Uchaguzi 2020 Dkt Bashiru: CCM haipo tayari kupoteza jimbo la Iringa Mjini

Uchaguzi 2020 Dkt Bashiru: CCM haipo tayari kupoteza jimbo la Iringa Mjini

Hivi
Hivi Mwisho wake nani alishinda? Kama unamjua aliye shinda basi usilinganishe - aliyo yasema Katibu wa CCM.
Unaujua ushindi wa vita ni nini? Ukishatambua hilo rudi tena uulize swali lako. Vita vina ushindi wa aina nyingi sana, kwa nini Mkwawa aliitwa shujaa?
 
Egnecious,
Anayeweza kusema hayupo tayari kupoteza ni aliyenacho sasa hivi... unapotezaji ukiwa huna..??? MASIKINI HAFILISIKI
 
1576691108249.png


Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Bashiru Ally, akiwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani Iringa, amewahakikishia wanachama, mashabiki na wakereketwa wa CCM kuwa Chama hakipo tayari kupoteza jimbo la Iringa Mjini kama ilivyofanyika miaka michache nyuma.


Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na viongozi wa kamati za siasa za wilaya ya Kilolo, Iringa Mjini na Iringa Vijini mara baada ya kupokelewa akitokea Mkoani Dodoma.

“Ujumbe ninao utoa kwa vyama vya upinzani leo tarehe 17 Desemba, 2019 ni kuwa, nataka jimbo la Iringa mjini na Manispaa yake lirudi CCM, na Mkoa wa Iringa umekuwa ni ngome ya CCM miaka yote, hapa mjini yalifanyika makosa ambayo ndani ya uongozi huu hayatojirudia tena.”

Aidha Katibu Mkuu ameongeza kuwa,
Jimbo hilo lilipotea kutokana na migawanyiko ndani ya CCM, na awamu hii, jimbo na manispaa yake inarudi CCM na Chama hakitarajii kufanya makosa tena.

Katika hatua nyingine, Dkt. Bashiru ameendeleea kuwaasa wanaCCM kuwa, heshima wanayopatiwa viongozi, ni heshima kwa Chama, ambapo ndani ya CCM hakuna mtu maarufu wala kiongozi maarufu kuliko chama, nje ya Chama, hakuna mtu maarufu hivyo ni lazima viongozi na wanachama wajue wanapata heshima kwa sababu ya Chama na ni lazima tukilinde ili kiendelee kubaki na heshima wakati wote.

Wakati huo huo, Katibu Mkuu ametumia fursa hiyo kueleza msimamo wa CCM katika uongozi, ambapo ni mtu mmoja kofia moja na kiongozi yeyote hana sababu ya kujiuzulu nafasi aliyonayo kabla hajapata nafasi aliyoiomba, hivyo ameshauri nchi nzima wale waliojiuzulu nafasi zao kwa lengo la kugombea serikali za mitaa na hawakufanikiwa kuchaguliwa, warudi kwenye nafasi zao kwa kuwa wengi hawakuwa na sababu za msingi.

Katibu Mkuu yupo Mkoani Iringa kwa siku mbili ambapo kesho atakuwa mgeni maalum katika uzinduzi wa chuo cha Mafunzo cha CCM Ihemi kitakachofunguliwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Ndg. Philip Japhet Mangula.
 
Kwani Iringa Mjini jimbo la nani?!
Wanapotezaje kwani?!
 
Hoja ya ukabila umekuja nayo wewe! Au unaizungumzia Ile hoja ya kabudi mwanza kuwa nguvu ya ccm ipo Kanda ya ziwa huku kwingine ni za kujazilizia tu?! Kauli Ile inahamasisha Nini Kama sio ukanda na ukabila?
Nikutaarifu tu kuwa, bashiru na polepole wapo ccm kimkakati ili wakipasue chama mapande manne kama siyo sita na ccm itapotolea na kuwafia mikononi mwao! Utaniita mpiga ramli, ni sawa.
Hamueleweki, kusema sehemu yetu ya Strong hold ni ukabila? Huko upinzani wapanga mikakati wameisha asee, mpigieni magoti to Dr. Arudi la sivyo bashiru anawalaza na viatu
 
Hamueleweki, kusema sehemu yetu ya Strong hold ni ukabila? Huko upinzani wapanga mikakati wameisha asee, mpigieni magoti to Dr. Arudi la sivyo bashiru anawalaza na viatu
Unajipa moyo usiokuwa nao! Kama kwenye tests na mitihani yake tulilala na boksa Hadi asubuhi na tukatoboa utakuwa huku mtaani? Kwa kifupi tu hanaga lolote zaidi ya kujibebesha na dola!
 
CCM ilikwishasema hii nchi INA wenyewe na wenyewe ni CCM, hivyo majimbo yote ni mali ya CCM.
 
Back
Top Bottom