Dkt. Janabi na Wanaharakati wa Afya tuache upotoshaji. Nchi ina tatizo kubwa la Utapiamlo na sio uzito wala unene

Mimi hapo alipoongelea suala la sukari na kulihusisha na afya ndio kanichosha na nimemdharau na pia pale aliposema eti mwananchi anashindwa kulipia matibabu lakini anakuja na V8 jamani nchi ina shida nyingi hii imagine watu tunaowaamini wamefita ujinga wanaongea ujinga
 
Finland imechagua rais mpya hata hajaapishwa. Alikuwa hana gari na alikuwa nasafiria economy class kwenye ndege. Akishaapishwa anapewa gari mbili za serikali na atayokuwa anaitumia ina miaka 11 tangu inunuliwe. Hii nchi huwa inaipa Tanzania yetu misaada, nchi ambayo hata mkuu wa mkoa huwa anasafiriri kwa business class.
 
Huyu daktari hata kama ana hoja ila anavyoziwasilisha ni kama vile Tanzania yote ni ya vibopa.
 
Hongera sana Ndug, leo umeshusha Nondo....πŸ€žπŸ‘πŸ‘
 
Naunga mkono hoja..

Prof. Janabi anatoa elimu nzuri kwa walengwa, na siyo kila mtu anaweza kuwa mlengwa wa kila jambo.

Hawa wapingaji wa Dr Janabi bila shaka watakuwa ambao wanaona Prof anaingilia maslahi yao, mfano wauzaji wa:-
β€’ madawa za tiba mbadala
β€’ chips
β€’ energy drinks, soda
β€’ majeneza
β€’ sembe, sukari, nk..

Kama unaona anachoongea Prof hakikuhusu si unaacha kusikiliza tu huku ukijua kuna wanaopenda?!
 
Kumbe tatizo kubwa sio utapiamlo bali ni Wataalam wasiokuwa na ujasiri wa kusema ukweli. Utadhani wanatoka sayari ya mbali na hawana macho. Huyo Mheshimiwa ameshasahau ule msemo wa kisayansi usemao " kama huna takwimu kaa kimya usiongee".
 
Mi nashangaa sana, utasikia msile ugali, wali wala ngano vina sukari nyingi, kuleni matunda!!!! Samli ndio ilishapigwa marukuku kabisa, wakati 70% ya waamerica ndio wanayatumia, eti mtakufa na presha
 
Profesa Janabi anaongea anachojua Kwa sababu yupo kwenye medical field, anaona jinsi magonjwa yanayotokana na lishe mbovu yanavyotesa Watanzania wengi na kuwa mzigo wa Serikali kwenye matibabu.

Nashangaa sana mtoa mada anapinga kitu gani?!
Ukiangalia wastaafu wengi ni wahanga wa magonjwa yasiyoambukiza, kama kisukari, presha, kupooza viungo, nk.
Haya ni magonjwa ambayo hayaanzi ghafla kama mafua. Yanatokana na tabia za ulaji wa vyakula na vinywaji visivyofaa kwa muda mrefu, yaani miaka kadhaa.

Pia siku hizi kuna baadhi ya watoto huzaliwa wakiwa na kisukari tayari kutokana na lishe mbovu ya wazazi.

Watalaamu wabobezi kama Prof Janabi wanatoa elimu kwa nia njema ili watu wajue, wajihadhari kwa manufaa yao, watu wengine wanakuja na kejeli za kijinga.

Tatizo watu huwa wanataka wajifunze baada ya kuwa wagonjwa, siyo kabla ili kujihami. Utasikia, siku fulani kuna clinic ya wagonjwa fulani, wanaenda wanafundishwa kama darasani kwanza halafu wanapewa dawa za kupunguza maumivu tu, maana kupona haiwezekani.

Kama unadhani unajua si kaa kimya tu wengine wajifunze?
 
Mi nashangaa sana, utasikia msile ugali, wali wala ngano vina sukari nyingi, kuleni matunda!!!! Samli ndio ilishapigwa marukuku kabisa, wakati 70% ya waamerica ndio wanayatumia, eti mtakufa na presha
Umesema kweli broo. Watu wanadanganyana Mitandaoni, kwenye vijarida uchwara, makongamano/Semina za upigaji halafu wanashabikia wasichokijua. Eti ule matunda e.g. malimao au mapera halafu ukalale. Kesho unalalamika vidonda vya tumbo.
 
Kwahio watu wanaokula vizuri mfano Ulaya na Japan, hawafi kwa sukari Wala presha? Wao vifo vyao vinatokana na nini? Mwili wa binadamu ni Kama mazao ya musimu mfano mahindi, hata ukiendelea kupalilia na kuweka mbolea baada ya miezi sita yatakauka na kufa, uhai umefika mwisho
 
Siiafiki hoja yako kwa sababu utakaaje kimya huku ndugu zako wakidangaywa mchana kweupe? Mtu kuwa daktari kwa Taaluma haimaanishi anajua vyote.
Wengi wa wataalam wetu wanajua vizuri upande wa Maandiko tena hawajayaandika wao. Wao wamekariri tu. Lakini Uhalisia katika Field ni finyu sana. Wanajua kidogo tu hususan vyakula vyetu vya asili na madawa ya asili.Kwa mfano hata ukiangalia Tv (e.g. ITV -kipindi cha mapishi) utakona ni makaangizo kwa kwenda mbele. Hutasikia matumizi ya magadi, Samli, Ulaji wa miwa n.k. Vitu vingi ni vya Viwandani. Tunasahau Watu walikwepo toka zamani na walikula hivyo vyakula wanavyovihafifisha au kuvidunisha.
Samahani kama nimewakwaza Health & Nutritionist professionals.
 
Naunga hoja mkono, kuna kipindi flan niliwahi kumskia wazir wa afya akisisitiza juu ya kuongeza virutubisho kwenye vyakula

Sasa mpaka wazir wa afya amezungumza maneno hayo ni baada ya kuona asilimia kubwa ya watanzania afya no mgogoro kutokana na lishe mbovu
 
Yani sijui anatuchuliaje binafsi huwa nampuuza sana maana ye anajiona ni bora zaidi ya binadamu wenzie πŸ˜•πŸ˜
Ona/Tazama: Anakula vizuri, analala pazuri bila kero, usafiri binafsi au wa Serikali (Vieiti) akishindwa sanasana ndo usafiri wa Public. Usimtajie habari za bodaboda au Bajaji. Sasa kwanini asijione bora zaidi ya wenzie? Hajaifahamu wala haijui rangi halisi ya Tanzania huku mitaani.
 
Lakini kama mwanadamu bado hajamaliza hapaswi kudharau mtu

Akae kwa kutulia...nobody is perfect
 
LEO UMEONGEA POINT SANA. JANABI AMESHAKUWA MSANII NA ANATAKA MU TREND KAMA AKINA MWIJAKI TU. SIKU HIZI NIMEONA HANA JIPYA. ANAACHA MATATIZO YA MSINGI ANASHIKILIA VITU AMBAVYO SI MATATIZO KWA TAIFA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…