Dkt. Dorothy Gwajima: Kama unataka nitumbuliwe ili uchukue nafasi yangu, fanya kazi zaidi yangu sio ufitini

Dkt. Dorothy Gwajima: Kama unataka nitumbuliwe ili uchukue nafasi yangu, fanya kazi zaidi yangu sio ufitini

Bado namkumbuka mama mwenye zake hekima Mama Ummy Mwalim! Wizara ilimpenda, naye akaipenda.

Ummy Mwalimu alipwaya sana hapo, alikuwa hana mbele wala nyuma alikuwa anaburuzwa tu!!! Jiwe alifanya vizuri kumuondoa hapo!!! Kapelekwa kule kushuhulika na mazingira naona analala usingizi tu watu wanaharibu fukwe za Bahari kule Mbezi Beach kwa kujenga hovyo bila kuzingatia sheria!!
 
Kwa hiyo mnaiba dawa kwa kuwa wezi wako hata huko polisi?
Mh....wewe naona hoja zako ni dhaifu dhaifu ( In Prof Assad Voice).

Yaani umesahau kuwa waliotuhumiwa kuchota fedha za Escrow ni mawaziri.?Ndo maana nasema wizi upo kila mahali na ni kosa la jinai.

Majukumu ya waziri ni kutengeza sera nzuri na mifumo mizuri ya usimamizi ili dawa zimfikie mlaji wa mwisho na vile vile kuongeza morali wa kazi na ubunifu kwa mtoa dawa.
 
Wakuu habari za mchana.

Naomba walio karibu na huyu mama waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na watoto, wampe semina ya ku-behave kama top government official. Naona hilo linamshinda. Mama atulize ubongo aje na solutions. Aache majungu na malalamiko kila kukicha.

Hizi clip tunazoziona hazimpi heshima kabisa. Anajiita Field Marshall wa wizara lakini mimi namuona bado sana. Kama ana vinyongo na maumivu ya huko nyuma, asahau. Ajulishwe majukumu yake kama waziri. Aache kuleta viswahili kama vya vijiwe vya kina mama wakiwa peke yao.
Niliijua peke yangu nimeliona Hilo
Simjui vizuri lakini namuona kama anapenda kusutana
 
Kazi inaendelea
 

Attachments

  • IMG-20210117-WA0035.jpg
    IMG-20210117-WA0035.jpg
    50.9 KB · Views: 1
Wakuu habari za mchana.

Naomba walio karibu na huyu mama waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na watoto, wampe semina ya ku-behave kama top government official. Naona hilo linamshinda. Mama atulize ubongo aje na solutions. Aache majungu na malalamiko kila kukicha.

Hizi clip tunazoziona hazimpi heshima kabisa. Anajiita Field Marshall wa wizara lakini mimi namuona bado sana. Kama ana vinyongo na maumivu ya huko nyuma, asahau. Ajulishwe majukumu yake kama waziri. Aache kuleta viswahili kama vya vijiwe vya kina mama wakiwa peke yao.

Bora umeyatoa ya moyoni mkuu hope ataona hii post[emoji1666][emoji1666][emoji1666]
 
Wakati mwingine unakua innocent na huwezi kujitetea maana kuna chain ya events ambayo huwezi kuielezea ukaeleweka. kuna kipindi nikiwa kama mtumishi katika hospital X niliwahi kujievaluate na nikagundua kwamba kuna mambo mengi niliyafanya kwa nia nzuri lakini sio documents zote zilikaa sawa na isingewezekana kabisa zikae sawa na kama kuna mtu mkubwa angefuatilia vizuri na kuniuliza basi nisingekua na points nzuri za kueleweka bila kuonekana mwizi.
Unajua JF na hizi media zetu tia maji tia maji azitoi picha kamili wanafuta info za msingi na kuweka contents zitakazowapa YouTube views nyingi.

Jamaa wamedai hawana paracetamol tangia December mkuu wa wilaya kaenda mara kadhaa kuulizia kaambiwa hakuna; yeye alipoenda ndani ya dakika chache za kukagua makaratasi jamaa ikabidi wamwambie ukweli zipo box 30 kila box nadhani zinakaa mia.

Yeye akuridhika akataka wampeleke storage akaone akakuta kuna box 130 na hazi match na auditing trail. Baada ya kuona ivyo wakataka kumuongopea tena hao wagonjwa awakwenda kwao, akataka kuwaletea ushahidi wa mgonjwa.

Nadhani mpaka hapo unapata picha kwanini alikasirishwa na ndio akawaambia hawana huo uwezo wa kumdanganya wahusika wenyewe walikiri makosa na kuomba msamaha.

Sema clip nyingi zinaonyesha akijiita field Marshall tu lakini sakata zima lililopelekea kujiita ivyo ni media moja tu ndio imeonyesha. Na ndio sababu akasema nisingekuwa mtaalamu si ndio tayari mshanirushia changa la macho.
 
