Dkt. Abbas na Watendaji wengine mlioko Serikalini kama hatuna uhakika na Viingereza vyetu vya 'Ukubwani' na 'Uchochoroni' tutumie tu Kiswahili chetu

Dkt. Abbas na Watendaji wengine mlioko Serikalini kama hatuna uhakika na Viingereza vyetu vya 'Ukubwani' na 'Uchochoroni' tutumie tu Kiswahili chetu

kienglish aka kikristo.....hii lugha ukiijua mpaka kutukana inakua tamu sana....ngoja nipige JD niingie kwenye kamusi yangu...
 
Wewe inasemaje mkuu?

mimi sijui ujue,🤣🤣🤣

wewe unajua, hata kama unajua one vocabulary

English ina maneno yanayotumika sasa 172,000 na yaliyoachwa kutumika 42,000 na katika hayo

20,000 ni ya kawaida sana kwa watu wengi

ukijua lolote tu umejua!!
 
Lugha ya mtu mwingine haijawahi kuwa na kanuni wakati wa kuizungumza, muhimu ni msikilizaje aelewe ulitaka kumaanisha nini. Hii lugha isituleetee presha, kwanza sio yetu, mbona hata kiswahili tunakosea?
 
Mimi nikisema "Kingereza" na wewe ukasema "Kiingereza" unadhani unaweza kuwa mjadara hapa jf, Hilo ni tatizo dogo sana kwenye mazungunzo ila kwenye maandishi ni kubwa sana na ukizingatia unategemea kusahihishwa na mwalimu akupe maksi
 
Ninakubaliana nawe hapa tena 100% tu.
Ila pia kwa kiinglishi kulicho kizuri huwezi kusema A lot. Ukidema tu Reforms are going on or rather A number of reforms are going on in our Ministry inatosha. A lot ni wingi na reforms ni wingi na inabeba a lot na a number.

Lugha ya malkia na ni ya 4 kwetu. Mimi wazazi wangu lugha 2 tofauti ongeza Kiswahili hivyo ya 4 ni Kiingereza tunachosoma shuleni tena enzi zetu hakuna Academy na English ilianzia darasa la 5 na yale mavitabu magumu ya malkia hata huekewi kitu. Ya Cambridge 🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Kwa miaka 15 sasa Chuo Kikuu ambacho kinazalisha Candidates ambao si tu wako Excellent Academically lakini pia hata Kivitendo ( Kiutendaji ) popote pale walipo wanafanya vizuri mno ni wa kutoka Chuo cha SAUT. Hili nina uhakika nalo 100% ukibisha ( ukilibishia ) utakuwa umeamua tu.
Chuo gani hicho wanafunzi na walimu wao wanaenda kufanya ufuska kwenye mapango ya mawe? Labda ungetoa mfano ni wapi walifanya vizuri kitaaluma, vitendo na maadili baada ya kuondoka chuoni ili wana jukwaa walinganishe.
 
Ngoja nijaribu
There is no subject - verb agreement

A lot of reforms are....
Nimejaribu tu mkuu
hamia uingereza basi mbona hawajakupa uraia hata visa una shida kuipata ya kwenda uingereza .Unajikomba sana kwa waingereza kwa kipi unachofaidi mbona uko choka mbaya tu.Nyooooo
 
Kumbe mtoa mada na wewe hujui kidhungu!! Mh. Yuko sawa kwa vyote gramma na semantic.

Kula shule kwanza:

“A lot of Reforms is going on now in our ministry “ tuigawanye hii sentensi katika kiima (subject) na kiarifu (predicate).
Kiima = “A lot of reforms” kiarifu = “is going on now in our ministry.” Neno “a lot” humaanisha wingi wa vitu visivyohesabika, na unapotendesha neno kama hilo kitenzi kiunganishi huwa ni ‘is’ mf. I saw ‘a lot’ of snow fall.....

hivyo, basi, tunaweza kusema mh. amemaanisha kuwa ‘kuna wingi usiyohesabika wa mabadiliko yanayofanywa ndani ya wizara yetu hivi sasa.’

sio sawa kusema ‘a lot of....are going on....’
Hapo unaendelea kuwapeleka shimoni. Vitu visivyohesabika ni mchanga, maji na mwazo yasiyoisha (infinity continuity). Kama wewe ni mtaalamu wa lugha hasa kiingereza hebu weka mapendekezo yake katika lugha halisia ya 'Wales' (Native English) ili somo lieleweke vema kama mfano katika utungaji wa sentensi Uwezo mzuri wa kuongea au kuandika kwa kutumia lugha ya kiingereza kunategemea kuwa ni sharti iwe ndio lugha yako ya kwanza kwa mawasiliano na kufikiria badala ya kutumia kimatengo kufikiria unahamishia kwenda kiswahili kisha ndio unapeleka namna ulivyofikiria, kuelewa, kutafisiri na kuamua hicho kilichojitengeza ndio kinapaswa kuzungumzwa. Ni bora wakati unaandika unaweza ukatumia 'proofreading' grammar and spelling correction' kupiga msasa ujumbe wako.

