Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Mbunge wa Kigamboni na Naibu Waziri wa Afya wa zamani Dkt. Faustine Ndugulile, ameshinda uchaguzi wa kiti cha Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani Kanda ya Afrika.
Katika Uchaguzi uliofanyika leo jijini Brazzaville nchini Congo, wajumbe 25 kati ya 46 wa Mkutano Mkuu wa 74 wa WHO uliofanyika leo wamemchagua Ndugulile na hivyo kuwashinda wagombea wengine kutoka Niger na Senegal.
Tayari Ndugulile ameeleza wazi kuwa vipaumbele vyake ni kuhakikisha Watu wanapata haki ya kupata huduma bora za afya, kuboresha utayari wa nchi za Afrika katika kukabiliana na majanga ya magonjwa ya mlipuko, kuimarisha uwajibikaji ndani ya WHO kanda ya Afrika pamoja na kuimarisha mawasiliano baina ya nchi wanachama katika masuala ya Afya.
Soma Pia: Kama Dkt. Ndugulile atateuliwa kuwa Mkurugenzi wa WHO (Afrika) basi Komredi Makonda atakuwa na Nafasi ya kugombea Ubunge Kigamboni