Dkt. Janabi na Wanaharakati wa Afya tuache upotoshaji. Nchi ina tatizo kubwa la Utapiamlo na sio uzito wala unene

Bahati mbaya hatujafika level ya kula kupitiliza. Hicho cha kula kupitiliza hakipo kwa familia nyingi
Mpango wa afya sasa hivi unajikita kwenye kuzuia zaidi kuliko kutibu. Magonjwa yasiyoambukiza ndio yanaongoza kwa vifo Tanzania na nchi nyingine kusini mwa Jangwa la Sahara kwa hiyo elimu inahitajika sana zaidi ya hiyo inayotolewa na Prof. Janabi.

Wewe unafikiri kwa sasa Shinikizo la damu na Kisukari zinawapata matajiri tu. Sasa hivi masikini kibao wanaugua Kisukari na Shinikizo la damu na wengi wanakufa mapema kwa kukosa matibabu.

Malnutrition/ utapiamlo umegawanyika mara mbili kuna undernutrition and Overnutrition (Obesity) sasa wewe unataka umlazimishe Dr. Janabi aongelee kitu ambacho sio alichoboea,yeye ni mbobezi kwenye magonjwa hasa moyo na figo ambayo husababishwa kwa kiasi kikubwa na mtindo wa maisha usiofaa.
 
Angalau leo umekuja na thread ya maana. Tatizo ni siasa. Vyuo vikuu vyetu vyote vimekalia mambo ya uchawa badala ya kufanya research za vitu kama hivi. Huwezi kuwaambia watu wapunguze sukari bila kuwa na data wanakula kiasi gani kwa siku. Tanzania mambo ya mafuta, sukari n.k. ni anasa na viongozi ndiyo wenye access navyo kwa wingi. Vijijini watu wanakunywa kikombe kimoja cha chai ya rangi wataathirika wapi na sukari?
 
Angalau leo umekuja na akili kwenye kusoma thread yangu.
 
Tatizo ni kuwatisha watu. Ukila vyakula vya wanga uko hatarini kufa kwa magonjwa ya moyo na figo. Upuuzo mtupu. Hana tofauti na wale Manabii Uchwara wanaowatisha Waumini wao kuwa 90% ya nguo zinazouzwa Duniani zimezalishwa kwenye viwanda vya ma freemason.
 

Mkuu, hoja yako ya msingi ungeiweka kuwa unashauri Wizara ya Afya izidishe zaidi nguvu kukabiliana na changamoto ya Utapiamlo. Ukiweka hoja yako kusisitiza tuzidishe elimu kwa umma na jitihada nyingine za kukabiliana na Utapiamlo nitamuunga mkono.

Upande mwingine unatakiwa kueleweshwa kuwa tatizo la Unene Uliopitiliza limeendelea kuongeza kwa takribani miaka 15 sasa. Utaratibu wa maisha ya Watanzania wengi na shughuli wanazofanya hivi sasa ni tofauti na miaka 15 iliyopita. Hivi sasa ongezeko kubwa la wananchi wanajikuta katika tabia-bwete na ulaji usiofaa kwa sababu mbalimbali. Sayansi inasema hii huongeza uwezekano wa kuwa na Unene Uliokithiri na hatimaye huweza kupelekea ongezeko la Magonjwa Yasiyoambukiza.

Uwekezaji kwenye Sekta ya Afya hatuangalii eneo moja na kuacha mengine. Njia nzuri ni kuhakikisha kuwa tunakabiliana na changamoto A wakati tukiendelea na changamoto B huku tukiendelea pia na changamoto C n.k. Mathalani, hatuwezi kusema tusifanye jitihada za kukabiliana na Anemia Seli Mundu (Sickle Cell Anaemia) kwa kuwa wenye Sickle Cell Anaemia ni wachache na tukasema tushughulike pekee na Maambukizi ya Njia ya Mkojo (UTI) ambayo yapo kwa sehemu kubwa n.k. n.k.

Ni muhimu kuimarisha jitihada za kukabiliana na changamoto za Sekta ya Afya kwa ujumla wake na kuziangalia kila changamoto kwa umuhimu wake.

Mfano mwingine, kuna watu kwa maisha wanayoishi hatutarajii wavunjike mguu/mkono kwa kuumia wakiwa wanaendesha bodaboda au kama abiria na kunufaika na uwekezaji wa huduma za dharura au kulazwa MOI hospitali LAKINI wao wanaweza wakawa ni candidates wa kuhitaji huduma za Kinga na matibabu ya ugonjwa kama Saratani ziimarishwe ili kuwanufaisha.
 
Nadhani hujamuelewa Prof. au wewe unamchukia tu yeye anazungumzia magonjwa yasioambukizwa na sababu zake.
Ni vema na wewe ukaja na Magonjwa ya utapiamlo na sababu zake alafu kila mgonjwa amfuate mshauri anayemfaa. Mf. Wewe au Jirani yako apo ana shida ya Figo na kisukari kweli utampuuza Janabi eti kisa watoto huko Iringa wana utapiamlo.
 

Profesa Janabi anaongea anachojua Kwa sababu yupo kwenye medical field, anaona jinsi magonjwa yanayotokana na lishe mbovu yanavyotesa Watanzania wengi na kuwa mzigo wa Serikali kwenye matibabu.


Nashangaa sana mtoa mada anapinga kitu gani?!
 
Maelezo yako ni mazuri lakini hayajibu ujinga unaofanywa na watu wachache kuhalalisha ukosefu wa sukari. Hili la kusema watu wachukuwe fursa ya ukosefu wa sukari kupambana na utumiaji wa sukari uliopitiliza ni kejeli mbaya sana kwa wananchi wa Tanzania kutoka kwa watu walioshiba mpaka wakavimbiwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…