Tatizo ni kwamba ni lugha yako ya kwanza ambayo hata mama na baba walikukuza kufanya mawasiliano ya siku kwa siku. Pili lugha hiyo ndio unayotumia kufikiria, kuelewa na kutafsiri kabla hujatamka au kuandika?

Native English
A "native speaker of English" refers to someone who has learned and used English from early childhood. It does not necessarily mean that it is the speaker's only language, but it means it is and has been the primary means of concept formation and communication.

Katika nchi za Afrika Uganda ndio inaongoza kwa watu wake kuongea kwa kiingereza fasaha ijapokuwa kinaharibiwa na lafudhi ya makabila yao.

Afrika Kusini inayofuatia kwa kuongea kiingereza fasaha kiasi, kasoro lafudhi ya kikabila na kiiafrikaner

Inayofuata ni Nigeria ijapokuwa nao lafudhi na maneno ya kienyeji huchanywa sana

Malawi, Zambia na Zimbabwe ziko kwenye nafasi sawa kwa kuongea kiingereza kinachoshabihiana, kilichonyooka na ufasaha kiasi

Kenya wanaongeza kwa kujiamini lakini hakina ufasaha wa mzizi wa lugha halisia kutokana na majivuno na athari za lugha za kienyeji

Tanzania haiko kwenye kumudu matumizi ya lugha ya kiingereza kama taifa kutokana na kufikiri, kuelewa na kutafsiri kwa kutumia lugha ya mama na Kiswahili kisha kutafsiri neno kwa neno kwa mfuatano wa maneno katika lugha ya kiingereza hivyo kupoteza mantiki. (watu wachache sana ama waliosoma wakati nchi inapata uhuru au walienda nje kusoma au kufanya kazi kwa muda mrefu kisha kurejea hao kwa vyotevyote vile huko walikokuwa walikuwa wanafikiri, kuelewa na kutafsiri kwa kutumia lugha ya ughaibuni.
 
Jana jioni wakati nikisikiliza Kipindi cha BBC Dira ya Dunia ( kama kawaida yangu ) nilishtushwa kidogo nilipoisikia 'insert' ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari 'Mwanazuoni' Dkt. Hassan Abbas na 'Kiingereza' alichokitumia.

Wakati akizungumza kuhusiana na Masuala ya Habari, Wadau wa Habari huku akikaribisha Maoni ya Mabadiliko ya Kisera katika Wizara yake hiyo ndipo 'akachomekea' na Kiingereza chake hicho ili kuwadhihirishia Watu kuwa amesoma na hiyo 'Doctorate' yake hakuipata Kimakosa na hata huko Ulaya hadi Marekani ameishi vile vile.

Kiingereza chenyewe alichokisema ni hiki nakinukuu hapa..." A lot of reforms is going on now in our Ministry " mwisho wa Kumnukuu Msomi wa PhD Hassan Abbas.

Hivyo basi leo nawaomba wana JF wote ( ambao nawakubali sana kwa Kujua Kiingereza vyema ) japo nikiri tu kuwa GENTAMYCINE sikijui kabisa mnisaidie ni Sentensi ipi bora ( hasa Grammatically ) kati ya hizi zifuatazo.....

1. A lot of reforms is going on now in our Ministry

2 There has been a lot of reforms going on in our Ministry

3. A lot of reforms are going on now in our Ministry

4. There are lots of reforms going on now in the Ministry

Najua Wasomi Nguli ( Intellectuals ) hapa JamiiForums hamtaniangusha GENTAMYCINE katika Kunichagulia Kiingereza sahihi kabisa ( Grammatically ) kati ya Sentensi Nne hapo ( hapa ) juu.

Hakuna Lugha niipendayo duniani ( Ulimwenguni ) kama Kiswahili na hakuna Lugha ambayo huwa naipenda Kuisikia kwa Mtu akiiongea vizuri ( japo hata siijui ) kama ya Kiingereza na hakuna pia Lugha ambayo siipendi Mtu aikosee Kuizungumza kwa 'Kuishobokea' hata kama ( siijui ) kama ya Kiingereza.

Karibuni nyote mnifundishe Kiingereza.

Hata wewe hapo hamna jibu sahihi ulilotoa.
Zaidi umetumia tafsiri ya moja kwa moja. (Yaani direct translation).
Next time uandike hivi.

A lot of (legal or policy) reforms are currently going on in our ministry.

A lot of (legal or policy) reforms are currently taking place in our. ministry.
 
hamia uingereza basi mbona hawajakupa uraia hata visa una shida kuipata ya kwenda uingereza .Unajikomba sana kwa waingereza kwa kipi unachofaidi mbona uko choka mbaya tu.Nyoooo
Asante mkuu kwa kunimwagia povu
Sikuwa na povu la kufulia nguo.
 
Acha kupalilia ujinga wa mtu kwa kumuacha aishi na makosa.
Siku akijua amukumwambia makosa yake atawachukia.
Unauhakika huyo anaesemwa amekosea yupohumu anaona wanavyo mkosoa ama unaongeatu kama umekatwa kichwa.
 
Back
Top Bottom