#COVID19 Dkt. Akwilapo: Kwanini wathibiti Ubora wa Elimu Mashuleni hamvai barakoa?

#COVID19 Dkt. Akwilapo: Kwanini wathibiti Ubora wa Elimu Mashuleni hamvai barakoa?

Kwa kweli kuna shida kabisa shule za serikali bila masomo ya ziada mwanafunzi hawezi pata chochote na kama wana uchungu namna hiyo kwanini wasiongeze walimu shuleni kwa ajili ya kuwasaidia watoto kipindi cha masomo walimu hawafundishi wazazi tunafuatilia maendeleo yao hadi shuleni lakini ni mameno matupu na siku hizi hata mithiani yao wanayoifanya hawapewi matokeo wakati hicho ndo kipimo kwa wanafunzi na wazazi mzazi akiona mtoto anafanya vibaya somo fulani (kwenye matokeo ya mthiani) ataangalia ni namna gani amsadie (Hatuutaki huo upendo wao wafanye kitu kingine) hii ni nchi huru sio jela au tuambiwe sasa watakuja kutupangia ni lini na lini tutakuwa tuna lala na wake zetu naona hilo kwa mbaali
Halafu siku hizi kumhamisha mtoto kutoka sekondari ya serikali kwenda ya binafsi - mh.. Utahangaishwa wee, sijui!!
Kumbuka wote wanaomaliza darasa la 7 hupangwa shule za serikali - sasa njoo umhamishe mtoto!
 
OTE="OKW BOBAN SUNZU, post: 41006198, member: 52569"]
Msako waja kwa watakaosomesha wanafunzi likizo

Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk Leonard Akwilapo ametoa agizo kwa wathibiti wa ndani wa elimu nchini kufanya msako kwa watakaosomesha wanafunzi kipindi cha likizo.

Pia, Dk Leonard Akwilapo amesema kutatolewa kutatolewa barua kwa shule zote sa Serikali na binafsi kuweka msisitizo wa utekelezaji wa agizo hilo ambalo hivi karibuni Serikali ililitoa.

"Kupitia hadhira hii nawaagiza maofisa udhibiti kipindi hiki cha likizo hakikisheni mnafanya msako kuwabaini wanaokiuka agizo hili la Serikali la kuwataka watoto wapumzike na katika kuweka msisitizo hilo tutazipa barua shule zote," amesema Katibu huyo.

"Ni muhimu kufuata ratiba za mihula ya masomo kwani kumeibuka siku hizi makamishna wengi wa elimu huko mashuleni mpaka wanasiasa, nasema kamishna ni mmoja tu wa elimu nchi hii anayepanga ratiba za masomo, hivyo ni vema ikafuatwa,"amesisitiza Katibu huyo.

Amesema hata tabia ya kuwaamsha watoto saa kumi usiku kusoma sio sawa na badala yake wanajikuta wanakariri badala ya kutafakari kile walichofundishwa.

My Take
Sina shida na hoja ya serikali. Kero yangu ni kwa nini iwe lazima mpaka kwa mtu binafsi na mwanae? Kwani mwanangu akitwishwa mzigo wakati wa likizo mnapungukiwa nini?
Haya mahaba kwa nini msiyaonyeshe kwenye kuajiri walimu wa kutosha mpaka kusaza.

Darasa moja wanafunzi 100 kuna nini hapo? Vipi na sisi wazazi tuanzishe msako kwa waziri kuhusu watoto wetu 100 kujazana darasa 1?

Sisi tulioponea tuisheni tunajua unyeti wake. Kuna shule hazina kabisa walimu kwa baadhi ya masomo,inabidi ukasome tuisheni. Kuna hawa A Level mambo kibao mazito muda mchache,kwa government bila tuisheni hutoboi

Au kuna ajenda ya siri?
[/QUOTE]
Ticha unawazia pato peperushwa la twisheni?
 
Tuache watoto wapumzike

Ticha unawazia pato peperushwa la twisheni?[/QUOTE]
 
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo ameshangaa kuona watu kwenye Mafunzo na Semina Wizara ya Elimu hawavai Barakoa wala kufuata kanuni za afya za kujikinga na Covid-19.

Ameonge hayo wakati akifungua Mafunzo ya Uthibiti Ubora kwa Maafisa Elimu Kata na Wakuu wa Shule katika Shule ya Msingi Mnazi mmoja. "Kwanini hamjavaa Barakoa na hamtumii Vitakasa Mikono, Mnadhani Corona haipo? Amehoji Akwilapo.

