Rugaiyulula
JF-Expert Member
- Jul 29, 2015
- 2,524
- 1,705
Hakuna kulazimishana hapa ila ni kukumbushana kuwa KAZI NA BATA kama ilivyo HAPA KAZI TUU ambavyo siyo kulazimisha kwamba watu wafanye kazi tuuuuuu.Naona unakuja na matusi, muungwana huongea lugha iliyojaa busara! Anyway, tatizo linaloonekana hapo ni msisitizo wa kula bata, ikimaanisha watu wafanye starehe! Sasa kula bata iwe kauli mbiu, unafikiri jamii inachukuliaje? Wapo watakaofikiri kuwa kumbe kufanya starehe ni lazima hata kama uchumi hauruhusu kufanya hivyo (hii ndio maana ya kauli mbiu, in other words we can say it is a command).
Mtu akifanya kazi, akichoka, atahitaji kupumzika, kula, au hata kunywa (it is a natural phenomenon), huhitaji kumwambia ‘nenda kale’. Hata Nyerere alipojenga hizo kumbi alijuwa kuwa kuna wakati watu watachoka na watahitaji kupumzika, lakini kamwe hakuwalazimisha kula bata, maana alijuwa kungekuwa na mapokeo ambayo yangeleta impact mbaya kwenye uchumi aliouanzisha.
Upande wa lugha niseme samahani sana kama sijaleweka maana matusi siyo sitahili yangu ya uhandishi.