Dkt. Hassan Abassi: Agizo la Rais Samia kufungulia vyombo vya habari linahusu televisheni za mitandaoni pekee

Sijaelewa huyu daktari ameyasema hayo kwa nafasi ipi inayompa jukwaa la kusema hayo.
Katibu mkuu wa wizara ya habari ndiye boss wa mkurugenzi wa habari. Greson Msigwa ni mkurugenzi kwenye wizara ya habari chini ya Dr Abbasi ambaye ndiye katibu mkuu wa wizara hiyo. Kuwa msemaji wa tasisi hakufanyi kuwa ndiyo mkuu wa tasisi hiyo na hakuwaondolei wakuu wa tasisi husika kuwa wasemaji wa tasisi zao. Unafanya kwa niaba yao.
 
Post ya Dk. Abbas apewe Greson Msigwa - Msigwa fits the bill yuko well organised anajiamini na anajua kijieleza. Sio hawa wanao pewa kazi halafu wanasubiri maelekezo ya zaida kutoka kwa Rais nini cha kufanya - he goes "mimi sijapewa maelekezo" what a laughable comment! !
 
Katika hotuba yake ni kweli alisema'' Fungulieni TV za mitandaoni''.
 
Dr Hassan Abbas bado haamini kama 'Ukuta wa Berlin' uliokuwa ukiwatenganisha Wajeruman umeanguka
 
“Wizara ya Habari, nasikia kuna Vyombo vya Habari mmevifungia* sijui Viji- TV vya mikononi vile, vifungulieni lakini wafuate sheria na miongozo ya Serikali, tusiwape mdomo wa kusema tunabinya Uhuru wa Vyombo vya Habari, tusifungie tu kibabe”-Rais Samia Suluhu Hassan
 
Kimsingi hana adabu, yeye binafsi anapata faida gani kufungia vyombo vya habari, kwa kuwa taifa linapata fedheha mbele ya jumhuia ya kimataifa, Rais ameagiza kuvifingulia vyombo vya habari, pia ameagiza makosa na adhabu ziwe wazi, sio kosa huyu analiona yule alioni adhabu haijulikani, akae afikiri vizuri!
 
Mama amesisitiza watumie akili. Ninachokiona hapa huyu Dkt Hassan ameshindwa kutumia akili, na badala yake anaendelea kutumia misuli.

Tumuachie mama mwenyewe ampe kadi ya njano.
 
Kajitoa ufahamu na kuja na tafsiri zake mwenyewe...

Mama ameshawaambia wasipopaelewa wamuulize...
 
Mkuu, Gerson Msigwa ndiye aliyepaswa kutoa taarifa hii kwa kuwa tayari amepewa post mojawapo aliyokuwa anaishika huyu bwana Abass (Ukurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Usemaji wa Serikali), lakini ni kama hajakubali kuiacha nafasi hiyo, ameamua kufanya majukumu ya msaidizi wake na ndio katoa boko kama hivyo. Bado hajakubali kilichotokea na kinachoendelea kutokea
 
Sawa kabisa mkuu, ila Mwenye Mamlaka ya kufungia magazeti ni Waziri wa Habari. Huyu bwana Abass kwa aliyoyasema na hata kwa jinsi ulivyoeleza kuwa ni Mkuu wa Taasisi huoni kama amepoka/amepora mamlaka ya Waziri wa Habari? Yaani yeye Katibu Mkuu ndie amejivika mamlaka ya kufungulia vyombo vilivyofungwa wakati barua zake za kufungia (wakati akiwa ni Msemaji wa Serikali) zilieleza kuwa aliyefanya hivyo ni Waziri wa habari.


 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…