Dkt. Bashiru awashangaa wapenda ‘Kazi na Bata’. Asema kauli hiyo inachangia kuzorotesha Uchumi

Dkt. Bashiru awashangaa wapenda ‘Kazi na Bata’. Asema kauli hiyo inachangia kuzorotesha Uchumi

Kama vile umaskini ni sifa ambayo baadhi ya Viongozi wanatumia kuwaonea huruma wahusika wakati wao wanakula mpaka wanatapikia kwenye viatu vyao....
Huyo mzee bado anadhani watu wanaishi dunia ya hadaa. Yeye anajifanya anajali watu masikini, wakati anatembea na VX na anakula na kusaza. Ni nani kamwambia anavutiwa na hizo kalimbiu za kimaskini za ccm?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Dkt. Bashiru Ally, amewataka wananchi kupuuza kauli ya kufanya kazi na kula Bata ambayo imeratibiwa na Mbunge wa Kighoma Mjini Zitto Kabwe na kusema kauli hiyo itachangia kuzorotesha uchumi wa Taifa.

Dkt. Bashiru amesema kuwa, katika nchi ambayo wananchi wanapambana kujikomboa kiuchumi, hasa katika nchi zetu za Afrika ambazo bado tupo nyuma kimaendeleo ya mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla, kutokea kiongozi mmoja kuwaambia watu wafanye kazi kwa starehe ni usaliti mkubwa wa mapambano ya kiuchumi.

“nchi hii ambayo tunaongoza mapambano ya kujikomboa kiuchumi, inamuhitaji kila mtu kwa nafasi yake kuhimiza kufanya kazi kwa bidii, na huku CCM kuna kauli mbalimbali za kuhimiza kazi zikiwemo, Hapa Kazi tu, Kazi na Maendeleo, Uhuru na Kazi na Kazi ni Utu, ila kuna baadhi ya Vyama wao wanahubiri kazi na starehe, na huo ndiyo utofauti wa Chama kiongozi na Vyama vya uchaguzi.’’ Dkt. Bashiru

"Unaposema kazi na bata, maana yake ni kudharirisha wanawake na mama zetu ambao wakati wote wamekuwa wakifanya kazi kusomesha watoto wao, wakifanya kazi kulisha familia zao, na sote hapa ni matokeo ya juhudi kubwa za mama zetu, ambao kuwambia wale bata, ni sawa na kuwataka washinde kwenye starehe huku watoto wakidhalilika kwa kutokwenda shule."
Inashangaza sana huyu kiumbe haelewi maana ya kazi na bata
 
I dont blv in jalalaz phd
 
DKT. BASHIRU AWAOMBA WANANCHI KUPUUZA SERA NA KAULI ZINAZOHIMIZA UVIVU ZA BAADHI YA VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA NCHINI

29 Desemba, 2019

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Dkt. Bashiru Ally, amewaomba wananchi kupuuza sera na kauli zinazotolewa na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa nchini zikitaka wananchi wale bata (wafanye starehe) badala ya kufanya kazi jambo ambalo likiachwa bila kukemewa litafanya kuwa na taifa legelege la kupenda starehe badala ya kazi.

Dkt. Bashiru amesema kuwa, katika nchi ambayo wananchi wanapambana kujikomboa kiuchumi, hasa katika nchi zetu za Afrika ambazo bado tupo nyuma kimaendeleo ya mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla, kutokea kiongozi mmoja kuwaambia watu wafanye kazi kwa starehe ni usaliti mkubwa wa mapambano ya kiuchumi ambayo kama taifa tunayahimiza.

Katibu Mkuu ameyasema hayo alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa ofisi ya CCM Kata ya Bwanjai wilayani Misenyi tarehe 28 Desemba, 2019 na kuzungumza na wanachama na wananchi waliojitokeza katika ukaguzi huo.

“Nchi hii ambayo tunaongoza mapambano ya kujikomboa kiuchumi, inamuhitaji kila mtu kwa nafasi yake kuhimiza kufanya kazi kwa bidii, na huku CCM kuna kauli mbalimbali za kuhimiza kazi zikiwemo, Hapa Kazi tu, Kazi na Maendeleo, Uhuru na Kazi na Kazi ni Utu, ila kuna baadhi ya Vyama wao wanahubiri kazi na starehe, na huo ndio utofauti wa Chama kiongozi na Vyama vya uchaguzi.’’ Dkt. Bashiru ameeleza

Ameongeza kwa kusisitiza kuwa, “Unaposema kazi na bata, maana yake ni kudharirisha wanawake na mama zetu ambao wakati wote wamekuwa wakifanya kazi kusomesha watoto wao, wakifanya kazi kulisha familia zao, na sote hapa ni matokeo ya juhudi kubwa za mama zetu, ambao kuwambia wale bata, ni sawa na kuwataka washinde kwenye starehe huku watoto wakidharirika kwa kutokwenda shule, hizi ni kauli za kipumbavu za Vyama vya uchaguzi, ambazo hatuna budi kuzidharau na kuzipuuza."

