TANZIA Dkt. Faustine Ndugulile, aliyekuwa Mbunge wa Kigamboni afariki Dunia

TANZIA Dkt. Faustine Ndugulile, aliyekuwa Mbunge wa Kigamboni afariki Dunia

Tanzia

View attachment 3162827

Spika wa Bunge Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb) anasikitika kutangaza kifo cha Mbunge wa Kigamboni, Mheshimiwa Dkt. Faustine Ndugulile kilichotokea usiku wa kuamkia leo tarehe 27 Novemba, 2024 nchini India alipokuwa akipatiwa matibabu.

"Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Mbunge wa Kigamboni na Mkurugenzi Mteule wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Kanda ya Afrika, Mheshimiwa Dkt. Faustine Ndugulile. Kwa niaba ya Wabunge natoa pole kwa familia, wakazi wa Kigamboni na Watanzania wote. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi", amesema.

Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na familia inaendelea kuratibu shughuli za mazishi na taarifa zaidi zitaendelela kutolewa.

BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA, APUMZIKE KWA AMANI.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano na Elimu kwa Umma,
Ofisi ya Bunge,
DODOMA.
27 Novemba, 2024
Mbona 27 Novemba, 2025 bado hatujafika??!!
 
Tumepoteza watu Wenye CV za kidunia

Tumebakiwa na Waigizaji watupu waliojibatiza kuwa wao ni chawa

Nikitoka hapa Kituo cha Kupigia KURA naelekea Kanisani direct

Ahsanteni sana

Yuko wapi Lucas Mwashambwa? 🐼
Hivi huyo Mafuru alikuwa mtanzania kweli? Mbona wasifu wake ulizua maswali!
Ndugulile, may his soul rest in peace.
Duniani tunapita tu
 
Duh,
Aliumwa lini? Tanzania yetu ina mambo

----

Huu utaratibu tuliojiwekea wa kutangaza kifo cha mtu tu bila kujali aliugua au ni ajali ni mbaya sana

Kwenye taarifa rasmi ya Bunge inaonesha kafariki 2025??? bahati mbaya?

Sasa jamii inabaki na mtanziko na sintofahamu kubwa..

1.Aliumwa
2 Kama aliumwa aliumwa nini na alianza lini?
3.Ajali?
4.Matibabu India ilikuwaje?
5.Chronic deaseases? Taarifa haisemi...

Ndungulile ni mtu mkubwa sana kuacha kujibu hayo maswali kwenye taarifa rasmi ya Kifo chake...

Tunaweza dhani ni jambo jema na privacy lakini minongono na 'umbea ' na 'siasa' zetu, ikatugharimu baadae...

Binafsi nilipenda sana hustle zake,

Poleni sana familia ya Dr. Faustine.

Pumzika kwa amani kaka.
"Kwenye taarifa rasmi ya Bunge inaonesha kafariki 2025??? bahati mbaya?"

Labda aliyeandika kakurupuka tu. La sivyo alipaswa aandike "atafariki" 27 Novemba, 2025 maana bado hatujafika!
 
Binadamu tunapenda sana kutafuta uhalali wa kwanini mwingine kafa, hii inatokana na woga wa kifo.

Tarehe ya leo Wapo wengi tu wa umri wa huyu ndugu na hata chini yake wameondoka. Tuache mambo ya kufikirika.

Kama hujui sema RIP endelea na maisha ukisubiri zamu yako siyo unaanza kubuni buni sababu za kifo kuidanganya akili yako kuwa wewe upo salama na hicho kifo sababu hupitii aliyopitia marehemu.
 
Tumepoteza watu Wenye CV za kidunia

Tumebakiwa na Waigizaji watupu waliojibatiza kuwa wao ni chawa

Nikitoka hapa Kituo cha Kupigia KURA naelekea Kanisani direct

Ahsanteni sana

Yuko wapi Lucas Mwashambwa? 🐼
Nchi imekuwa ya madondocha , ccm hawapendi sikia mtu anayejitambua , wametengeza machawa , hali ni mbaya lakin Mungu yupo kazini
 
Back
Top Bottom