Dkt. Dorothy Gwajima ndiye waziri anayekubalika kwasasa nchini Tanzania

Dkt. Dorothy Gwajima ndiye waziri anayekubalika kwasasa nchini Tanzania

Dr. Gwajima ni waziri wa wanawake, jinsia nk, tena jinsia yake ni ya kike, lakini mpaka leo ameshindwa kujitokeza hadharani kushinikiza kukamatwa kwa yule Kigogo wa Polisi aliyehusishwa na mpango wa kupeleka wanaume wa kulawiti yule binti wa kule Yombo.
Dr. Gwajima ameshindwa hata kulaani tamko la kamanda wa Polisi wa Dodoma aliyetaka kuifunika ile issue.

Kwangu mimi Dr. Gwajima nimemuona wa ovyo mnoo kupitia hili sakata la Yombo.
 
upo sahihi mkuu ila pendekezo lako la awe waziri wa Mambo ya ndani kwa ukweli wake na kupenda kwake haki bila uonevu mara zije amri toka juu za hao wazee wa kazi zita mchafulia tu CV yake nzuri..kwa waziri mtendaji na mfuatiliaji kama huyu mama mm naona ni bora sana akiwa WAZIRI WA TAMISEMI panahitaji waziri dizaini ya huyu mama..
 
View attachment 3075064


Nsikuchoshe na Usinchoshe, Tusichoshane!


Kwanza kabisa nipende kukiri hadharani ya kwamba,Binafsi huyu ndiye waziri ninaye mkubali Kwa Sasa nchi Tanzania.

Huyu waziri anazosifa kadhaa ambazo zinamfanya aendelee kukubalika Kwa Watanzania kibwena.

SIFA ZINAZOMFANYA KUPENDWA NA WATANZANIA WALIO WENGI


1.Ni mzuri wa Sura na Umbo (Uzuri wake unaendana na Roho yake nzuri)

2.Siyo mtu wa kujikweza

3.Siyo mtu wa dharau kama walivyo mawaziri wengine

4.Mpenda haki

5.Siyo mtu wa hasira za Kijinga

6.Anapenda kusikiliza kila mtu (Ukipitia kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii unakuta anajibu komenti za wananchi Kwa upole na nidhamu ya hali ya juuu,hata kama ukiwa umekwazika utashusha hasira zako)

7.Anachukia sana uovu na Uonevu

8.Ni mtu ambaye madaraka hayajamfanya akengeuke kama mawaziri vishoka wengine!

9.Siyo mtu wa kuongea ongea sana Bali ni mtendaji sana kitu amabacho kinafanya kazi zake ziongee sana kuliko Mdomo wake kama walivyo mawaziri wengine wapiga zomari

Yaani kiukweli nikiamua kuziweka hapa Sifa zake ni nyingi mno,itoshe kusema hapa Rais Samia alitutendea haki watanzania.


Ningekuwa Rais Samia au Mshauri wake,nadhani huyu angetufaa Kuwa WAZIRI WA MAMBO YA NDANI


Nadhani pia ukarimu wake na hofu ni matokea Bora ya kumuabudu Mungu,huyu mama anamuabudu Mungu katika roho na kweli,siyo kama waigizaji wengine walioko kwenye Baraza la mawaziri.



Hongera sana Mh Dkt. Gwajima D
Ni mfuatiliai na mtekelezaji mzuri
 
Ukimsifia kiongozi wa kiafrika ndio umeharibu kabisa.

Anyway, kutuambia uwezo wake akiwa hai pia Si jambo baya, Abarikiwe.
 
Anachapa kazi, hongera kwa mama Dorothy, Tangu kile kipindi cha corona alikuwa makini.
 
Mara ya kwanza wakati ameingia kwenye jukwaa alikutana sana na upinzani, kebehi toka kwa wadau mbali mbali, lakini busara zake na ufuatiliaji kiukweli vimemfanya akubalike mno .. tunachomuombea tu asije kubadilika kama ilivyozoeleka ..
 
Back
Top Bottom