Aidha ameongeza kuwa, Chama Cha Mapinduzi kitaendelea kuwa chama cha kutetea haki za wanyonge na kitaendelea kusisitiza sekta zote za serikali zikiwemo afya, elimu, miundombimu na maji kutoa huduma kwa wananchi bila usumbufu wala ubaguzi na kuthamini utu wa watu wote.

Mkutano huo umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kagera mama Costancia Buhiye na Mkuu wa wilaya ya Misenyi Kanal Mstaafu Denis Mwila

Ikumbukwe kuwa, Dkt. Bashiru yupo nyumbani kwake Bukoba mkoani Kagera kwa mapumnziko ya siku kumi, na anatarajiwa kumaliza mapumziko hayo mapema mwezi Januari, 2020.

Imetolewa na;
Afisa Habari
Ofisi ya Katibu Mkuu
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
IMG-20191230-WA0022.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Home boy bwana wakati mwingine siasa zake ni shida kuzielewa.

Yaani mtu kufanya kazi na baada ya kazi kustaarehe ni upumbavu kweli?
Hapo Bwanjai Mugana saa kumi ikifika atakuta watu akiwemo yeye mwenyewe wanakula bata kama Lubisi, Kapelele kiti moto choma na kadhalika. Kesho yake kazi kama kawa.
 
Mwanaume ndio Mlishaji wa Familia.. Mtafutaji wa Familia.

Ache kututoa kwa reli.....

Hapa ni Kazi na Bata
 
Home boy bwana wakati mwingine siasa zake ni shida kuzielewa.

Yaani mtu kufanya kazi na baada ya kazi kustaarehe ni upumbavu kweli?
Hapo Bwanjai Mugana saa kumi ikifika atakuta watu akiwemo yeye mwenyewe wanakula bata kama Lubisi, Kapelele kiti moto choma na kadhalika. Kesho yake kazi kama kawa.

Dr yuko sahihi sana. Anachomaanisha hapa ni kuwa kipaumbele ni kujenga uchumi na sio kudumaza uchumi. Ukihubiri kazi na bata (sijuwi kama na yenyewe ni kauli mbiu), tafsiri yake ni kuwa ‘fanya kazi na kipato upatacho tumia kwa starehe’ (no saving). Sasa huu ni uchumi wa aina gani?

Nakumbuka wakati fulani tulipokuwa shuleni kuna msemo tulikuwa tunasema ‘work done equal to zero’ pale ikionekana mtu amejitahidi kufanya jambo fulani lakini hakuna matokeo, hili nalifananisha na kazi na bata, maana kipato unachopata unakitumia kwa starehe, kesho huna kitu. Tupige kazi, tupate kipato, and then we save for future investment!
 
Katibu Mkuu CCM Dr.Bashiru Ally amewaomba Wananchi kupuuza sera na kauli zinazotolewa na baadhi ya Viongozi wa Kisiasa Tanzania zikitaka wale bata (starehe) badala ya kazi na kusema jambo hilo lisipokemewa litasababisha Taifa kuwa legelege, tegemezi na kula bata badala ya kazi.
_
“Katika Nchi ambayo Wananchi wanapambana kujikomboa kiuchumi, hasa ktk nchi zetu za Afrika ambazo bado tupo nyuma kimaendeleo ya Mtu mmojammoja na Taifa kwa ujumla, kutokea Kiongozi na kuwaambia watu wafanye kazi kwa starehe ni usaliti mkubwa wa mapambano ya kiuchumi”-Dr.Bashiru
_
“Unaposema kazi na bata, ni kudhalilisha Wanawake na Mama zetu ambao wakati wote wamekuwa wakifanya kazi kusomesha Watoto, wakifanya kazi kulisha familia zao, kuwambia wale bata,ni sawa na kuwataka washinde kwenye starehe huku watoto wakidhalilika kwa kutokwenda shule”-Dr.Bashiru
 
Dr yuko sahihi sana. Anachomaanisha hapa ni kuwa kipaumbele ni kujenga uchumi na sio kudumaza uchumi. Ukihubiri kazi na bata (sijuwi kama na yenyewe ni kauli mbiu), tafsiri yake ni kuwa ‘fanya kazi na kipato upatacho tumia kwa starehe’ (no saving). Sasa huu ni uchumi wa aina gani?

Nakumbuka wakati fulani tulipokuwa shuleni kuna msemo tulikuwa tunasema ‘work done equal to zero’ pale ikionekana mtu amejitahidi kufanya jambo fulani lakini hakuna matokeo, hili nalifananisha na kazi na bata, maana kipato unachopata unakitumia kwa starehe, kesho huna kitu. Tupige kazi, tupate kipato, and then we save for future investment!
Nyerere hakuwa mjinga aliyejenga kumbi za starehe pale alipojenga viwanda. Na pale penye shughuli / ofisi za kiserikali hapakukosa kumbi za starehe hadi leo. Police & Offciers Messes / clubs. NBC, Bandari TANESCO Club na kadhalika.
Tusiwe makasuku Fulani staehe in nafasi yake katika maisha ya binadamu.
Huyo Bashiru anajua fika hata wanazuoni wanajengewa kumbi za starehe kama ilivyo hapo UDSM ili baada ya kazi waburudike.
 
Back
Top Bottom