Dkt. John Pima aliyekuwa DED Arusha na wenzake wahukumiwa kifungo cha miaka 20 jela

Dkt. John Pima aliyekuwa DED Arusha na wenzake wahukumiwa kifungo cha miaka 20 jela

Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imewahukumu aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha, Dk John Pima na wenzake wawili kifungo cha miaka 20 jela baada ya kukutwa na makosa ya uhujumu uchumi.

Hukumu hiyo imetolewa leo Alhamisi Agost 31, 2023 na Hakimu Seraphin Nsana, katika kesi namba 5/2023 ya uhujumu uchumi, iliyokuwa inawakabili Dk. Pima, aliyekuwa Mweka Hazina wa jiji la Arusha, Mariam Mshana na aliyekuwa Mkuu wa Idara ya Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji, Innocent Maduhu.

Akisoma hukumu hiyo ya kesi namba 5/2023, mbele ya mahakama hiyo, Hakima Nsana amesema kuwa baada ya kupitia ushahidi wa pande zote mbili, mahakama imewatia hatiani washtakiwa katika kesi ya uhujumu uchumi iliyokuwa inawakabili.

"Kwa kuzingatia maombi ya mawakili wa upande wa washtakiwa, ikiwemo kutokuwa na rekodi ya makosa ya nyuma, utegemezi wa familia na ushirikiano mlioutoa katika kipindi chote cha uendeshaji wa kesi hii, mahakama inawapa adhabu ya kutumikia miaka 20 jela huku miezi 14 mliokuwa kizuizini ukizingatiwa," amesema

Mbali na hilo, washtakiwa wana haki na nafasi ya kukata rufaa katika Mahakama Kuu endapo hawajaridhika na hukumu hiyo.

Mwananchi
Watakata rufaa watakuwa free
 
Jambazi SABAYA pamoja na kukiri Makosa kwa DPP yupo huru
 
Huyu jamaa alikuwa ana jiamini sana wakati wa mwenda zake. Kuwatishia watumishi wenzake kwamba ni mtu wa system na hakuna wa kumgusa. Hata Rc hakuwa na mamlaka juu yake. Akimwambia yeye ana ripoti Ikulu direct.
Wakati wa uchaguzi akampora Lema ushindi wake.
Huyu Mungu kweli halali wala hasinzii. Upandacho ndicho utakacho vuna.
 
1693502772996.png

Kada wa CCM Dkt. John Sima akutwa na hatia na kuhukumiwa kwenda jela kwa ufisadi.

Elimu :
Dr. John Marco Pima

Coventry University

Doctor of Philosophy (Ph.D.)Computer Science​

2013 - 2017

Coventry University

MScSOFTWARE DEVELOPMENT​

2009 - 2010
Activities and Societies: Member of Bad Designs and Systems Test Member of PTN UK Member of Source Market Team Member of Tanzania Students Association-UK

Graduate at IAA 2006 in Information Technology.

Registered Technical Teacher by NACTE Tanzania
Founder Secretary General and Director of Positive Thinkers Network of Tanzania

Kutoka maktaba :
1693502879238.png
 
Duh

Basi walimuamulia

Pole yake

Ova
Mzee wa Kino ni kwamba huyo jamaa alikuwa kwenye inner circle ya JPM. Kiburi chake sio poa. Kwa Afrika lazima utawala mpya unapoingia madarakani ishughulikie baadhi ya watu. Hata Gambo bungeni harudi. Yule Gambo alishawahi waweka ndani watu waliokuwa wamejichanga kwenda kupeleka rambirambi kwenye msiba wa watoto wa Lucky Vicent. Aliweka utaratibu kuwa rambirambi zote zipitie kwake. Na katika aliowatia ndani kwa sasa baadhi ni vigogo wa awamu ya 6.
 
Hukumu hizi pia zingekuwa zinatoka kwa mawaziri wezi, makatibu wakuu wezi, MaRC wezi nk na hata MaRais wezi bila shaka Taifa lingekuwa mbali sana kiuchumi.

Mahakama zenyewe zingebaki tupu bila watendaji na wananchi mtaani tungeisha maana waTz udokozi upo kwenye damu!
 
Mwendazake crews, internal Auditors walitishiwa sana na huyu jamaa
Kwamba mwendazake ndio alikuwa anawalinda waibe hizo pesa..? Umejiuliza bizo hela zimepigwa enzi za huyu dhaifu au dikteta wa maendeleo?
 
Back
Top Bottom