Uchaguzi 2020 Dkt Bashiru: CCM haipo tayari kupoteza jimbo la Iringa Mjini

Uchaguzi 2020 Dkt Bashiru: CCM haipo tayari kupoteza jimbo la Iringa Mjini

Dr ,impartiality is quite needed during general election political intrigues are temporary measures that will spoil our political image internationally
 
Acha ukabila wewe jibu hoja ya msingi mpangaji anatakiwa kupisha mwenye nyumba yake anaitaka
zwazwa kwelikweli. mwenye nyumba ya jimbo la iringa mjini ni wapiga kura wa jimbo hilo. walimwona msigwa wa chadema anatosha. wakamchagua na kumwacha wa ccm. labda kwa goli la mkono!
 
Kupoteza au kutokupoteza jimbo ni maamuzi ya wananchi wala sio katibu mkuu wa chama, hawa ccm wana dharau sana wanaonaga wananchi kama mazombie/misukule isiyojitambua,isiyoweza kujua kiongozi gani anafaa.

Sent using Jamii Forums mobile app

Mkuu kwani awamu hii ya tano viongozi wanapatikana kwa njia ya kura? Huyo katibu mkuu hayuko sahihi kusema hivyo, lakini kiuhalisia ndio hivyo. Ni jimbo lipi wapinzani watatangazwa washindi eti kwasababu wameshinda kwenye box la kura?
 
Usilie mchungaji ajiandae kuchunga kanisa sio jimbo au kama vipi anunue mbuzi akachunge

USSR

Sent using Jamii Forums mobile app
kama watakwenda kwa ubabe wa polisi na mabomu ya machozi na ubabe wa kutumia risasi hapo sawa, lakini kama watakwenda kwa haki, sidhani kama ccm itapita, labda wampige chini na wa kwao apite bila kupingwa kama walivoyfanya serikali za mitaa
 
Dr ,impartiality is quite needed during general election political intrigues are temporary measures that will spoil our political image internationally
kwanza nikushangae kwa ruhusa yako mwenyewe. at last you have come to your senses. kuhusu huyu dr, it's an abortion. alijijengea heshima kama mchambuzi wa siasa. kama mwanamke mpumbavu abomoavyo nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe, bashiru anabomoa heshima yake kwa maneno yake mwenyewe. hajawa profesa lakini aliheshimika kuliko hao maprofesa na hata mentot wake dr bana!:kyaruzi mfanyie huo ushauri kwa kilugha cha kwenu( bojo kaziro). upumbavu amwachie m/kiti wake na sampuli zake. he's stooping too low!
 
DKT. BASHIRU: CCM HAIPO TAYARI KUPOTEZA JIMBO LA IRINGA MJINI

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally, akiwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani Iringa, amewahakikishia wanachama, mashabiki na wakereketwa wa CCM kuwa Chama hakipo tayari kupoteza jimbo la Iringa Mjini kama ilivyofanyika miaka michache nyuma.

Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na viongozi wa kamati za siasa za wilaya ya Kilolo, Iringa Mjini na Iringa Vijini mara baada ya kupokelewa akitokea Mkoani Dodoma.

"Ujumbe ninao utoa kwa vyama vya upinzani leo tarehe 17 Desemba, 2019 ni kuwa, nataka jimbo la Iringa mjini na Manispaa yake lirudi CCM, na Mkoa wa Iringa umekuwa ni ngome ya CCM miaka yote, hapa mjini yalifanyika makosa ambayo ndani ya uongozi huu hayatojirudia tena."

Aidha Katibu Mkuu ameongeza kuwa,
Jimbo hilo lilipotea kutokana na migawanyiko ndani ya CCM, na awamu hii, jimbo na manispaa yake inarudi CCM na Chama hakitarajii kufanya makosa tena.

Katika hatua nyingine, Dkt. Bashiru ameendeleea kuwaasa wanaCCM kuwa, heshima wanayopatiwa viongozi, ni heshima kwa Chama, ambapo ndani ya CCM hakuna mtu maarufu wala kiongozi maarufu kuliko chama, nje ya Chama, hakuna mtu maarufu hivyo ni lazima viongozi na wanachama wajue wanapata heshima kwa sababu ya Chama na ni lazima tukilinde ili kiendelee kubaki na heshima wakati wote.

