Dkt. Charles Kimei: Samia amefanya makubwa Vunjo

Dkt. Charles Kimei: Samia amefanya makubwa Vunjo

Alizopata tangu akiwa CEO CRDB na mali chungu nzima alizonazo lakini bado haridhiki anahangaika kutaka kupewa tena ubunge ??
Actualy hakuwa na moango wa kuwa politician, mwendazake ali force ila amfanye waziri wa fedha, bahati mbaya akatanglia, sasa kimei amebaki ana hang

No offense huyu mzee bado ana hela hata before siasa
 
Huwa nawashangaa wananchi wa vunjo eti walimchagua huyu kimei🚮
Unamfananishq kimei na mbatia?au Kimei na yuke mpuuzi wa chadema toka uru eti anataka kuwa mbunge wa Vunjo.
 
Hili zee sijui nani alilishauri liingie kwenye siasa..mvuto halina,vivu
 
Mbunge wa Jimbo la Vunjo Mheshimiwa Dkt Charles Stephen Kimei ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwa imeendelea kuwekeza kwenye miundombinu ya vifaa vya uchunguzi na vifaa tiba katika kuboresha huduma kwenye vituo vya kutolea huduma za afya hapa nchini ikiwemo Jimbo la Vunjo.

Ambapo katika kipindi cha miaka takribani minne Jimbo la Vunjo limenufaika kwa kupata mashine ya ultrasound, mashine mpya ya kisasa ya kutolea huduma za kinywa na meno, digital X -Ray na gari la wagonjwa. Kituo cha Afya Himo kitaanza kutoa huduma ya X - Ray baada ya taratibu za ukaguzi toka tume ya mionzi kukamilika.

Aidha, Serikali imeendelea kuboresha huduma za afya ya msingi katika Jimbo la Vunjo kwa kujenga zahanati na vituo vya afya ikiwa ni kuweza kufikia azma ya kumuwezesha mwananchi kupata huduma za afya ndani ya kilomita 5 toka kwenye makazi yake ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM 2020 - 2025.

Ameongeza kuwa katika kipindi kifupi Jimbo la Vunjo limeshuhudia mabadiliko makubwa kuanzia sekta ya elimu, Afya, Maji Safi, miundombinu ya barabara na umwagiliaji, umeme na ufugaji ikiwa ni dhamira na upendo wa dhati wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.

Dkt Kimei amesema ni kazi nzuri ya maendeleo iliyofanyika kila kona katika Jimbo la Vunjo ambayo itakua nyenzo muhimu ya kukipa ushindi Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi wa serikali za mitaa Novemba 27, 2024.

#VunjoTumechagua
#CCMTeamMaendeleo
#MaendeleoKwaVitendo
#TeamMaendeleo
#HatunaMbadala2025
#KaziIendelee
Aseeeh! Kimei hata wewe umegeuka kuwa Chawa!
Wewe ni mbunge
. Tukuulize zile millioni 500 mnapewa za kusaidia jimbo uliweka kwa mfuko wa nyuma au! Duuh kweli bado tunayo safari ndefu!
Wananchi wa Maeneo mengi tumeona wanajitolea wenyewe kutengeneza mabarabara kwa gharama zakwao wakati TARURA wapo! Leo tunaelekea chaguzi ndio mambo ya hovyo kama haya!
 
Kwani wewe Kimei umefanya nini kama yote amefanya Raisi?
Uchaguzi ujao kaa pembeni wenye uwezo wafanye kazi kwani wewe umeungama hukufanya kitu!
 
Back
Top Bottom