Pre GE2025 Dkt. Emmanuel Nchimbi ateuliwa kuwa Katibu Mkuu mpya wa CCM kumrithi Daniel Chongolo

Pre GE2025 Dkt. Emmanuel Nchimbi ateuliwa kuwa Katibu Mkuu mpya wa CCM kumrithi Daniel Chongolo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Nchimbi atakuwa anajiona kama ‘king maker’ kwa sasa ndani ya Tanzania (he is entitled to, you can’t blame him).

Imagine mtu amefanya siasa zake mpaka amechoka mwenyewe, ameachia jimbo ambalo hakukuwa na mtu wakumsumbua angelitaka ata uchaguzi ujao.

Nchimbi mwenyewe kwa utashi wake ameaga hadharani viongozi wa CCM, umma wa Songea mjini (akawapa na bus team ya maji-maji), akaaga na watanzania 2015 jamani mimi kwa ridhaa yangu siasa basi tena nataka kufanya shughuli zingine za maisha.

Mara uoga wa Magufuli aamini uwepo wa Nchimbi anaona nguvu yake ya fitna inaweza mletea shida katika uongozi wake, solution tumtoe nje ya nchi na ubalozi.

‘Bi Tozo’ nae uoga 2025 wanaweza niletea fujo wakaninyan’ganya tonge tumrudishe Nchimbi anisaidie.

Nchimbi mwenyewe walaah, alishasema toka 2015 mimi basi tena, wenyewe wanajipendekeza kwa kumuhofia, sure anayo haki ya kujiona ‘king maker’ kwa sasa and you can’t blame him.
 
Ohhoo! Nilikua sifahamu hili, na pia kama ni hivyo kweli ni hivi karibuni limekusnywa na kurudishwa kwenye line kupitia mgongo wa hilo la mtandao! timu lowasa ilipotezwa kabisa kipindi kile cha mwendazake, waliosalia waliunga mkono juhudi, waliopona kama wakini Emma kutoka na stutus yao waliwekwa sehemu laini mbali na mfumo ndio wakaibuliwa leo.
Kuna mengi yanaendelea kwenye makundi ya CCM ila tuachane nao tujenge taifa letu
 
Nchimbi atakuwa anajiona kama ‘king maker’ kwa sasa ndani ya Tanzania (he is entitled to, you can’t blame him)...
"Mwanasiasa amini jina lake na salaam yake tu"---- Zitto Kabwe.

Hakuna mwanasiasa anayestaafu kwenye umri wa miaka 40 au 50.
Hilo lingewezekani basi mzee Mangula asingerudi siasani mwaka 2012 hasa baada ya utumishi wake uliotukuka kama Katibu Mkuu CCM kwa miaka 10.

Lakini kwakuwa siasa ni tamu mzee Mangula amerudi kutumikia chama chake akiwa na umri wa miaka 71.
Kama ilivyo kwa Kinana pia kwa Msekwa

Nchimbi alijiweka pembeni baada ndoto zake za kuamini ushindi wa Lowassa ndani ya CCM kuzimwa.
Ulikuwa upepo mbaya wa kisiasa, umeshapita, naye amerejea.
 
Namshauri akimbize hicho kijiti alichopewa kwa hadhari kubwa. Atambue kuwa huo unaweza kuwa mtego kwake wa kummaliza kisiasa. Be care
 
WASIFU WA DKT. EMMANUEL NCHIMBI
Elimu yake ya Msingi aliianzia jijini Dar es Salaam katika Shule ya Msingi Oysterbay kati ya mwaka 1980 – 1986.
Mkuu Sir John Roberts , asante kwa wasifu huu, kumbe mimi ni kaka yake, wakati yeye anaanza darasa la kwanza, sisi tulikuwa darasa la 5!, Dr. Mwinyi darasa la 7!. Hata Maria Sarangi ni dada yake alikuwa darasa la 3!.
Dk Nchimbi amemuoa Jane na wana watoto watatu.
Jane ni miongoni mwa wanafunzi wa shule ya sekondari ya Zanaki waliotembelea RTD early 90s wakati huo mimi ni mtangazaji wa external service, ndio ilikuwa redio pekee ya Kiingereza hapa Bongo. Hivyo namfahamu Dr. Nchimbi ni mdogo wangu kabisa wa shule, shemeji pia nimemfahamu toka akiwa Zanaki, hivyo I can reach him dakika sifuri na kunipeleka kwa Mama!, hivyo wale mnaodhani naandika ili kukaa karibu na waridi na mimi ninukie, endeleeni kudhania, hili waridi sasa ni letu!.
Dr. Emmanuel Nchimbi is the right man in a right place at the right time!.
Tena 2015 tuliwahi kumdhaniaga
Is It Possible, Mgombea wa CCM kwa 2015 ni Nchimbi?!. Yule "Jamaa Yangu" ni "Yohana Mbatizaji Tu?!., hivyo uteuzi huu sasa ni wa kupiga ndege wawili kwa jiwe moja la 2025 or 2030 haswa kwa kuzingatia hii ni 'Kurasini'!.

Hongera Sana Dr. Emmanuel Nchimbi.
P
 
Uchaguzi wa 2025 inaelekea unaanza kutake shape.
Inaelekea mama Samia inaelekea ameamua kwenda uchaguzini na kundi la mzee Lowassa katika uchaguzi ujao.
Nchimbi atakumbukwa kuwa ni mmoja wa walioimba "tuna imani na Lowassa, oyaaa...oyaaa...oyaaa..!

View: https://youtu.be/xAq-winQLtU

Nchimbi vile vile alipinga vikali kukatwa jina la Lowassa katika kinyang'anyiro cha uchaguzi wa mwaka 2015.
Kitendo hiki ndicho kilimwingiza Mgufuli madarakani.

View: https://youtu.be/vX_orcX9k2Y

Sasa ni zamu ya kundi la JK kutupa karata yake uwanjani.
 
Back
Top Bottom