Miradi ya Maji sio kwamba inashida ya design la hasha.
Mkuu
Jidu La Mabambasi ameeleza sababu za wazi zinazokwamisha utekelezaji wa miradi ya Maji uki compare na miradi mingine ya Ujenzi, kama umewahi kufanya Kazi ya Ukandarasi utaona utofauti.
Miradi ya Maji tatizo lake kubwa ni Ucheleweshaji wa Malipo, hii hupelekea miradi isikamilike kwa wakati, inafikia kipindi Una raise madai ya labda 300M, lakini utakuja kulipwa labda baadaya ya miezi 6 au mwaka.
Sote tunajua mradi unapochelewa kukamilika unakuwa na cost implication hasa kwa Mkandarasi, unaweza kuta wakati Una bid bei ya bomba la 3" ilikuwa pengine 1,500,000 lakini kutokana na ucheleweshaji wa malipo hence mradi kuchelewa ambapo utakuta bomba imepanda tena bei, kwahiyo itakulazimu mrudi tena mezani na kuanza kuitumia hela ya Contingency ambayo itapelekea gharama ya Mkataba kupanda.
Ndiyo stage hii wasiojua kinachoendelea kusema miradi ya Maji kuna Upigaji.
Mkandarasi kama analipwa kwa Wakati hutakuja kuona hizo mambo.
Jifunzeni kwa miradi inayofadhiriwa na Donnars kama UNICEF, World bank au Ukaid ambayo inafanywa kwa Force account mbona inakimbia, ni kutokana na Wafadhiri kuingiza hela kwa watekelezaji kabla ya kuanza kujenga.
Kwa hili unaona kabisa mwenye shida ni Serikali nasio Makandarasi.
Asante kwa kuelezea matatizo makubwa yanayowakabili makandarasi wengi katika miradi ha Wizara ya Maji.
Hata hivyo tukumbuke kuwa miradi ya Maji ndiyo inapendwa na wanasiasa wengi.
Na wanasiasa hao wanapenda kuonekana mbele ya umma kuwa wanafanya kitu ili kutatua matatizo ya maji, hususan huko vijijini.
Kuna wanasiasa hadi wakatunga msemo ati kumtua mama ndoo kichwani.
Wizara ya Maji nayo imejiingiza kuendeshwa ili kuwaridhisha wanasiasa.
Chanzo cha maji kwa watu 1,000, wanasiasa pamoja na wataalam wa Maji wana extrapolate na kwa chanzo kile kile kujenga distribution ya watu 5,000, kinyume na usanifu wake.
Matokeo yake ni kiwa hata wale 1,000 hawapati maji hayo.
Hili ni tatizo la awali kabisa katika kuingiliwa miradi na Wanasiasa na kufeli kwa usanifu.
Pili, ni kweli kabisa fedha za miradi aidha zinachelewa au kkutofika kabisa kwenye mradi.
Ni jambo la kawaida fedha za mradi kuishia Wizara ya Maji au Halmashauri mradi uliko.
Hili swala la kweli kabisa lakini kule kwenye mradi, mkandarasi baada ya kusubiri malipo
kwa miezi sita au mwaka anaamua kuvunja kambi na kuondoka mwenye mradi.
Huku nyuma waziri mwenye dhamana anakagua mradi na kuelezwa mambo ambayo si ha kweli hivyo kumwongezea hasira mwanasiasa juu ya mkandarasi.
Miradi mingi sana makandarasi wamewekwa ndani lakini mashitaka hayaendi mahakamani.
Miradi midogo midogo ya visima na vyanzo vya maji vijijini ni ya watendaji wenyewe.
Tatu,miradi mingi ya maji haina usimamizi kabisa.
Mkandarasi anapewa mkataba na hasimamiwi kabisa, hivyo matatizo yanayojitokeza hakuna wa kuchukua hatua na kuakisi matokeo yake kimkataba na ongezeko la gharama.
Matokeo yake ni mradi kusimama kwa muda mrefu, ukisubiri maamuzi toka wasimamizi ambao hawapo.
Nne, kuna vijikampuni vingi vya watendaji vilivyopewa kazi za Maji.
Kama kampuni ni ya mtu aliyetoa kazi, atajichukuliaje hatua?
Matatizo yote haya yanahitajimsukumo maalum wa kuainisha jinsi ya kutekeleza miradi ya Maji.
Lakini mwanzo mwema ingalau umeanza kuonekana kwa kuanzisha mamlaka ya utekelezaji miradi ya Maji, RUWASA.
Mamlaka hii inabidi iwezeshwe ili iwepo kila mkoa kama TANROADS ilivyo na mamlaka hii iwe very technical na ipate watendaji wenye weledi.
Tatizo kubwa la Wizara ya Maji ni kuendesha miradi bila kuzingatia misingi ya Project Management.
Wanasiasa wajinasibu kuziba ombwe hilo kwa kutafuta mchawi wa kufikirika, kimakosa ati ni mkandarasi.
Proffessionals wanawacheka kimoyomoyo maana tatizo lipo pale pale.