Dkt. Biteko: Rais Samia anachukizwa Haki za Kidini zikipuuzwa

Dkt. Biteko: Rais Samia anachukizwa Haki za Kidini zikipuuzwa

Rais Samia Suluhu Hassan anasikitishwa anapoona haki za kidini zinapuuzwa
Ona ulaghai kama huu; sijui kama ni kweli Samia kayasema haya maneno, au hawa wanaotumika kama vikaratasi vya chooni wanayatunga wenyewe!
na akiwaalika ili kuzungumza masuala mbalimbali ya kitaifa.
Kwa hiyo mpango ndio huo, wa kuwaalika wazungumze ili wasalimishe jahazi linalozama?
Hajui watu sahihi wa kuzungumza nao kuhusu maswala ya kisiasa yanayolikabili taifa hili sasa hivi? Anaogopa kujibu hoja zilizo wazi kabisa, za kuwepo na marekebisho za kanuni kabla ya uchaguzi?
Anakwepa kwepa hivi kwa sababu gani?
 
Huyu dogo simuelewagu kabisa! Yaani hana Charisma kabisa....hata akiongea ni kama Mzee wa Kanisa anahamisidha mavuno!
Bora hata angekuwa hana charisma halafu anaongea point.

Hana charisma halafu anaongea uchawa.

Samia anafungia watu wasiende makanisani mwao kwa sababu Gwajima kamwambia ukweli.

Hiyo ni mtu anayechukizwa haki za kidini zikipuuzwa?

Upumbavu gani huu?
 
Kumekuwa na hii tabia ya kumsemea Samia. Nimesikia Makalla akimsemea Samia pia leo.

Kwani Samia mwenyewe hawezi kusema tukamsikia?

Zaidi, kwa nini marais wa Tanzania ni nadra sana kufanya press conference na waandishi wa habari, wakaulizwa maswali ya hapo kwa papo, wakajibu?

Sasa hivi nchi ipo katika tafrani nyingi zenye maswali mengi, kwa nini rais hajitokezi na kukaa na waandishi akajibu maswali?
Yeye Samia akiwa anahutubia anaongea utumbo mtupu lakini chawa wake wanamsemea vinginevgo
 
Kwanini wanasiasa hupewa airtime kwenye majukwaa ya kidini kwenda kuzungumza unafiq?

Wanasiasa kama ni kuzungumza masuala ya dini ingefaa wazungumze na watu wa dini zao tena yanayohusiana na dini zao Mkristo azungumze na Wakristo wenzake Muislam azungumze na Waislam wenzake tena asizungumze siasa atoe nasaha za kidini tu.
Haya mambo ya kipuuzi puuzi yameanza kukuzwa miaka ya hivi karibuni wanasiasa walipoanza kujipendekeza kwa viongozi wa dini.
Maswala ya serikali yangefaa yaachane kabisa na habari hizi za dini; na hivyo hivyo maswala ya dini yasiwahusu kabisa viongozi wa kisiasa
Kiongozi wa dini awe ni mshiriki tu katika dini inayomhusu kama waumini wengiine wa kawaida.
Unafiki wa kulazimisha maombi kwenye mikutano ya kisiasa yapigwe marufuku kabisa. Hata huko Bungeni na kwingineko, anayetaka kusali, asali kivyake, siyo kwa muda wa maswala ya serikali.

Kumekuwepo na upuuzi mwingi sana wa mwingiliano wa siasa na imani za watu, na ndiyo sababu sasa tumo kwenye matatizo haya. BAKWATA sasa ndio wanaoiendesha serikali na chama.
 
Asipotoshe, Samia amedhihirisha kuwa ni adui wa ukristu
Hawa marobot wake wanampamba kwa lugha, mtu ambaye matendo yake ni tofauti kabisa na anavyouzwa kwa wananchi. Sijui wao wanafikiri wananchi hawana akili ya kuona matendo maovu?
 
Biteko kajishushia kabisa personality yake. Alipaswa atafute namna ya kuongea na siyo kusema Dkt Samia anapenda viongozi wa dini huku huyo huyo Dkt Samia akiagiza Padre auawe kwa kupigwa na kitu kizito na huyo huyo Dkt Samia aagize kanisa la Gwajima lifugwe na kupigwa waumini wake, in short Dkt Biteko kaonesha si ujinga tu bali uchawa utakao mgharimu siasa zake hapo mbeleni
 
Yeye mwenyewe Biteko hachukizwi nazo ? Au kuna nani anazipenda ?; Haya mambo mengine makes you wonder hawa watu wapo pale kwa ajili ya nani ? Matumbo, Mtu au Wenye Nchi ambao ni Wananchi na ambao ndio wanawalipa kwa kupitia Kodi
 
Ila viongozi wa Tanzania huwa wana tu chukulia kama mazombii hivi, inamaana sisi hatuoni yanayo endelea nchini!
 
Back
Top Bottom