Dkt. Dorothy Gwajima: Kama unataka nitumbuliwe ili uchukue nafasi yangu, fanya kazi zaidi yangu sio ufitini

Tafuta wewe clips ndefu zaidi uwaonyeshe watu
Kitu ambacho atujaonyeshwa kwenye hizi clips hadi yeye kujitapa; ni auditing skills alizotumia hadi kubaini uongo waliotaka kumletea.

Ndio maana huwa anasema angekuwa mtu mwingine si wangemribuni kirahisi ila sio yeye wakajipange.
 
Dorothy mitano tena endelea tu mama kuropoka wewe wajua kila kitu cha Afya Angalia .....ushirikiano wenzako unavuruga nao unaona sawa ? Au pia unaweza Fanya kazi alone ?? Nonsense
 
Hahahaa ukiumwa na wewe utanyoshwa na madaktari
 
Huyu mama inaonekana alikuwa na visasi sana na watu wa wizara aliyoitumikia kwa miaka mingi. Huko inawezekana alikutana na madaktari wakorofi, waongo, wezi, wanyanyasaji, wakabila, waopenda Tasnia ya afya, wavivu na wale waliokaribu na utawala na inawezekana walitumia ubabe kumnyanyasa ikiwemo kimgonga bila ridhaa yake Sasa amepenya na kuwa juu yao. Mimi ninamsifu kwa huo muhemko alio nao lkn namshauri awaone wale Kama wenzake iwapo anataka kudumu kwenye hiyo nafasi ya uwaziri..yaani aache visasi field mashall ni kiongozi mkubwa wa jeshi kule jeshini ndiko kwenye ushenzi wa kila aina lkn baada ya mafunzo mnamaliza tofauti na kuwa kitu kimoja. Sasa kama anatamani ufield mashall Basi aache visasi jeshini hakuna visasi.
 
Serikali kiwanda cha nyati cement wamefunga kiwanda Chao kwa ajili ya matengenezo.mpaka tarehe 5 mwezi wa 2.
Mmejiandaje na uhaba wa cement?
Pia Bei huku mitaani ni 16,000 kwa 15,000
Bado Ni moto
Mimi nanunua kwa shs 19000
 
Katika mawaziri wa ovyo ovyo waliowahi kuongoza wizara ya Afya, huyu mama ndio ovyo kupita wote.
Amekaa kiswahili swahili sana, ana maneno mengi tena ya ovyo ovyo halafu hana mbinu zozote za kiutendaji. Ni kama hajiamini vile kuwa anastahili kuwa waziri hivyo anajaribu kujitutumua ili aonekane. Poor lady.

Kwa maoni yangu, huyu mama hafai hata kuwa mfagizi wa zahanati.
 
Irene Uwoya angepewa iyo wizara angemzidi hata huto mama. Hivi ni kweli phd yake ni halali?
 
Hahahaa ukiumwa na wewe utanyoshwa na madaktari
Madaktari wanatunyoosha kila siku,wengi wanadharau siku nilimpeleka Bi mkubwa pale Amana tena usiku ana hali mbaya ila Kale kadktari kanachat na smartphone yake huku anatuuliza maswali yani hata hatuangalii mara atukolomee. Sema ndio hivyo inabidi uwe mpole ila unaweza ukawatia makofi bure.

Yani polisi na madoctor huwa hawataki kuguswa wanajiona wao ndio kila kitu.
 
Sasa hapo anasafisha au anachamba!?
Kila clip anaonekana akichamba wenzie na kuwadharau
Watu wanamlalamikia kwa kujifanya anajua kuliko mtu yeyote kwenye hio wizara
Anamdharau mpaka mtangulizi wake ummy kana kwamba hakuna alichofanya mpaka anakuja yeye
Inaonekana amezoea kuchambana huko vijiweni
Shame!
 
Imebidi mpaka nicheke, bora ulivyomjibu hivi huyo jamaa. Eti anasafisha😆😆
 
Kwa namna navyomuona hata hashauriki mgumu mgumu, naibu wake atapata tabu sana kuendesha wizara kama teammate
 
Wewe nawe ni kama mpambe nuksi tu huna lolote, kwanza Kwa mishahara gani wanaolipwa madaktari na hizo posho wanazopata ukilinganisha na majukumu yao mpaka wanyoshwe, tuanze na maslahi yao kama watumishi wa umma kwanza ni vyema ifike mahali walimu, madaktari waangaliwe sana kwenye stahiki zao
 
Madaraka hayamuongezei mtu maarifa, ufahamu na hekima bali yanamfunua alivyo mjinga!
 
Serikali kiwanda cha nyati cement wamefunga kiwanda Chao kwa ajili ya matengenezo.mpaka tarehe 5 mwezi wa 2.
Mmejiandaje na uhaba wa cement?
Pia Bei huku mitaani ni 16,000 kwa 15,000
Bado Ni moto
Mafuta ya kupikia na baadhi ya nafaka zimepanda bei
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…