Jana jioni wakati nikisikiliza Kipindi cha BBC Dira ya Dunia ( kama kawaida yangu ) nilishtushwa kidogo nilipoisikia 'insert' ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari 'Mwanazuoni' Dkt. Hassan Abbas na 'Kiingereza' alichokitumia.
Wakati akizungumza kuhusiana na Masuala ya Habari, Wadau wa Habari huku akikaribisha Maoni ya Mabadiliko ya Kisera katika Wizara yake hiyo ndipo 'akachomekea' na Kiingereza chake hicho ili kuwadhihirishia Watu kuwa amesoma na hiyo 'Doctorate' yake hakuipata Kimakosa na hata huko Ulaya hadi Marekani ameishi vile vile.
Kiingereza chenyewe alichokisema ni hiki nakinukuu hapa..." A lot of reforms is going on now in our Ministry " mwisho wa Kumnukuu Msomi wa PhD Hassan Abbas.
Hivyo basi leo nawaomba wana JF wote ( ambao nawakubali sana kwa Kujua Kiingereza vyema ) japo nikiri tu kuwa GENTAMYCINE sikijui kabisa mnisaidie ni Sentensi ipi bora ( hasa Grammatically ) kati ya hizi zifuatazo.....
1. A lot of reforms is going on now in our Ministry
2 There has been a lot of reforms going on in our Ministry
3. A lot of reforms are going on now in our Ministry
4. There are lots of reforms going on now in the Ministry
Najua Wasomi Nguli ( Intellectuals ) hapa JamiiForums hamtaniangusha GENTAMYCINE katika Kunichagulia Kiingereza sahihi kabisa ( Grammatically ) kati ya Sentensi Nne hapo ( hapa ) juu.
Hakuna Lugha niipendayo duniani ( Ulimwenguni ) kama Kiswahili na hakuna Lugha ambayo huwa naipenda Kuisikia kwa Mtu akiiongea vizuri ( japo hata siijui ) kama ya Kiingereza na hakuna pia Lugha ambayo siipendi Mtu aikosee Kuizungumza kwa 'Kuishobokea' hata kama ( siijui ) kama ya Kiingereza.
Karibuni nyote mnifundishe Kiingereza.