Dkt. Charles Kimei apewe Uwaziri wa Fedha haraka

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
7,823
Reaction score
10,857
Ndugu yetu Mwigulu anajifunza kazini na hii wizara inahitaji mtu ambaye anaweza na kujua jinsi ya kutatua matatizo na sio kila siku kubishana na wanasiasa. Matatizo makubwa ni haya ambayo Dr Kimei ndiye anaweza kurekebisha kwa haraka

1. Tatizo la dollar
2. Tatizo la riba kuwa juu
3. Kuanzisha credit rating system Tanzania
4. Nchi yetu kupata bond za uchumi kama kujenga barabara au reli badala ya kuchukuwa mikopo.

Yote haya Kimei atafanya vizient kuliko hawa wanasiasa kama Mwigulu ambao hawana uzoefu wa kutosha. Tuache kuogopa watu ambao ni bosses

 
Kuendesha benki uchwara kama crdb na kuwa waziri wa fedha ni vitu viwili tofauti.
 
Tatizo la Dollar ni universal, acha porojo na itadumu mpaka mwezi wa kumi na mbili ama mpaka mwakani hivi kwasababu FED wameamua kutackle tatizo la mfumuko wa bei nchini Marekani ambapo imeonyesha kuwa na data nzuri za labour market (although ni tight labor market ila inaridhisha). Na wameshasema hawa-cut interest rates mwaka huu.

Kuhusu riba kubwa, Kuna muda mlianza lalamika kuwa bei ya unga Iko juu, B.O.T ikastep in kuongeza riba kushusha inflation although Serikali iliendelea na expansionary fiscal policy ila matokeo umeyaona.
 
Bei ya unga haikushuka kwa sababu BOT iliongeza riba. Bali ilishuka kwa sababu ya mavuno makubwa ya mahindi na zuio la serikali kwa wafanya biashara kuuza mahindi nje.

Kama hujui kitu kaa kimya.
 
Atakausha sefu zote pale treasury, asilani asipewe kabisa uwaziri wowote, tutakaushwa.
 
Kwamba ndio ataleta Dola au? 🤣🤣 Akili za kijinga sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…