nakushukuru kwa kuelewa kwamba Lowassa alishinda kwa zaidi ya kura mil 10 na aliyepata mil 3 unusu ndio akatangazwa , lakini elewa kwamba wengi watapiga kura kwa Lissu na hasa baada ya kufichua kwamba hatakubali kuibiwa
Spin doctoring----- propagandist. wakati sisi kaskazini kura zetu nyingi tulizipeleka upinzani, wenzetu Mwanza, Simiyu, Shinyanga, Geita, Tabora, Dodoma, Iringa, Ruvuma, Katavi na Kagera walipeleka CCM. angalia takwimu za NEC wao ni kama 77% ya wapiga kura wote nchi yetu.
Upinzani tungeshindaje?.
Tuelimishane ili tupunguze ushabiki maandazi.
Ni kura za Dar es salaam ndio zilizo tupatia kiwango kikubwa cha kura.
Nadhani hufamu hili: Wilaya ya Kinondoni ina wapiga kura wengi kuliko Mkoa mzima wa Arusha.
Wilaya ya Ilala inawakaazi wengi kuliko Kilimanjaro,
Temeke Ina wakaazi wengi kuliko Mbeya.
Na kutokana na elimu kwa ujumla kuwa chini Magharibi mwa Tanzania kilingana na idadi ya wakazi wake, wenzetu wana zaana sana. na wana zungumza karibu lugha moja au inayofanana sana, ukiondoa sehemu chache kama Kagera na Dodoma.
2015 - TULIPIGWA TUU NA HATA TUNG'AN'GANIE UPINZANI, 2020 WATATUPIGA TENA SAFARI HII.