Dr Akili
JF-Expert Member
- Aug 21, 2011
- 5,119
- 4,569
Alichokisema rais ndicho hicho. Kila mtu alisikia hivyo. Kwa kuwa kwa kawaida serikali huendeshwa kwa maandishi au nyaraka na kwa sababu rais katika hotuba ile alitaja tu vi online tv vidogo vidogo vilivyokuwa vimefungiwa, Dr Abbas yuko sahihi. Kama rais aliimanisha na magazeti yaliyokuwa yamefungiwa Dr Abbas atapaswa kwanza kumuuliza Katibu Mkuu Kiongozi ili kupata uhakika. Halafu kwani ni magazeti yapi yalifungiwa? Si ni lile la Mbowe (Tanzania Daima), la Kubenea (Mwanahalisi) na lile la Tundu Lissu (jina nimelisahau) tu? Haya hata yakiruhusiwa wamiliki wake hawana uwezo tena wa kifedha kuyaendesha.Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Dkt. Hassan Abassi amesema agizo la kufungulia vyombo vya habari lililotolewa na Rais Samia Suluhu linahusu televisheni za mtandaoni pekee na siyo pamoja na magazeti.
Amesema endapo kukiwa na maagizo mengine yanayohusu magazeti, atatekeleza.
---
Huyu ni kichwa ngumu bado amelala, tunaomba mama yetu umuache huyu mtu aendelee kulala, hakufai.
Amelipuuza agizo lako...anajifanya mjuaji...anakujua sana kuliko unavyojielewa...