Dkt. Dorothy Gwajima ndiye waziri anayekubalika kwasasa nchini Tanzania

Dr. Gwajima ni waziri wa wanawake, jinsia nk, tena jinsia yake ni ya kike, lakini mpaka leo ameshindwa kujitokeza hadharani kushinikiza kukamatwa kwa yule Kigogo wa Polisi aliyehusishwa na mpango wa kupeleka wanaume wa kulawiti yule binti wa kule Yombo.
Dr. Gwajima ameshindwa hata kulaani tamko la kamanda wa Polisi wa Dodoma aliyetaka kuifunika ile issue.

Kwangu mimi Dr. Gwajima nimemuona wa ovyo mnoo kupitia hili sakata la Yombo.
 
upo sahihi mkuu ila pendekezo lako la awe waziri wa Mambo ya ndani kwa ukweli wake na kupenda kwake haki bila uonevu mara zije amri toka juu za hao wazee wa kazi zita mchafulia tu CV yake nzuri..kwa waziri mtendaji na mfuatiliaji kama huyu mama mm naona ni bora sana akiwa WAZIRI WA TAMISEMI panahitaji waziri dizaini ya huyu mama..
 
Ni mfuatiliai na mtekelezaji mzuri
 
Ukimsifia kiongozi wa kiafrika ndio umeharibu kabisa.

Anyway, kutuambia uwezo wake akiwa hai pia Si jambo baya, Abarikiwe.
 
Anachapa kazi, hongera kwa mama Dorothy, Tangu kile kipindi cha corona alikuwa makini.
 
Mara ya kwanza wakati ameingia kwenye jukwaa alikutana sana na upinzani, kebehi toka kwa wadau mbali mbali, lakini busara zake na ufuatiliaji kiukweli vimemfanya akubalike mno .. tunachomuombea tu asije kubadilika kama ilivyozoeleka ..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…