Dkt Ayub Rioba akana tuhuma za yeye kuwa chawa

Dkt Ayub Rioba akana tuhuma za yeye kuwa chawa

Ukishakuwa Mtumishi wa Serikali au kampuni unafuata maagizo ya Boss wako.
Hao mnawaonea tuu
Ndio maana wanaitwa machawa, kwani wanasimamia wasichoamini, bali maagizo ya boss hata yasiyokuwa sahihi. Mfano halisi ni huyo Rioba. Tazama alichokuwa anasimamia kabla ya hiyo nafasi, na alipoipata nini alifanya.

anajifanya kutoa historia ya umasikini aliokuwa nao huko utotoni, na eti hata sasa atauweza. Atauweza wapi wakati umri umemtupa mkono, na alishapanda ngazi?
 
Cdm haina machawa serious maana haina dola wala hela ya kuhonga. Labda useme machawa wa enzi za Mbowe, ambao wametimkia Chauma. Lakini chini ya utawala wa Lisu ina manazi tu hakuna machawa maana hakuna hela ya kuwahonga.

Tanzania uchawa ni Mfumo.
Mfano watanzania wengi hawana uwezo wa kuusema ukweli. Kumwambia ukweli Mzazi kitamaduni za jamii nyingi za afrika ni kosa.

Kuikosoa dini yako hata kwa ukweli uliowazi ni kosa.

Mfumo wa kusifia sifia ndio upo
Ndio maana wanaitwa machawa, kwani wanasimamia wasichoamini, bali maagizo ya boss hata yasiyokuwa sahihi. Mfano halisi ni huyo Rioba. Tazama alichokuwa anasimamia kabla ya hiyo nafasi, na alipoipata nini alifanya.

anajifanya kutoa historia ya umasikini aliokuwa nao huko utotoni, na eti hata sasa atauweza. Atauweza wapi wakati umri umemtupa mkono, na alishapanda ngazi?
 
Ukishakuwa Mtumishi wa Serikali au kampuni unafuata maagizo ya Boss wako.
Hao mnawaonea tuu
Shida ya Rioba anakataa kuwa alikuwa anafuata maelekezo ya CCM!
Angekubali tu kuwa alikuwa CHAWA wa CCM kama matendo yake yalivyomdhihirisha!
 
Kwa hiyo mzee Rioba kwa maono na mipango yako mizuri uliitoa tbc wapi na ukafikisha wapi?
Je maono na mipango yako mizuri:.
1. Ilivutia watu kuipenda tbc?
2. Ilitengeneza program bora zaidi?
3. Ilingiza mapato mengi zaidi?
4. Iliacha kupata ruzuku serikalini?
Kwa kukataa kwenda kanada na Namibia ni kitu gani ulichoifanyia nchi yako cha kukumbukwa?
Kwa wale walioamua kuendelea kunitukana na kusema mimi 'chawa' na kwamba sasa ninarudi kushika jembe au kusota, nina ujumbe wenu pia!

Nilizaliwa ktk familia ya mwalimu wa shule ya msingi. Niliishi maisha ya Mtanzania wa kawaida kabisa. Wali au sukari vilikuwa vitu adimu. Mnavipata tu siku za sikukuu.
Sikuwahi kuwa na God Father au mtu wa kuniunganisha na fursa za uongozi. Lakini nilisoma Ilboru na Chuo Kikuu cha Makerere, Uganda.

Sikuwahi kuomba kuteuliwa nafasi yoyote ktk uongozi wa Taifa letu. Lakini nilifanikiwa kuwa mhadhiri wa UDSM, na nilikuwa na maisha mazuri tu kuliko niliyoishi utotoni!

Mwaka 2012 nilipata fursa za kufanya kazi vyuo vikuu vya nje (Kanada na ) ambapo ningelipwa dolari nyingi sana lakini nilizikataa (ushahidi upo). Ni kwa sababu ya kuamini ktk uwezo alionipa Mwenyezi Mungu na nia yangu ya kutumikia Nchi yangu!

Ndugu zangu ktk hii dunia huwezi kufanikiwa - au kuwa mtu wa maana zaidi - ati kwa sababu tu, unawavunjia heshima binadamu wengine.
Na huwezi kupata mafanikio, ati kwa sababu tu unawazodoa na kuwachafua wale unaotofautiana nao kimaoni.
Siku zote mafanikio huja unapokuwa na maono, mikakati sahihi, mipango thabiti, ubunifu, kujali muda na jitihada thabiti za utekelezaji wa maono na mipango yako.

Ukiona siku zote wewe ni mtu wa kulalamika, kutukana na kulaumu wengine - hata kwa udhaifu wako mwenyewe - basi ujue hayo ndiyo maono yako, mikakati yako, mipango yako na mavuno yako sawia.
Umaskini au ufukara ni hulka, ni imani, ni utamaduni na ni jinsi unavyojiambia mwenyewe kila siku.
Ukiwa na mawazo hasi ya kulaumu, kunung'unika, kutukana na kukashifu wengine kila siku, basi utaishi kwa nakisi na hata ukwasi utausikia tu kwa wengine.

Endapo unaamini kwamba maisha yako yanaweza kuwa bora zaidi leo kuliko jana, basi anza na maono, mikakati, mipango, utekelezaji na nidhamu yako mwenyewe! Hakuna miujiza!

Haya maneno ya ana 'njaa', 'kapata ulaji', 'kaula', 'kapataje hizo pesa', 'katumbuliwa', n.k. ni kielelezo cha jamii inayoishi kwa K 3. Kusoma, Kuhesabu na Kuandika. Mnaishia tu kwenye majungu, fitna na kukashfu wengine, ili walau nanyi 'mpande juu'!

Jamii inayofundisha watoto K5, Kusoma, Kuandika, Kuhesabu, Kufikiri na Kubuni ni lazima itatengeneza Taifa la watu wanaofikiri sawasawa na wanaotatua matatizo yao ya kila siku kwa kujitegemea, badala ya kuwa na watu ambao siku zote wanalaumu, wanatukana na kuzodoa wengine - hasa wale wanaoonekana wana 'mafanikio' fulani.

Kutukana, kukashifu, kuzodoa au kudhalilisha binadamu mwenzio - na wakati mwingine hata pale unapokuwa humfahamu sawasawa - ni kielelezo kwamba wewe unaishi maisha ya shida, ya hovyo na magumu mno!
Na ni ushahidi tosha kwamba madhali wewe mwenyewe umeshindwa kuboresha maisha yako mwenyewe, basi huna uhalali wa kuwasema wale - unaodhani - wameshindwa kuboresha maisha yako!

Hivi karibuni nitaanza kuandika Safu (nitawajulisha) ambapo nitajadili uzoefu wangu kuhusu mikanganyiko na mitanziko ya kidhana tunayoishi nayo, kama Waafrika, bila kuhoji kwa fikra tunduizi. Na inatugharimu!
Nitajadili kwa mtazamo wa Kiumajumui wa Afrika.
 
Back
Top Bottom