Dkt. Bashiru: Siyo kweli kwamba CCM itatumia wingi wao Bungeni kubadilisha Katiba ili kumuongezea muda Rais Magufuli kukaa madarakani!

Katibu mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru amekanusha uvumi unaoenezwa na wapinzani kwamba wabunge wa CCM watatumia wingi wao bungeni ili kumuongezea Rais Magufuli muda wa kukaa madarakani iwe zaidi ya miaka 10.

Dkt. Bashiru amesema Rais Magufuli atahudumu madarakani kwa miaka 10 kwa mujibu wa katiba ya sasa na kwamba propaganda za wapinzani hasa Chadema zipuuzwe.

Nawatakia ninyi nyote Dominica yenye baraka!

Maendeleo hayana vyama!
Hizi nyuzi zote zitafukuliwa kwa kasi mambo yatakapokuwa peupe.
 
Katibu mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru amekanusha uvumi unaoenezwa na wapinzani kwamba wabunge wa CCM watatumia wingi wao bungeni ili kumuongezea Rais Magufuli muda wa kukaa madarakani iwe zaidi ya miaka 10.

Dkt. Bashiru amesema Rais Magufuli atahudumu madarakani kwa miaka 10 kwa mujibu wa katiba ya sasa na kwamba propaganda za wapinzani hasa Chadema zipuuzwe.

Nawatakia ninyi nyote Dominica yenye baraka!

Maendeleo hayana vyama!
Marais wote watakaofuata baada ya Rais Magufuli kuna uwezekano wakaitumia katiba kikamilifu kama ambavyo Rais Magufuli anavyoitumia.

Na wote wakiitumia kama wanavyoapa NITAITETEA NA KUILINDA uwezekano waMadikteta kuwa wote ni mkubwa sana.

Hakuna Rais atakaye kuja ambae atakuwa Dikteta, ila Katiba yetu ina uwezo mkubwa wa kuzalisha Madikteta. Na kwa kuwa wanafuata katiba kwa hiyo Marais wetu sio madikteta ila katiba inawataka wafanye hivyo.
 
Bora Katibu mkuu ameclarify hili mapema maana ndio habari inayojadiliwa mjini kwa sasa ,

Nimefarijika mno kuwa viongozi wakuu wa chama wamelitolea ufafanuzi mapema.
 
Mbona hata Rais alishaweka wazi hataongeza hata sekunde moja hii ipo wazi kabisa.
Usimwamini sana, Museveni alipopata madaraka alieleza kutoongeza hata dakika ikiwa muda wake utafika ukomo kwa mujibu wa Katiba miaka hiyo, lakini leo yupo madarakani anaifanya katiba anavyo jisikia.
 
Usinitajie huyo Mzee aisee.
 
Usimwamini sana, Museveni alipopata madaraka alieleza kutoongeza hata dakika ikiwa muda wake utafika ukomo kwa mujibu wa Katiba miaka hiyo, lakini leo yupo madarakani anaifanya katiba anavyo jisikia.
Kweli Rais hataki kuongeza lakini 84% ya Watanzania tunataka katiba ibadilishwe na tutashinikiza hilo kwa maandamano nchi nzima
Kama ulivyosikia katika salamu za Christmas viongozi wote wa kidini wameshinikiza lazima atawale milele Yaani kifo Ndio kikomo chake
Huyu Rais ni mwema sana mwenye roho ya huruma na upendo kwa RAIA wake
Katika kipindi chake maisha yameboreka na watanzania tunaishi kama masultani kuanzisha wafanyakazi,. Wafanyabiashara hadi Wakulima
Shule bure
Huduma za afya bure
Miundo mbinu kila pahala
Yaani raha tupu
Ila wapiga dili lazima muumie maana mianya imeziba kabisa
 
Baba wa taifa Mheshimiwa JPM hana shida na CCM ili awepo miaka mingi ijayo,maana wananchi walio wengi wameona utendaji wake wa kazi hakuna ccm mwenye uwezo wa kufikia kiwango hicho.
Wananchi wamejiridhisha kuwa Mkuu aendelee ni suala la muda tu tutaingia barabarani kutaka aendelee uongozi wake umetoa nuru kwa future ya Tanzania,sasa hivi viongozi wote wa serikali wanakwenda na kasi ya mheshimiwa Raisi Magufuli.
bashiru hana ubavu mbele ya mwenyekiti wake wa CCM.
 
....tutaomba kuwe na referendum na tuwe na chombo huru cha kusimamia kura zetu.
MAAJABU HAYATAISHA DUNIANI.

Kukiwa na Tume huru ktk hiyo kura ya maoni... Na majibu yakawa Ni Hapana kuongeza muda.
Hili litakuwa pigo kubwa kwa CCM... Kuwepo madarakani.
 
Kweli Rais hataki kuongeza lakini 84% ya Watanzania tunataka katiba ibadilishwe na tutashinikiza hilo kwa maandamano nchi nzima
Kama ulivyosikia katika salamu za Christmas viongozi wote wa kidini wameshinikiza lazima atawale milele Yaani kifo Ndio kikomo chake
Huyu Rais ni mwema sana mwenye roho ya huruma na upendo kwa RAIA wake
Katika kipindi chake maisha yameboreka na watanzania tunaishi kama masultani kuanzisha wafanyakazi,. Wafanyabiashara hadi Wakulima
Shule bure
Huduma za afya bure
Miundo mbinu kila pahala
Yaani raha tupu
Ila wapiga dili lazima muumie maana mianya imeziba kabisa
Sina shaka na utendaji wake lakini ni muhimu kuzingatia Katiba.

Mwalimu Nyerere anasema na yeye alikuwa na watu wanamwambia usiondoke nchi bado changa akagundua si kweli kwamba waliwaza nchi ni changa bali waliangalia kama akiondoka madarakani je, nafasi zao nani angezilinda?

Naamini Rais ni mtu mwenye busara na amesisitiza juu ya hili kuwa hataongeza muda.
 
Back
Top Bottom