Dkt. Bashiru: Siyo kweli kwamba CCM itatumia wingi wao Bungeni kubadilisha Katiba ili kumuongezea muda Rais Magufuli kukaa madarakani!

Dkt. Bashiru: Siyo kweli kwamba CCM itatumia wingi wao Bungeni kubadilisha Katiba ili kumuongezea muda Rais Magufuli kukaa madarakani!

Baba wa taifa Mheshimiwa JPM hana shida na CCM ili awepo miaka mingi ijayo,maana wananchi walio wengi wameona utendaji wake wa kazi hakuna ccm mwenye uwezo wa kufikia kiwango hicho.
Wananchi wamejiridhisha kuwa Mkuu aendelee ni suala la muda tu tutaingia barabarani kutaka aendelee uongozi wake umetoa nuru kwa future ya Tanzania,sasa hivi viongozi wote wa serikali wanakwenda na kasi ya mheshimiwa Raisi Magufuli.
bashiru hana ubavu mbele ya mwenyekiti wake wa CCM.
Mwalimu Nyerere alishasema hakuna mtu mwingine atakayetawala zaidi ya miaka 10 kama yeye endapo ataheshimu katiba.

Acheni kumpa shinikizo Mkuu ili kufurahisha nafsi zenu.
 
Wapinzani wakikosa hoja huwa wanakuja na vioja. Nakumbuka haya waliwahi kuyasema hata ktk miezi ya mwisho mwisho ya utawala wa JK kwamba anapanga kuongeza siku za kukaa madarakan, JK akawajibu kwamba hatozidisha hata dakika 1 ya kukaa madarakan kwa mujibu wa sheria. Sasa leo tena badala ya kuja na hoja zenye mashiko wao wanakuja na hoja za masikitiko.
Ally Kessy aliyeanzisha hiyo hoja bungeni ni mpinzani, Job ndugai aliyemuahidi kessy kuwa ahifadhi hoja yake hadi bunge hili (bahati mbaya hakufanikiwa kurudi) ili ifanyiwe kazi na kumhakikishia kuwa itapitishwa kwa nguvu na kumlazimisha jiwe kuongeza muda naye ni mpinzani. Tatizo la vijana wa ccm mna usahaulifu mkubwa
 
Kumuelewa ni Hadi ufahamu code za kuelewa,Kama Hakuna nia ya kubadilisha katiba why wamelazimisha wawe pekee yao bungeni
 
Mwalimu Nyerere alishasema hakuna mtu mwingine atakayetawala zaidi ya miaka 10 kama yeye endapo ataheshimu katiba.

Acheni kumpa shinikizo Mkuu ili kufurahisha nafsi zenu.
Nyerere sio Mungu na angekuwepo hata Sasa wasiojulikana wangeshamtembelea siku nyingi Sana.
Afrika mfumo ukishakutupa unaweza fanywa chochote na aliyeshika usukani
 
Nyerere sio Mungu na angekuwepo hata Sasa wasiojulikana wangeshamtembelea siku nyingi Sana.
Afrika mfumo ukishakutupa unaweza fanywa chochote na aliyeshika usukani
Unaongea usichokijua wewe yule Mzee alikuwa na kipawa cha ajabu sana wangeanza kusalitiana wao kwa wao na pia alikuwa hanyamazi katika kukemea mambo yasiyofaa na Watanzania walimsikiliza.
 
Hawa wanajitekenya hakuna mtu mwenye habari nao tena wanabaki kujiongelesha ongelesha tu
Haohao ccm si ndiyo walikuwa wanabwbwaja bungeni kwamba rais aongezewe muda
Inashangaza leo Katibu mkuu wa CCM anaanza kusingizia vyama vya upinzani wakati hoja ilisemwa na wabunge wa CCM na kuungwa mkono na spika kwa shangwe nyingi za wabunge wa CCM. Angeanzia hapo kwanza kabla ya kuja kwa wananchi.
 
We babu si ulisema CCM haitatumia wasanii mwenye kampeni zake; ehe ikawaje tena ? leo tena unasema atii??
Kutumia wasanii ni baada ya kuona bidhaa yao haiuziki ilibidi kuepuka aibu watu wajae kumtazama Diamond.
 
