Dkt. Bashiru Ally anafanya mikutano ya hadhara kama nani ?

Mambo haya yanajenga hasira miongoni mwa wananchi ambayo mlipuko wake ni kama mlipuko wa volcano. Kinachotengenezwa kitaiweka amani yetu katika hali isiyojulikana
 

Mwandishi Wetu
Jeshi la Polisi wilayani Kigoma limezuia mkutano wa hadhara wa Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini, Zitto Kabwe kwa madai ya sababu za kiusalama.

Mkutano huo wa Zitto ambaye pia ni Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, ulipangwa kufanyika leo Ijumaa Januari 17, katika Viwanja vya Mwanga Center, Manispaa ya Kigoma Ujiji.

Kwa mujibu wa barua ya Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kigoma, Raphael Mayunga kwa Ofisi ya Mbunge huyo, Jeshi la Polisi limezuia mkutano huo kwa sababu za kiusalama kutokana na taarifa za kiintelijensia zilizopo.

“Napenda kukujulisha kuwa mkutano huo umezuiliwa kwa tarehe uliyoomba kwa sababu za kiusalama kutokana na kiitelijensia zilizopo. Kwa hiyo huruhusiwi kufanya mkutano wala kuendelea na maandalizi ya mkutano huo.

“Aidha rejea Sheria ya Jeshi la Polisi na Huduma Saidizi sura ya 322 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002 katika Kifungu 43 (3) (4) (6),” imesema barua hiyo.

Akizungumzia uamuzi huo wa jeshi la polisi, Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano na Umma, ACT Wazalendo, Ado Shaibu amesema; “sababu iliyotajwa bila shaka haina mashiko na inalenga kumzuia Zitto Kabwe kutekeleza shughuli zake halali za kutumikia wananchi wa jimbo lake.”
 
Hii ni sheria isiyorasmi toka kwa viongozi wa wanyonge wa sasa na malaika akiitwa mbinguni(Watamkoma) na watalimia meno.
 
Tanzania inawenyewe na wenyewe ni CCM, wananchi tumekubaliana na hali hii inabidi tuipokee vinginevyo tuwasaidie polisi kuizuia.
 
Hivi huwa unasoma ulichoandika kabla ya ku-post?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usimamizi wa chama kwa Serikali haina mipaka ya jimbo Wala kata kamanda

Sheria ya Vyama vya Siasa haijaweka mipaka ya Majimbo wala Kata kwa Wanasiasa.

Matamko yanayoweka mipaka ya Majimbo na Kata kufanya siasa ni UKIUKAJI WA KATIBA NA SHERIA ZA TANZANIA.

HIYO NI BIOLOGICAL WEAPONS.
 
Sheria ya Vyama vya Siasa haijaweka mipaka ya Majimbo wala Kata kwa Wanasiasa.

Matamko yanayoweka mipaka ya Majimbo na Kata kufanya siasa ni UKIUKAJI WA KATIBA NA SHERIA ZA TANZANIA.

HIYO NI BIOLOGICAL WEAPONS.
😆😆😆😆
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…