Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
WAZIRI DKT. DAMAS NDUMBARO AMEJADILI MCHAKATO WA KATIBA MPYA NA TAASISI ZA DINI MBALIMBALI
Waziri wa Katiba na Sheria, Mheshimiwa Dkt. Damas Ndumbaro amekutana na kufanya mazungumzo na Uongozi wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania na Uongozi wa Jumuiya ya Mabohora Tanzania tarehe 13 Mei, 2023 jijini Dar es Salaam.
Mhe. Dkt. Ndumbaro amepata wasaa wa kujadili masuala mbali mbali yakiwemo masuala ya Mchakato wa Katiba Mpya, Marekebisho ya Sheria ya Ndoa na Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia “Mama Samia Legal Aid Campaign”.
Katika mazungumzo hayo uongozi wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania uliongozwa na Mufti na Shekh Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakari Zuberi na upande wa Jumuiya ya Mabohora uliongozwa na Sheikh Taiyebali Patanwala, Mwakilishi Mkazi wa Jumuiya hiyo na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Mabohora nchini Tanzania.
Aidha, Waziri wa Katiba na Sheria, Mheshimiwa Dkt. Damas Ndumbaro ameshiriki Mkutano Mkuu wa Chama cha Mawakili Tanganyika tarehe 11 Mei,2023 jijini Arusha katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Arusha. Mkutano huo umefunguliwa na Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.