Pre GE2025 Dkt. Emmanuel Nchimbi ateuliwa kuwa Katibu Mkuu mpya wa CCM kumrithi Daniel Chongolo

Pre GE2025 Dkt. Emmanuel Nchimbi ateuliwa kuwa Katibu Mkuu mpya wa CCM kumrithi Daniel Chongolo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hata dr Lawrence Gama ametokea Ruvuma.
Kwahiyo mkoa wa Ruvuma pekee umetoa makatibu wakuu wa CCM watatu.

Hata hivyo ukanda na ukabila havipo tena, ndiyo maana kanda ya Kaskazini imefanikiwa kutoa PM 4 . Mkoa mmoja wa Arusha kabla haujagawanywa umetoa PM 3. Yote yanawezekana na haijawahi kuwa tatizo kwenye nchi yetu
Ni kweli kabisa
 
Hapo naungana na wewe.Huyu jamaa ana fitina yuko tayari akuondoshe duniani. Amina Chifupa nyota ilipong'ara, Nchimbi alimfitini mno binti wa watu. Ipyana aliposhinda UVCCM ,Nchimbi hakukubali kushindwa. Ipi alikufa kwa mazingira ya kutatanisha. MAKONDA ACHUNGE SANA YAANI. AKIMZIDI JAMAA UMAARUFU TU,BAASII,. HATA CHAI PALE LUMUMBA ASINYWE.
Mpika chai wake Mwita Waitara alimkimbia akaenda Chadema! Sasa sijui wataelewana tena?
 
Hiki cheo naona ni mahsusi kwa watu wa kusini na nyanda za juu kusini,Iringa ikiwa kinara.Hebu angalia orodha hii:-
1.Rashid M Kawawa - Ruvuma
2. Horace Kolimba - Iringa
3. Philip Mangula - Iringa
4. Daniel Chongolo - Iringa
5. John Nchimbi - Ruvuma
Msekwa
Mukama
Bashiru
 
Makundi ni Msoga sukuma na la visiwani,hayo kwa sasa ndio yana run.
Hayupo miongoni mwao.
Kundi la Lowassa ni kikundi ndani kundi la "mtandao."
Baada ya joto la uchaguzi wa mwaka 2015 na yale yaliyotokea baada ya uchaguzi kundi hilo limerudi/ limerudishwa kundini ili kuimarisha ""mtandao",
 
Nilikua namaaanisha makundi haya yalio active kwa sasa mkuu.

Kundi la mzee wa bwagamoyo halijawahi kufa mkuu, hilo kundi ndio pingili za chama na pengine nchi, wana nguvu hatari...

Kuna raia wao sio wanasiasa lakini ndio vinara wa kutoa dira na mwelekeo wa nani awe juu na nani afuate...
 
Mmmh! Siasa zinaenda kupita kipindi kigumu. Chadema pangeni upya safu ya viongozi, bila ukorofi wa Dr Slaa, Jeuri ya Lissu, akili ya Mnyika, ubabe wa Mbowe, hekima za Prof Baregu na harakati za MM Mwanakijiji kutoboa ni ngumu.
Niliwashauri kumrudisha Dr Slaa, Bado wanasuasua.
 
Kundi la mzee wa bwagamoyo halijawahi kufa mkuu, hilo kundi ndio pingili za chama na pengine nchi, wana nguvu hatari...

Kuna raia wao sio wanasiasa lakini ndio vinara wa kutoa dira na mwelekeo wa nani awe juu na nani afuate...
Sijui nitakuwa sifahamu vizuri .
KM watu huyu alikua team ya safari ya matumaini. Ambayo ilihitimishwa 2015 timu yote ikasambaratika na wengine wakaunga mkono juhudi na wengine wakapotea moja kwa moja akiwepo na huyu wa leo.

Timu ya watoto wa mjini wakawa wapo kwenye ligi na timu ya bush iliyokua ina run , timu bush ikapata mushkel ikatolewa kwenye reli, kwa mbali ama nyuma ya timu ya watoto wa mjini wakawa wana run nadhani mpaka sasa , kumezaliwa pia timi ya visiwani nayo inataka kuitoa timu ya watoto wa mjini washike haramu wao moja kwa moja, bado timu ya bush hawakubaliani na kilicho tokea kwa hiyo tuna timu tatu zinazopambana ambazo zote New KM hayupo.
Nisahihishwe tafadhali.
 
Mmmh! Siasa zinaenda kupita kipindi kigumu. Chadema pangeni upya safu ya viongozi, bila ukorofi wa Dr Slaa, Jeuri ya Lissu, akili ya Mnyika, ubabe wa Mbowe, hekima za Prof Baregu na harakati za MM Mwanakijiji kutoboa ni ngumu.
Umenikumbusha mbali mkuu, sijui kama hii jana inaweza kurudi tena leo.
 
Kundi la Lowassa ni kikundi ndani kundi la "mtandao."
Baada ya joto la uchaguzi wa mwaka 2015 na yale yaliyotokea baada ya uchaguzi kundi hilo limerudi/ limerudishwa kundini ili kuimarisha ""mtandao",
Ohhoo! Nilikua sifahamu hili, na pia kama ni hivyo kweli ni hivi karibuni limekusnywa na kurudishwa kwenye line kupitia mgongo wa hilo la mtandao! timu lowasa ilipotezwa kabisa kipindi kile cha mwendazake, waliosalia waliunga mkono juhudi, waliopona kama wakini Emma kutoka na stutus yao waliwekwa sehemu laini mbali na mfumo ndio wakaibuliwa leo.
 
Back
Top Bottom