Kwani uamuzi wa kuongezewa mda wanao wao kama chama,au anao Magufuli kama ni mtu amabaye huamua mambo anavyotaka yeye
Kuongeaza muda ni kutokan kwamba kma cham kitamuamin tenah lazima ashike miak mingne hivyo yaaaan
 
Unaongea usichokijua wewe yule Mzee alikuwa na kipawa cha ajabu sana wangeanza kusalitiana wao kwa wao na pia alikuwa hanyamazi katika kukemea mambo yasiyofaa na Watanzania walimsikiliza.
Shida sio kunyamaza.
Inategemea ni wakati gani.Awamu hii aliye juu ni mmoja tu mwenye uwezo wa kufanya chochote mtu yeyeto,uwaogopa mabeberu tu na tena sababu ya pesa zao
 
Inashangaza leo Katibu mkuu wa CCM anaanza kusingizia vyama vya upinzani wakati hoja ilisemwa na wabunge wa CCM na kuungwa mkono na spika kwa shangwe nyingi za wabunge wa CCM. Angeanzia hapo kwanza kabla ya kuja kwa wananchi.
Yule Mh.Mbunge aliyepigwa chini alisema aongezewe apende asipende,kiti kikamwambia kwa vile tunarudi kwenye next bunge kaa na hiyo hoja uilete halafu tutaipitisha bila hata ya kusema Mwenyezimungu akitujaalia uzima.
 
Toka Enzi za mwinyi hakukuwa n'a rais ambaye alihisiwa ataongeza muhula wake Mpaka awamu hii... Tena tetesi zilianza mapema sana
 
Rais wetu amesema hataki, acheni umbea. Kama ingekuwa uwezo wangu binafsi ningemfanya angalau aongezewe miaka 15, ana maono makubwa he is Genius . Lakini tumeshimu kile anachosema, tumuache amalize kipindi chake kitakachokua na mafanikio ya kihistoria.
 
Ni kweli kabisa ht Mseven alipinga kujiongezea muda wa kukaa madaraka ....

Bashiru,Polepole na JIWE wanatuletea FUTUHI ,Hivi watu wanafikiri CHAMWINO inajengwa kwa ajili ya kukaa nani? Hivi Mpaka ikamilike iwe vizuri si mpaka 2022? Sasa unafikiri anajengewa nani wa kukaa miaka mitatu kisha aachie MJENGO?
 
Bora Katibu mkuu ameclarify hili mapema maana ndio habari inayojadiliwa mjini kwa sasa ,

Nimefarijika mno kuwa viongozi wakuu wa chama wamelitolea ufafanuzi mapema.
Speaker mmeshaongea naye kwamba aachane na hiyo hoja huko Bungeni?
 
CCM akuna Rais wa kudumu wala mwenyekiti wa kudumu kama wenyeviti wa kudumu kwenye vyama vingine,ni miaka kumi tu unaachia madaraka.
 
Bashiru,Polepole na JIWE wanatuletea FUTUHI ,Hivi watu wanafikiri CHAMWINO inajengwa kwa ajili ya kukaa nani? Hivi Mpaka ikamilike iwe vizuri si mpaka 2022? Sasa unafikiri anajengewa nani wa kukaa miaka mitatu kisha aachie MJENGO?
Mbona hapo Ufipa hakuna mjengo lakini mwenyekiti ameng'ang'ania zaidi ya miaka 20?!

CCM ni chama kikubwa!
 
Mbona hapo Ufipa hakuna mjengo lakini mwenyekiti ameng'ang'ania zaidi ya miaka 20?!

CCM ni chama kikubwa!

Bwasheee Kukosa Mbowe CDM ingekuwa ishakufa!! CDM imesimama kwa Juhudi za Mwamba MBOWE!! Fedha za ruzuku haziwezi kujenga Makao Makuu kwa sasa ,Subiri CDM ichukue nchi ndio ijenge HQ.
 
Back
Top Bottom