Dkt. Leonard Akwilapo ametoa Maelekezo kwa Mafunzo na Semina zinazoendelea Nchini, Wahakikishe Wanafuata Taratibu zote za Afya za kujikinga na Maambukizi ya Corona sababu bado ipo. "Usalama wa afya kwanza" Amesema.

Dkt. Leonard Akwilapo amewagiza Wathibiti ubora wa Elimu kuhakikisha. Shule zinazingatia ratiba za kufunga na kufungua shule, Kamishina wa Elimu ndo Sheria imempa mamlaka ya kupanga Ratiba sio Mwanasia, au mtu yoyote. Amedia sasa hivi Shule zinaendeshwa ovyo ovyo kwani kila Shule inajipangia itakavyo.

Dkt. Leonard Akwilapo amesema Makuzi, malezi na Maendeleo ya mtoto kitaaluma, yanazingatia Vitu vingi. Kuna wakati Mtoto anatakiwa acheze, asome na apumzike. Lakini siku hizi Watoto Wanaamshwa saa kumi usiku wanaingizwa darasani kusoma, Mtoto hapati Muda wa kupumzika wala Kucheza. Watoto wanapigwa Viboko bila huruma. Hivyo ameagiza Wadhibiti ubora wa Elimu kulifanyia kazi. "Mafunzo haya yawe Chachu na ufanisi katika shughuli zenu za udhibiti Ubora". Amesema Dkt. Akwilapo.

"Kupitia hadhira hii nawaagiza maofisa uthibiti kipindi hiki cha likizo hakikisheni mnafanya msako kuwabaini wanaokiuka agizo hili la Serikali la kuwataka watoto wapumzike na katika kuweka msisitizo hilo tutazipa barua shule zote," amesema Katibu huyo.

Naye Mkurugenzi wa uthibiti ubora Wizara ya Elimu Euphrasia Buchuma amesema Awamu ya kwanza elimu wakuu shule za msingi Nchi nzima 8096, Maafisa elimu Mkoa 26 Maafisa elimu taaluma 26 Maafisa elimu Wilaya wa shule za Msingi 180. Awamu ya pili wametoa Mafunzo kwa Waalimu Wakuu 7, 679 Nchi nzima Isipokuwa shule mpya. Pia Wametoa Mafunzo kwa Waratibu Elimu kata 3, 901 Vipo Vituo 164 Nchi nzima ambavyo vinatoa mafunzo hayo.

Euphrasia amesema Wakaguzi wa Shule sasa Wanaitwa Wadhibiti Ubora.

Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk Leonard Akwilapo ametoa agizo kwa wathibiti wa ndani wa elimu nchini kufanya msako kwa watakaosomesha wanafunzi kipindi cha likizo.

Pia, Dk Leonard Akwilapo amesema kutatolewa kutatolewa barua kwa shule zote sa Serikali na binafsi kuweka msisitizo wa utekelezaji wa agizo hilo ambalo hivi karibuni Serikali ililitoa.

Hivi karibuni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi), Ummy Mwalimu alisema kuwa wakati wa likizo wanafunzi wasisome bali wapumzike.

Leo Jumanne Desemba 7, 2021 alipokuwa akifungua mafunzo ya uthibiti wa ndani kwa maofisa elimu kata na walimu wakuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Dk Akwilapo amebainisha kuwa wathibiti wa ndani wa elimu nchini watafanya msako kuwabaini watakaofundisha wanafunzi wakati wa likizo.

Amesema maofisa elimu hao wamesoma somo la saikolojia na wanajua umuhimu wa mapumziko katika makuzi ya mtoto hivyo hawapaswi kufungia macho vitendo hivi.

"Kupitia hadhira hii nawaagiza maofisa udhibiti kipindi hiki cha likizo hakikisheni mnafanya msako kuwabaini wanaokiuka agizo hili la Serikali la kuwataka watoto wapumzike na katika kuweka msisitizo hilo tutazipa barua shule zote," amesema Katibu huyo.

"Ni muhimu kufuata ratiba za mihula ya masomo kwani kumeibuka siku hizi makamishna wengi wa elimu huko mashuleni mpaka wanasiasa, nasema kamishna ni mmoja tu wa elimu nchi hii anayepanga ratiba za masomo, hivyo ni vema ikafuatwa,"amesisitiza Katibu huyo.

Amesema hata tabia ya kuwaamsha watoto saa kumi usiku kusoma sio sawa na badala yake wanajikuta wanakariri badala ya kutafakari kile walichofundishwa

Ulianza kusikia mwangwi wa hili gonjwa kutokea serikali hii ni vyema kujua hali si shwari.
 
Back
Top Bottom