Dkt. Elisha Osati anaenda kuongelea hali ya Covid 19 Tanzania kama nani?

Dkt. Elisha Osati anaenda kuongelea hali ya Covid 19 Tanzania kama nani?

jingalao

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2011
Posts
36,197
Reaction score
29,717
Nimeona Tangazo kwenye jumbe za watsapp ikionesha kuwa kitakuwa na mjadala kuhusu wimbi la tatu la corona nchini Tanzania.

Katika mjadala huo nimeona mwenyekiti wa MAT pamoja na Mwenyekiti aliyemaliza muda wake.

Ieleweke kuwa kujadili covid sio tatizo ila ni muhimu pia sheria tulizojiwekea zizingatiwe.

Yaani linapokuja suala la mlipuko wa magonjwa wapo wasemaji sahihi kuhusu hilo. Hata ngazi ya kimataifa tuna Director General Dr Tedros ambaye anayo mandate ya kuongelea situation ya ugonjwa wa covid duniani na si mwingine.

Sasa nimeshangaa kuona kwenye ratiba kuna Dr Elisha Osati (mgombea ubunge jimbo la Temeke aliyekatwa na wajumbe wa CCM) ambaye inasemekana ataongelea covid 19 situation in Tanzania katika kikao cha zoom tarehe 22 mei 2021.

Ikumbukwe kikao hiki hakina mshiriki kutoka serikalini ambaye atasimama kama mtoa mada.

9.-{1) The Minister, in consultation with the authorized officer, shall notifY the public by a publication in the local newspaper circulating in the area notice boards on the area or any other method which may be considered fit on the occurrence, existence of any infectious, communicable and non-communicable disease prescribed in the First. Schedule to this Act(PUBLIC HEALTH ACT 2009)

Kwanini mnataka kutulazimishia wimbi la tatu ili wapendwa wetu wapotee?
 
Kama mtaalamu wa afya,ambae pia anahusika na tiba ya moja ya sehemu kuu inayoathiriwa na huo ugonjwa,kukusaidia tu enzi za siasa kwenye taaluma zimepitwa na muda.Hivyo hayo matamanio yako yamepitwa na muda.
Taaluma inamtaja mhusika wa kuzungumzia magonjwa ya mlipuko Tanzania.
 
Chanjo bado zipo kwenye majaribio.
Nchi kama Seychelles imechanja watu almost nchi nzima, ila imethibitika waliochanjwa wanaambukizwa tena.

Kuna chanjo mbili maarufu zinazoletwa Africa zinaonekana kuwa na madhara,

Je, namuuliza Mh Samia,
Daladala atatangaza level seat? Au tutabanana kama dagaa...

Je, kariakoo na mabaa atatangaza kuvifunga? Au tutajazana tu.

Je, magari ya Mwendokasi tunapojaa hadi milango haifungi, ataanzisha level seat?!

Je, viwanja vya mpira atazuia mashabiki?

Je, sherehe kama harusi, zitarudi kuwa za watu ishirini?!

Je, nani atasimamia uvaaji wa barakoa kila sehemu?!

Au hayo yote mtapuuzia halafu mseme Chanjo!!!

Kwa nini muwe makuwadi wa Chanjo?!

In fact, wanaotaka si wakachanje kama mh aliyechanjwa kule Dubai.

Mama Samia, unalitaka usilolijua na itakuwa ni maigizo, na kupigia chapuo biashara za chanjo tu.
 
Huyu Osati ana kimbelembele sana kwa wasiomjua watapata shida sana.

Hilo wimbi la tatu lipo wapi?...nani kamtuma?..huyu mjaluo ana matatizo sana.

Kwanza amesharudisha kadi ya chadema?
 
Kama mtaalamu wa afya, ambae pia anahusika na tiba ya moja ya sehemu kuu inayoathiriwa na huo ugonjwa,kukusaidia tu enzi za siasa kwenye taaluma zimepitwa na muda. Hivyo hayo matamanio yako yamepitwa na muda.
9.-{1) The Minister, in consultation with the authorized officer, shall
notifY the public by a publication in the local newspaper circulating in the
area notice boards on the area or any other method which may be
.considered fit on the occurrence, existence of any infectious,
communicable and non-communicable disease prescribed in the First
Schedule to this Act

Hivi kila mtaalamu wa tiba akitoka kuiongelea covid 19 situation in Tanzania kutakalika?
Elisha amefanya utafiti wowote kuhusu covid 19 in Tanzania?wapi amepublish?
 
Huyu Osati ana kimbelembele sana kwa wasiomjua watapata shida sana.
Hilo wimbi la tatu lipo wapi?...nani kamtuma?..huyu mjaluo ana matatizo sana.
Kwanza amesharudisha kadi ya chadema?
Kwa kawaida mwenye kimbelembele hawezi kujitambua mwenyewe,yaweza kuwa wewe ndiye mwenye kimbelembele.
 
9.-{1) The Minister, in consultation with the authorized officer, shall
notifY the public by a publication in the local newspaper circulating in the....
Tupatie ufafanuzi wa hiyo act kwakutuwekea hapa kwa ufasaha utichambue wenyewe.ni act gani hasa.
 
Waache watu watoe mawazo yao

Ova
Hakuna anayemzuia....ila siku zote kiherehere kina gharama yake.....Mh Rais kashapokea mapendekezo kutoka kwenye tume.....sasa kama yeye ataongea kwa niaba ya serikali sawa....
 
9.-{1) The Minister, in consultation with the authorized officer, shall
notifY the public by a publication in the local newspaper circulating in the...
Hii imfikie ikiwezekana.
Anataka kuwa limbukeni wa medicine.
 
Chanjo bado zipo kwenye majaribio.
Nchi kama Seychelles imechanja watu almost nchi nzima, ila imethibitika waliochanjwa wanaambukizwa tena...
Maswali mengi kuliko majibu wanakoisha na corona wameanza kuwaachia watu wao na barakoa si lazima tena,mashabiki wanaonekana hawajavaa barakoa.

sisi huku ndo viongozi wanakuja kwa mwendo kasi kila sehemu wakuu wamevaa barakoa,watangaze sasa corona imeingia nchini.
watutangazie visa hewa,na kuwekwa wasemaji kama hawa huku wakijua ni wanufaikaji na chanjo hizi.

Hatuhitaji wasemaji kutushawishi maana tunaujua ukweli haipo,maana hatujaona watoto wetu wanaojaa madarasani wakikanyagana wakianguka sababu ya kushindwa kupumua.

kama mna mpango wa kuleta corona ileteni tu ila mjue Mungu yupo.
 
Back
Top Bottom