Wakati huo huo, Katibu Mkuu ametumia fursa hiyo kueleza msimamo wa CCM katika uongozi, ambapo ni mtu mmoja kofia moja na kiongozi yeyote hana sababu ya kujiuzulu nafasi aliyonayo kabla hajapata nafasi aliyoiomba, hivyo ameshauri nchi nzima wale waliojiuzulu nafasi zao kwa lengo la kugombea serikali za mitaa na hawakufanikiwa kuchaguliwa, warudi kwenye nafasi zao kwa kuwa wengi hawakuwa na sababu za msingi.

Katibu Mkuu yupo Mkoani Iringa kwa siku mbili ambapo kesho atakuwa mgeni maalum katika uzinduzi wa chuo cha Mafunzo cha CCM Ihemi kitakachofunguliwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Ndg. Philip Japhet Mangula.

Imetolewa na:
Said Said Nguya
Afisa Habari
Ofisi ya Katibu Mkuu
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)

Sent using Jamii Forums mobile app
Haya kazi kwenu polisi na tume ya uchaguzi, jukumu jingine hilo mmepewa na bosi wenu.
KURA YANGU SIYO HAKI YANGU.
 
P
Hii ndio hizi trends tulizozingungumza humu
Na kwa Uchanguzi wa 2020
Formula hii itatumika kwa Majimbo yote yalichini ya upinzani, yatarejeshwa na Bunge la 2020-2025 litakuwa ni Bunge la chama kimoja CCM

Pascal unasapoti wizi wa kura uliopangwa na dunderhead mkuu aliyesukumizwa bila aibu kabisa.Swali Bashiru ndio anapiga kura?
 
Hivi
Wahehe mpo? Mnamsikia Mhaya huyo anayekuja kwenu kuwatukana kuwa maamuzi yenu hawezi kuyakubali lazima ya kwao ndio yawe?
Ana tofauti gani na gavana wa mjerumani aliyekataa maamuzi ya Mkwawa na watu wake kujipangia mambo yao akitaka ya kwao ndio yawe? Jee Mkwawa alikubali? La hasha, alionyesha ushujaa wake na ndio maana anakumbukwa mpaka Leo na wahehe wana heshimiwa.
Jee wahehe wa Leo CCM imewaona ni Mdebwedo hadi aje atambe?

Sent using Jamii Forums mobile app
Hivi Mwisho wake nani alishinda? Kama unamjua aliye shinda basi usilinganishe - aliyo yasema Katibu wa CCM.
 
Who cares?
Hii ndio hizi trends tulizozingungumza humu
Na kwa Uchanguzi wa 2020
Formula hii itatumika kwa Majimbo yote yalichini ya upinzani, yatarejeshwa na Bunge la 2020-2025 litakuwa ni Bunge la chama kimoja CCM


P

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bashiru ni msaliti wa wahaya, walidhulumiwa rambirambi yeye akahongwa ukatibu,akashindwa kuwatetea wahaya wenzake waliyokumbwa na tetemeko. Bashiru katumika kuwanyonga wahaya, jinga kabisa.
 
Chakaza,
Acha ukabila wewe jibu hoja ya msingi mpangaji anatakiwa kupisha mwenye nyumba yake anaitaka
Hoja ya ukabila umekuja nayo wewe! Au unaizungumzia Ile hoja ya kabudi mwanza kuwa nguvu ya ccm ipo Kanda ya ziwa huku kwingine ni za kujazilizia tu?! Kauli Ile inahamasisha Nini Kama sio ukanda na ukabila?
Nikutaarifu tu kuwa, bashiru na polepole wapo ccm kimkakati ili wakipasue chama mapande manne kama siyo sita na ccm itapotolea na kuwafia mikononi mwao! Utaniita mpiga ramli, ni sawa.
 
Back
Top Bottom