Dkt. John Pima aliyekuwa DED Arusha na wenzake wahukumiwa kifungo cha miaka 20 jela

Dkt. John Pima aliyekuwa DED Arusha na wenzake wahukumiwa kifungo cha miaka 20 jela

Kuna wakili mmoja msomi ,anaitwa magafu

Hiyo kesi ilipofikia apewe yeye ,kwenye rufani hua ananifurahisha Sana ,sabaya anajua habari gake
 
Mzee wa Kino ni kwamba huyo jamaa alikuwa kwenye inner circle ya JPM. Kiburi chake sio poa. Kwa Afrika lazima utawala mpya unapoingia madarakani ishughulikie baadhi ya watu. Hata Gambo bungeni harudi. Yule Gambo alishawahi waweka ndani watu waliokuwa wamejichanga kwenda kupeleka rambirambi kwenye msiba wa watoto wa Lucky Vicent. Aliweka utaratibu kuwa rambirambi zote zipitie kwake. Na katika aliowatia ndani kwa sasa baadhi ni vigogo wa awamu ya 6.
Duh ,visasi

Ova
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imewahukumu aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha, Dk John Pima na wenzake wawili kifungo cha miaka 20 jela baada ya kukutwa na makosa ya uhujumu uchumi.

Hukumu hiyo imetolewa leo Alhamisi Agost 31, 2023 na Hakimu Seraphin Nsana, katika kesi namba 5/2023 ya uhujumu uchumi, iliyokuwa inawakabili Dk. Pima, aliyekuwa Mweka Hazina wa jiji la Arusha, Mariam Mshana na aliyekuwa Mkuu wa Idara ya Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji, Innocent Maduhu.

Akisoma hukumu hiyo ya kesi namba 5/2023, mbele ya mahakama hiyo, Hakima Nsana amesema kuwa baada ya kupitia ushahidi wa pande zote mbili, mahakama imewatia hatiani washtakiwa katika kesi ya uhujumu uchumi iliyokuwa inawakabili.

"Kwa kuzingatia maombi ya mawakili wa upande wa washtakiwa, ikiwemo kutokuwa na rekodi ya makosa ya nyuma, utegemezi wa familia na ushirikiano mlioutoa katika kipindi chote cha uendeshaji wa kesi hii, mahakama inawapa adhabu ya kutumikia miaka 20 jela huku miezi 14 mliokuwa kizuizini ukizingatiwa," amesema

Mbali na hilo, washtakiwa wana haki na nafasi ya kukata rufaa katika Mahakama Kuu endapo hawajaridhika na hukumu hiyo.

Mwananchi
Hawa jamaa huenda hiyo pesa walikua wanakula wenyewe tu.
Mbona wenzao wanakwiba kila siku tena pesa ndefu mara 30 ya hiyo ya kwao na hawashitakiwi wala nini,?
 
Ingekuwa China risasi zingewahusu.
na ingekuwa Marekani restitution ingewahusu

restitution ya Marekani ukiiba dola mbili utalipa dola mbili, na kifungo kiko pale pale, very sensible crime deterance strategy

hawataki mtu aibe kwa ku test zali, yani ukikamatwa unalipa unaachiwa (Magufuli style), matajiri wanakuwa hawakai jela

na hawataki mtu aibe kimkakati, unavumilia kifungo ukitoka jela unaenda kwenye chimbo lako ulikoficha mabilioni maisha yanaendelea....

.... Marekani hela utaitema.... wanajua kukaza hukumu kuhakikisha kama hela huna unakufa masikini.... huku kwetu huyo Mkurugenzi mwaka kesho utamwona anadunda kwenye V8 VX
 
Raha ni China tu, wangeshakula shaba hao, na ukoo wao mzima kufilisiwa, mpaka marafiki zao wote wanafilisiwa.

Utakuwaje na urafiki na fisadi kama wewe si fisadi?
 
Haya mambo ya uhujumu uchumi si walisema hayatakuwepo tena baada ya Magu kufa..mbona bado yanaendelea sasa?
Hayatakuwepo Tena kwa maana kwamba wezi wa kiiba wasipelekwe Mahakamani au kwa maana ipi uliyo nayo wewe?
 
Raha ni China tu, wangeshakula shaba hao, na ukoo wao mzima kufilisiwa, mpaka marafiki zao wote wanafilisiwa.

Utakuwaje na urafiki na fisadi kama wewe si fisadi?
Nchi yako wenyewe kila mtu wezi huko

Ova
 
Back
Top Bottom