Mama anajitahidi na anamaono flan lakn aproach yake mbovu na kwa nchi hii ilivyo na kwa sekta hyo ilivyo kubalisha mambo ghafla been vuu ni ngumuuu...yalipo ndani ya sekta ni tofauti na jinsi watu wanaskia nje..afya na ulinzi ni sekta ambazo zinahitaji fedha sio kutishana wala kuumizana vichwa..kwanza wiz upo kila sehem koteee wiz upo..pili hicho kina
Chosemwa kimeibwa ukiambiwa haya hichi hapa hakikai hata siku 3 kinaisha maana demand ni kubwa mnoo..yan unataka watu waendeshe hosp za serekali kama zao [emoji16][emoji16] yani waumize vichwa namna ya kukusanya mapato badala waumize vichwa namna ya kutibu wagonjwa[emoji2303] serekali iweke hela na iweke utaratibu mzur wa kusimamia na waajiriwa wapige kazi wakiwa mawe relax sio Incharge anamgonjwa wa refferal anawaza mafuta anatoa wapi aisee
Na ole wako ukose mafuta upate mate Maternal death ndo utakuja kujua maharage nayo ni mbona.all in umezumgumz mambo ya msingi sana
 
Mkuu hayo unayosema ni kama marudio tu hapa jukwaani. Kwa miaka mitano iliyopita tumuona fokafoka, tumbua tumbua, karipia karipia, kick kick na kila mbwembwe kwenye serikali zikigusa wizara zote, na tukaambiwa kwa style hiyo ufisadi umekwisha, utendaji wa mazoea umekwisha na maendeleo makubwa chini ya miaka mitano ya kwanza ya Magufuli!!

Sasa Leo hii akija waziri mpya na kusema huko serikalini (Kilimo, Afya nk) kumeoza sana inabidi tushangae na kujiuliza upya, nini kilitokea hapo kabla na yeye ana kitu gani kipya cha msingi cha kuweza kufanya ili kupambana na hayo. Bahati mbaya tunaona na yeye anakuja na blah blah zile zile, kick kick, ropoka ropoka na mikwara kibao.

Sasa waziri wa Afya wa sasa amekuwa mnyapara wa kuzurura na kuvamia vituo cha afya ili kuangalia kama kuna wizi wa panadol!
Upuuzi mtupu.

Sasa hivi wanafanya kazi kama vile uongozi wa 2015-2020 ulikuwa ni awamu tofauti.
 
Mama msamba sana yule na hana swaga za kiongozi. Alitakiwa kuwa na funzo zito kutoka kwa Ummy
 
Huyu mama anatia aibu. Anakera kumuangia hata kumsikiliza....shida yake ni nini?
 
Kwenye Afya kuna madudu mengi, ngoja awachambe hao. Ukiumwa ukaenda kwenye hizi hospitali zetu ndo utajionea kero za huko.
Namuunga mkono.
 
Sekta ya Afya ni Sekta nyeti sana na in Sekta ambayo Serikali na wafadhili mbalimbali wamekua wakinwaga mifedha mingi ajabu ni Fedha nyingi sana zimepigwa na viongozi wa Sekta hiyo yani ma DMO na MaDED... Ukieenda saivi ktk hospital za Serikali yan Vituo vya Afya,Zahanati na Hospital za Wilaya huwezi amini HAKUNA MADAWA zaidi ya Diclopa,Aluu na Dawa za kuharisha... ma Dr wengi wameiba sana hadi kufungua Dispensary zao na Pharmacy zao... Dr Gwajima amekua Tamisemi upande wa Afya anaijua fika Sekta hii... Tusimkatishe Tamaa aendelee kutumbua plus kuwafokea maana wameiba vyakutosha
Kwa hiyo unamainisha Mtu akiwa Dr Au Pharmacist hawezi kuwa na mtaji wa kununua dawa zake za kuuza mpaka aibe au, nimegundua watu wengi sana wako obsessed na watumishi wa afya kuliko uhalisia, hivi unaanzaje kuuza dawa iliyoandikwa MSD, ukizeeka lazima uwe mchawi wewe
 
hata kama mnamcriticize sio hivi,kumdogolesha tu mama wa watu..sijui mnapata nini
 
Acheni wizi wa dawa mtamuelewa tu, Mh ni mtendaji sio mwanasiasa,
Kuna Mh Aweso anawanyoosha wahandisi feki, miradi mikubwa ya maji mbona hamuongelei!
Serikali inanunua madawa lakini mahospitalini hayapo..NI WIZI WIZI WIZI TU..!

Hahahaa eti serikali inanunua dawa! hii sekta ina changamoto sana hajui lolote kaa kimya.
 
Hapana wewe ndiye una upungufu wa uelewa. Pamoja na mapungufu yaliyopo ya eekta ya afya, ila kulikuwa na wizi sana na mlizooea kuiba mno na kutoa huduma mbovu bila kujua wajibu wenu. Acha awanyooshe kabisa mlijijaza uzembe. Kikubwa mfano wa kuacha kutumia GOT HOMIS sekta ya afya inaibiwa mno. Pia waziri huyu anayo dhamira ya kazi toka moyoni mwake. Labda lile tukio la mkunga ndiyo linahitaji busara juu yake.
Unajua hawa watumishi wa afya walizoea kuiba dawa, kuua vifaa vya tiba, kunyanyasha wagonjwa, uzembe, nk, na wakaona hiyo ni haki yao. Sasa kaja mtu anayeijua system ya afya kwa undani na anaweza kuwaumbua kwa uovu wao, wanamwona ni mnoko.
Dawa kwao ni kubadilika na kufanya kazi kwa kufuata maadili ya kazi zao.
 
Back
Top Bottom