Dkt. Dorothy Gwajima ndiye waziri anayekubalika kwasasa nchini Tanzania

Dkt. Dorothy Gwajima ndiye waziri anayekubalika kwasasa nchini Tanzania

Ni yule ambae alibanwa na hoja nyepesi bungeni akashindwa kuijibu na kuanza kulia kisanii ?
 
Ni yule ambae alibanwa na hoja nyepesi bungeni akashindwa kuijibu na kuanza kulia kisanii ?
Kujibu maswali bungeni sio utendaji Kuna wabunge na mawaziri ni mahodari ila ukija kwenye utendaji ni ovyo kabisa
 
Huyu Bi Mkubwa ni mfano wa kuigwa kwa Mawaziri na viongozi wanawake wana takiwa wajifunze kwake.
 


Nsikuchoshe na Usinchoshe, Tusichoshane!


Kwanza kabisa nipende kukiri hadharani ya kwamba,Binafsi huyu ndiye waziri ninaye mkubali Kwa Sasa nchi Tanzania.

Huyu waziri anazosifa kadhaa ambazo zinamfanya aendelee kukubalika Kwa Watanzania kibwena.

SIFA ZINAZOMFANYA KUPENDWA NA WATANZANIA WALIO WENGI
1. Ni mzuri wa Sura na Umbo (Uzuri wake unaendana na Roho yake nzuri)

2. Siyo mtu wa kujikweza

3. Siyo mtu wa dharau kama walivyo mawaziri wengine

4. Mpenda haki

5. Siyo mtu wa hasira za Kijinga

6. Anapenda kusikiliza kila mtu (Ukipitia kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii unakuta anajibu komenti za wananchi Kwa upole na nidhamu ya hali ya juuu,hata kama ukiwa umekwazika utashusha hasira zako)

7. Anachukia sana uovu na Uonevu

8. Ni mtu ambaye madaraka hayajamfanya akengeuke kama mawaziri vishoka wengine!

9. Siyo mtu wa kuongea ongea sana Bali ni mtendaji sana kitu amabacho kinafanya kazi zake ziongee sana kuliko Mdomo wake kama walivyo mawaziri wengine wapiga zomari

Yaani kiukweli nikiamua kuziweka hapa Sifa zake ni nyingi mno,itoshe kusema hapa Rais Samia alitutendea haki watanzania.

Ningekuwa Rais Samia au Mshauri wake,nadhani huyu angetufaa Kuwa WAZIRI WA MAMBO YA NDANI

Nadhani pia ukarimu wake na hofu ni matokea Bora ya kumuabudu Mungu,huyu mama anamuabudu Mungu katika roho na kweli,siyo kama waigizaji wengine walioko kwenye Baraza la mawaziri.

Hongera sana Mh Dkt. Gwajima D
Kiukweli huyu mama anafaa kabisa kuwa hata Waziri Mkuu.
 
Na ndio inapaswa kiongozi kuwa karibu na watu wake, ukaribunna raia ndo utajua Nini wanachi wanataka sio kiongozi unataka... Citizen voice is national voice cause are ones with needs not leaders 😊
Exactly 💯
 
Kujibu maswali bungeni sio utendaji Kuna wabunge na mawaziri ni mahodari ila ukija kwenye utendaji ni ovyo kabisa

Aaah wapi !
Nendeni kajipangeni upya ktk kumfanyia huo uchawa wenu.
Hatudanganyiki
 
Back
Top Bottom