serio
JF-Expert Member
- Apr 15, 2011
- 7,340
- 4,734
Dakitare kilaza.. hahaha...Katibu Mkuu CCM Dr.Bashiru Ally amewaomba Wananchi kupuuza sera na kauli zinazotolewa na baadhi ya Viongozi wa Kisiasa Tanzania zikitaka wale bata (starehe) badala ya kazi na kusema jambo hilo lisipokemewa litasababisha Taifa kuwa legelege, tegemezi na kula bata badala ya kazi.
_
“Katika Nchi ambayo Wananchi wanapambana kujikomboa kiuchumi, hasa ktk nchi zetu za Afrika ambazo bado tupo nyuma kimaendeleo ya Mtu mmojammoja na Taifa kwa ujumla, kutokea Kiongozi na kuwaambia watu wafanye kazi kwa starehe ni usaliti mkubwa wa mapambano ya kiuchumi”-Dr.Bashiru
_
“Unaposema kazi na bata, ni kudhalilisha Wanawake na Mama zetu ambao wakati wote wamekuwa wakifanya kazi kusomesha Watoto, wakifanya kazi kulisha familia zao, kuwambia wale bata,ni sawa na kuwataka washinde kwenye starehe huku watoto wakidhalilika kwa kutokwenda shule”-Dr.Bashiru
Kazi tunafanya, na bata tunakula..
Kazi na dawa,
Kazi na bata..
Sent using Jamii Forums mobile app