Dkt. Bashiru Ally anafanya mikutano ya hadhara kama nani ?

Dkt. Bashiru Ally anafanya mikutano ya hadhara kama nani ?

View attachment 1367061

Iko siku moja hawa Watanzania mnawaona wajinga mtawatafuta wawaokoe lakini hamtafanikiwa , ikiwa mzururaji kama Bashiru Ally anaruhusiwa kufanya mkutano wa hadhara , huku akiwa hana ajenda yoyote kwenye jimbo zaidi ya kutembea na hela za kununua wapinzani huku polisi wakimuwekea ulinzi , halafu wabunge halali wenye ajenda wanazuiwa kukutana na waajiri wao ambao ni wananchi basi bila shaka tunachokitafuta tutakipata tena kabla muda tuliokusudia

View attachment 1367066

Hii ni aibu kubwa sana kwa IGP na ni aibu kwa Msajili wa vyama na ni aibu kubwa sana kwa Nchi .

Dunia inaangalia .
Mambo haya yanajenga hasira miongoni mwa wananchi ambayo mlipuko wake ni kama mlipuko wa volcano. Kinachotengenezwa kitaiweka amani yetu katika hali isiyojulikana
 
Mwandishi Wetu
Jeshi la Polisi wilayani Kigoma limezuia mkutano wa hadhara wa Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini, Zitto Kabwe kwa madai ya sababu za kiusalama.

Mkutano huo wa Zitto ambaye pia ni Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, ulipangwa kufanyika leo Ijumaa Januari 17, katika Viwanja vya Mwanga Center, Manispaa ya Kigoma Ujiji.

Kwa mujibu wa barua ya Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kigoma, Raphael Mayunga kwa Ofisi ya Mbunge huyo, Jeshi la Polisi limezuia mkutano huo kwa sababu za kiusalama kutokana na taarifa za kiintelijensia zilizopo.

“Napenda kukujulisha kuwa mkutano huo umezuiliwa kwa tarehe uliyoomba kwa sababu za kiusalama kutokana na kiitelijensia zilizopo. Kwa hiyo huruhusiwi kufanya mkutano wala kuendelea na maandalizi ya mkutano huo.

“Aidha rejea Sheria ya Jeshi la Polisi na Huduma Saidizi sura ya 322 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002 katika Kifungu 43 (3) (4) (6),” imesema barua hiyo.

Akizungumzia uamuzi huo wa jeshi la polisi, Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano na Umma, ACT Wazalendo, Ado Shaibu amesema; “sababu iliyotajwa bila shaka haina mashiko na inalenga kumzuia Zitto Kabwe kutekeleza shughuli zake halali za kutumikia wananchi wa jimbo lake.”
 
Kwa nini mbunge asiwe na uhuru kufanya mkutano nje ya jimbo lake?

Mbona CHADEMA wabunge kibao walifanya mikutano Mwembeyanga kabla ya utawala wa Magufuli?

Hizi habari za kusema mbunge afanye mikutano jimboni kwake tu ni upumbavu gani huu?

Zimetoka katika sheria gani?

Sent using Jamii Forums mobile app
Hii ni sheria isiyorasmi toka kwa viongozi wa wanyonge wa sasa na malaika akiitwa mbinguni(Watamkoma) na watalimia meno.
 
View attachment 1367061

Iko siku moja hawa Watanzania mnawaona wajinga mtawatafuta wawaokoe lakini hamtafanikiwa , ikiwa mzururaji kama Bashiru Ally anaruhusiwa kufanya mkutano wa hadhara , huku akiwa hana ajenda yoyote kwenye jimbo zaidi ya kutembea na hela za kununua wapinzani huku polisi wakimuwekea ulinzi , halafu wabunge halali wenye ajenda wanazuiwa kukutana na waajiri wao ambao ni wananchi basi bila shaka tunachokitafuta tutakipata tena kabla muda tuliokusudia

View attachment 1367066

Hii ni aibu kubwa sana kwa IGP na ni aibu kwa Msajili wa vyama na ni aibu kubwa sana kwa Nchi .

Dunia inaangalia .
Tanzania inawenyewe na wenyewe ni CCM, wananchi tumekubaliana na hali hii inabidi tuipokee vinginevyo tuwasaidie polisi kuizuia.
 
Serikali ya chama lazima iisimamiwe vyema na chama ili kuhahakisha uwakilishi wa matarajio ya watu(wapiga kura) unazingatiwa. Nafasi na umuhimu wa Katibu Mkuu katika kuhahakisha hilo ni kubwa

Kama katibu mkuu angekaa tu bila kufatilia ahadi za chama hapo watu wangeuliza ni Nini nafasi ya chama katika kuisimamia Serikali? Kwa kuwa katibu mkuu anasimamia jukumu hilo vyema, wwatu wanapoñgeza tu.
Hivi huwa unasoma ulichoandika kabla ya ku-post?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sheria ya Vyama vya Siasa haijaweka mipaka ya Majimbo wala Kata kwa Wanasiasa.

Matamko yanayoweka mipaka ya Majimbo na Kata kufanya siasa ni UKIUKAJI WA KATIBA NA SHERIA ZA TANZANIA.

HIYO NI BIOLOGICAL WEAPONS.
😆😆😆😆
 
Back
Top Bottom