Dkt. Bashiru awashangaa wapenda ‘Kazi na Bata’. Asema kauli hiyo inachangia kuzorotesha Uchumi

Dkt. Bashiru awashangaa wapenda ‘Kazi na Bata’. Asema kauli hiyo inachangia kuzorotesha Uchumi

Huyu Dr fake kabisa

Sasa anategemea nini pale mtu anapofanya kazi na kufanikiwa kupiga pesa za maana anatakiwa afanye nini na hizo pesa baada ya kazi?
kazi lazima utufanye tuishi maisha ya raha na starehe!
Katibu Mkuu CCM Dr.Bashiru Ally amewaomba Wananchi kupuuza sera na kauli zinazotolewa na baadhi ya Viongozi wa Kisiasa Tanzania zikitaka wale bata (starehe) badala ya kazi na kusema jambo hilo lisipokemewa litasababisha Taifa kuwa legelege, tegemezi na kula bata badala ya kazi.
_
“Katika Nchi ambayo Wananchi wanapambana kujikomboa kiuchumi, hasa ktk nchi zetu za Afrika ambazo bado tupo nyuma kimaendeleo ya Mtu mmojammoja na Taifa kwa ujumla, kutokea Kiongozi na kuwaambia watu wafanye kazi kwa starehe ni usaliti mkubwa wa mapambano ya kiuchumi”-Dr.Bashiru
_
“Unaposema kazi na bata, ni kudhalilisha Wanawake na Mama zetu ambao wakati wote wamekuwa wakifanya kazi kusomesha Watoto, wakifanya kazi kulisha familia zao, kuwambia wale bata,ni sawa na kuwataka washinde kwenye starehe huku watoto wakidhalilika kwa kutokwenda shule”-Dr.Bashiru

Sent using Jamii Forums mobile app
 
CCM mtaongea sana, ila 2020 mjipange. Hata mfungue "OFISI ZA CHAMA - TAWI DOGO LA CCM" ndani ya "TRENI au BOMBADIA".
CCM ITASHINDA KWA KISHINDO kuna jamaa zangu ni wabunge wa upinzani huwa nawaambia kabisa watafute shuguli ya kufanya
 
Wanapotoa vibali kwa ajilil ya shughuli za starehe lengo lao huwa nini kama si watu kula bata? Mtu wao aliyekodisha mabehewa na kupeleka watu Kigoma kazi anayofanya ni nini kama siyo kuwafurahisha watu wanapokula bata baada ya kazi ngumu za kujitafutia riziki?
 
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Dkt. Bashiru Ally, amewataka wananchi kupuuza kauli ya kufanya kazi na kula Bata ambayo imeratibiwa na Mbunge wa Kighoma Mjini Zitto Kabwe na kusema kauli hiyo itachangia kuzorotesha uchumi wa Taifa.

Dkt. Bashiru amesema kuwa, katika nchi ambayo wananchi wanapambana kujikomboa kiuchumi, hasa katika nchi zetu za Afrika ambazo bado tupo nyuma kimaendeleo ya mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla, kutokea kiongozi mmoja kuwaambia watu wafanye kazi kwa starehe ni usaliti mkubwa wa mapambano ya kiuchumi.

“nchi hii ambayo tunaongoza mapambano ya kujikomboa kiuchumi, inamuhitaji kila mtu kwa nafasi yake kuhimiza kufanya kazi kwa bidii, na huku CCM kuna kauli mbalimbali za kuhimiza kazi zikiwemo, Hapa Kazi tu, Kazi na Maendeleo, Uhuru na Kazi na Kazi ni Utu, ila kuna baadhi ya Vyama wao wanahubiri kazi na starehe, na huo ndiyo utofauti wa Chama kiongozi na Vyama vya uchaguzi.’’ Dkt. Bashiru

"Unaposema kazi na bata, maana yake ni kudharirisha wanawake na mama zetu ambao wakati wote wamekuwa wakifanya kazi kusomesha watoto wao, wakifanya kazi kulisha familia zao, na sote hapa ni matokeo ya juhudi kubwa za mama zetu, ambao kuwambia wale bata, ni sawa na kuwataka washinde kwenye starehe huku watoto wakidhalilika kwa kutokwenda shule."
baada ya hiyo hotuba nayeye c anaenda kula bata au,dah ccm bhana hii slogan imewauma sana kamekuwa kamsumari kwao
 
Anataka tuseme kazi na rushwa? Ile rushwa yak ya 3 billion waliyopokea toka kwq wahindj
 
Mi nafikiri kazi ikulipe ikuingizie kipato unachostahili sio msuli tembo matokeo sungura ndo tafsiri ya bata uone matokeo ya kile unachokifanya sio hiki kinachofanyika kwa sasa hivi pesa hamna ajira hazipo mtaani Hali ngumu
 
Nyerere hakuwa mjinga aliyejenga kumbi za starehe pale alipojenga viwanda. Na pale penye shughuli / ofisi za kiserikali hapakukosa kumbi za starehe hadi leo. Police & Offciers Messes / clubs. NBC, Bandari TANESCO Club na kadhalika.
Tusiwe makasuku Fulani staehe in nafasi yake katika maisha ya binadamu.
Huyo Bashiru anajua fika hata wanazuoni wanajengewa kumbi za starehe kama ilivyo hapo UDSM ili baada ya kazi waburudike.

Naona unakuja na matusi, muungwana huongea lugha iliyojaa busara! Anyway, tatizo linaloonekana hapo ni msisitizo wa kula bata, ikimaanisha watu wafanye starehe! Sasa kula bata iwe kauli mbiu, unafikiri jamii inachukuliaje? Wapo watakaofikiri kuwa kumbe kufanya starehe ni lazima hata kama uchumi hauruhusu kufanya hivyo (hii ndio maana ya kauli mbiu, in other words we can say it is a command).

Mtu akifanya kazi, akichoka, atahitaji kupumzika, kula, au hata kunywa (it is a natural phenomenon), huhitaji kumwambia ‘nenda kale’. Hata Nyerere alipojenga hizo kumbi alijuwa kuwa kuna wakati watu watachoka na watahitaji kupumzika, lakini kamwe hakuwalazimisha kula bata, maana alijuwa kungekuwa na mapokeo ambayo yangeleta impact mbaya kwenye uchumi aliouanzisha.
 
Back
Top Bottom