Mkuu hayo unayosema ni kama marudio tu hapa jukwaani. Kwa miaka mitano iliyopita tumuona fokafoka, tumbua tumbua, karipia karipia, kick kick na kila mbwembwe kwenye serikali zikigusa wizara zote, na tukaambiwa kwa style hiyo ufisadi umekwisha, utendaji wa mazoea umekwisha na maendeleo makubwa chini ya miaka mitano ya kwanza ya Magufuli!!
Sasa Leo hii akija waziri mpya na kusema huko serikalini (Kilimo, Afya nk) kumeoza sana inabidi tushangae na kujiuliza upya, nini kilitokea hapo kabla na yeye ana kitu gani kipya cha msingi cha kuweza kufanya ili kupambana na hayo. Bahati mbaya tunaona na yeye anakuja na blah blah zile zile, kick kick, ropoka ropoka na mikwara kibao.
Sasa waziri wa Afya wa sasa amekuwa mnyapara wa kuzurura na kuvamia vituo cha afya ili kuangalia kama kuna wizi wa panadol!
Upuuzi mtupu.