Dkt. Hassan Abassi: Agizo la Rais Samia kufungulia vyombo vya habari linahusu televisheni za mitandaoni pekee

Mkuu huyu Abass hana kibri sana, hamsikilizi mama kwa ufasaha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haya masalia yanazidi kuonesha yalivyokuwa tatizo, yaani Rais kutolea mfano wa blogs na yeye uwezo wake wa kufikiri ukaishia hapo hapo.

Halafu kilaza kama huyu ndio alikuwa na vyeo viwili, katibu mkuu wa wizara ya habari, na msemaji wa serikali.
 
Dr Abbas, Mh SSH atakuaibisha soon
 
Huyu afukuzwe hafai kabisa anampangia kazi Rais. Halafu yeye sii Waziri wa Habari na wala sio msemaji wa serikali ana kiburi sana huyu. Mama umeshaanza kudharauliwa. Masikini

Serikali inafanya kazi kwa maandishi lazima atakuwa amepewa maelekezo kuwa ni tv za mitandaoni ndio maana kasema atawajuza kama kuna maelekezo mengine
 
Huyu Jamaa ni nini kinampa kiburi? Maana Rais ashaongea.Mhe.Rais kama anaona na ana wasaidizi wake humu ndani watu kama Dr.Abbas watakuharibia Mapema kabisa ilhali Hotuba zako zinaeleza kila kitu .Sasa KWA kauli kama hizi za Mteule wako mama.Watu wanachanganyikiwa.Huyu Abasi muonye Mapema Mama.Tunakupenda ila kauli za huyu jamaa zitakuharibia,Na Watu watakosa Imani Tena na Tanzania Mpya ya Uhuru wa Vyombo vya Habari
 
Kama Dr. Abbas anasubiri maelekezo kuhusu kufungulia magazeti na kwakuzingatia kwamba Rais kasema vyombo vifuate sheria, nategemea kesho vyombo vyote vilivyopotosha umma kuhusu maelekezo ya Rais ( kwa Tafsiri ya Abbas) vielekezwe kurekebisha taarifa zao nakuomba radhi au kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria. Akiwa ni mtendaji Mkuu wa Wizara na kabla waziri mwenye dhamana ajaingilia kati anapaswa kuonyesha msimamo wake unawagusa wale ambao kwa Tafsiri yake wamekiuka sheria ili kuondoa upotoshaji.

Tusubiri kuona hatua zitakazochukuliwa kwa wale waliotafsiriwa kumnukuu vibaya Mhe Rais.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…