi.
Kama kutakuwa na mapungufu basi ni swala la wizara husika kurekebisha na si kumbebesha mtu au chama flani.
Umeuliza kama "tumepima madhara kama akirejea darasani ikishakaa na ananyonyesha" kutakuwa na madhara gani. Ni vema ukatambua kwamba sheria zinapotungwa zinakuwa zimezingagia si tu Falsafa inayoongoza nchi katika eneo hilo Bali pia huwa utafiti wa kina umefanyika. Je unaweza kumuadhibu mama mwenye kichanga cha miezi mitatu pale anapokosea kama ukiwa mwalimu?...he unajua atapata utulivu upi darasani wa kuzingatia masomo akiamua mume wake, mtoto na cha kumnyonyesha mwanae?...sasa kwa nini tusiwaruhusu wazee na wabibi waliokosa elimu kusoma katika madarasa ya kawaida na bint yako ambaye hajavunja ungo darasa moja?....he unajua umuhimu wa Peter peer grps katika kusoma?
Namba tatu unauliza vipi kwa mwanafunzi mwenzake aliyempa mimba? ...he unajua juvenile court unakazi gani?
Kifupi huna hoja.
Hujataka tu kuzitambua hoja zangu!
1.Rejea ilani ya CCM 2015,Pia rejea hotuba ya Mama Samia suluhu akiwa huki kaskazini akizungumza jukwaani kuwa serikali itawapa fursa watoto watakaozaa kurudi shuleni na baada ya kauli hiyo ndipo JPM akatoka hadharani na kusema kwenye serikali yake hatasomesha mtoti atakaye zaa!So hiyo ni yake!
2.Unazungumzia Juvenile court lakini hapo ni ni kwa criminal case!Mtoto wa miaka 15 kumpa mimba mtoto wa miaka 15 unasema wa kiume anapelekwa juvenile court na wa kike anafukuzwa shule,hapa huna hoja maana hakuna criminal case hapo!Hakuna kosa la kumpa mtu mimba bali kuna makosa kama kumbaka mtu!Sasa watoto wamekubaliana,wakafanya ngono na mmoja akapata ujauzito,hapo hakuba ubakaji!Ubaki unatoke kwa namna hizi tu
-Mtu mzima kufanya mapenzi na mtoto!
-Kufanya mapenzi na mtu bila ridhaa yake!
So kwenye pointi hiyo huna hoja!
3.Eti tukiruhusu watoto waliojifungua unasema basi vikongwe warudi kusoma na watoto maana ni kitu hicho hicho!
Hivi mtoto akipewa mimba ndio umri unaongezeka na anakuwa mtu mzima?Mtoto akibakwa na ikapelekea kupata mimba akijifungua akiwa na miaka 12,baadaye na mimi mtu mwenye miaka 30 nikamtongoza binti huyo akiwa na miaka 13,nikafanya naye ngono,nakuwa sijambaka kwa scenario yako ya kujifungua tayari ni mtu mzima??Mbona sheria inamtambua mtoto kwa umri na sio kama amezaa au la?
4.Huko nyuma mabinti ambao walikuwa wakijifungua,kama wazazi wanauwezo walikuwa wanafanya mpango na akijifungua anaenda kusoma shule nyingine,na wengi tumewaona wanaweza kuwa mashuhuda!
5.Hoja ya kwamba itakuwa ngumu kumuadhibu nayo ni mfu!Anaweza kuadhibiwa vizuri tu kutokana na kosa alilotenda lakini kuna mazingira akasamehewa bila wenzake kujua!Mfano hakumaliza honework,unaweza kumwita ofisini na kumwuliza kwanini, labda akakueleza kuwa mtoto alikuwa anaumwa basi unamwelewa kutokana na mzigo alionao!Kuna watoto wengi tu wenye matatizo mbalimbali na wanapewa excuse kwenye baadhi ya mambo,sio lazima wenzake wajue!Nayasema haya kwasababu nimeona baadhi ya cases!
6.Nimekupa mfano wa Kenya na Uganda,tungeenda kujifunza huko pengine tungepata kitu!
Tamaduni hubadilika kulingana na wakati!Mfano kwenye makabila mbalimbali mtoto wa kike alikuwa hapaswi kwenda shule,kwingine ilikuwa wanakeketwa wasiwe malaya,kwingine hawakuruhusiwa kula baadhi ya vyakula NK!Mambo yamebadilika sana,hatupaswi kuwa sehemu ya kutengeneza wajinga bali kuwakomboa!Huko katika mfumo usio rasmi ni kwa kupunguzia ujinga tu,ni dumping area!
Narudia,sijaona sababu yoyote significant ya kumzuia mtoto wa kike kurudi shule kama ikitokea akajifungua!